Simba kuweni makini na drones wakati wa mazoezi yenu Casablanca

SAYVILLE

JF-Expert Member
Joined
Mar 25, 2010
Posts
7,895
Reaction score
12,975
Nawapongeza Simba kwa kwenda mapema huko Casablanca kuzoea hali ya hewa hasa ya majira ya jioni ila faida hiyo ya kwenda mapema ina hasara zake. Ningeweza kupendekeza mazoezi yangefanyikia hata Tunisia ambako hali ya hewa haitofautiani sana na ya Morocco halafu Simba waingie Casablanca siku moja kabla.

Toka game ya kwanza, kama sikosei Simba wamefanya mazoezi siku moja tu Dar es Salaam kabla hawajafanya safari ya Morocco. Kwa maana hiyo drill zote za mpango kazi wa mechi ya marudiano zitafanyikia huko huko Morocco.

Morocco ni nchi iliyoendelea sana katika nyanja nyingi na mpira wao wanauendesha kisasa mno. Inawezekana moja ya mbinu ambazo Wydad wamekuwa wanatumia ni kurekodi mazoezi ya timu pinzani wakiwa katika ardhi yao na baadae wanaenda kufanya analysis kujua mnajipangaje kwa mechi.

Mbadala wa hii changamoto ni kwa Simba kutumia zaidi chaki na ubao na kufanya drills za mbinu kwa kiwango kidogo sana maana kutofanya kabisa ni jambo lisilowezekana. Ikiwezekana drills za mbinu za mchezo fanyeni uwanjani usiku maana commercial drones hazirekodi video katika giza, mazoezi ya asubuhi yawe ya viungo au yale basic tu na si mbinu za mchezo.

Hizi drones zimewalaza sana Waarabu chini ya vifusi ila na wenyewe wameamka na kuzitumia kwa faida yao.
 
Nyie ata mfanye mazoezi usiku wa manane kama uwezo ni mdogo ni mdogo tu akuna kitachobadilika hapo
 
mtamuua mgonjwa kila mtu anakuja na dawa yake
Cha kushangaza siku hizi Simba na Yanga zinapendelea kucheza mechi zao usiku ila hazifanyia kabisa mazoezi usiku. Hata zikienda nje na mechi ni usiku sikumbuki kuziona zikifanya mazoezi muda huo wakati inabidi wafanye hivyo kuzoea hali ya hewa ya muda huo.
 
Sidhani kama wanaweza kuhangaika na hayo wakati tayari first leg imeshachezwa,na sioni kama Simba watacheza tofauti sana na walivyocheza dsm
Mbinu za timu zote mechi ya pili itakuwa tofauti sana na mechi ya kwanza. Na kila timu itakuwa inabadili mbinu kulingana na mbinu inayotumiwa na mpinzani wake wakati mechi inaendelea.
 
Yes mwarabu anaweza fungika ila hii mbinu ya kujitahidi kuzuia drone kwenye anga ya mazoezi Ya Simba ni ngumu sana kwa sababu utazuia drone na wakati zishafungwa hidden camera.

Mi nadhani jambo la muhimu ni nyie kuharibu mipango ya mwarabu hasa kwa sababu nyie ndio mna advantage kwakua mnaongoza
 
Back
Top Bottom