Simba kuweni makini na hiyo timu yenu, wekeni akiba ya maneno, ushindi dhidi ya Tabora, Singida fountain gate usiwafanye mkaona mko vizuri

Alaaa! Yaani unajisnitch mwenyewe. Kama unakiri mwenyewe kuwa Singida mpaka inakwenda kucheza na Simba ilikuwa imeshinda mechi zake zote mbili, haudhani hoja yako imefia hapo hapo? Kweli huko wenye utimamu wako wawili tu.

Halafu umeona mjumbe wenu wa bodi Zakayo Nchemba anavyotuvurugia ligi hadi unachanganya haujui timu ipi imecheza na Simba.
 
Usikurupuke Kama umeshikwa ugoni angalia alichoandika mwenzako na ndicho nilichomjibu usitake Tumaini Rage na msemo wake ebho!
 
Mapovu yanakutoka kisa Simba anaanza mechi tatu mfululizo Dar nyie mmesahau kipindi Cha zahera mnatembeza makopo mechi zote za duru ya kwanza mlicheza Dar.
Halafu Kama Simba kaanza na timu dhaifu si furaha kwenu maana akija kucheza na timu ngumu atapoteza point.
Mechibili mmeshaanza kulalamika.
 
Kwa hiyo ukitaka baada ya ushindi mashabiki walie?. Kazana Mkuu bado kidogo utaanza KUPAA🤣
 
Ila ukiwa yanga kweli unakuwa kituko kipindi simba anacheza champions league yanga walilamika kwa nn simba ina viporo ila sasa hivi yanga ina viporo viwili simba hawalalamiki ila yanga ndio wameanza kulalamika baada ya kushindwa kwenye sakata la kagoma na aweso na wachezaji wote wa ndani iliotaka kuwasajili simba yanga acheni kulalamika chezeni mpira mmeshinda NBC premier league misimu mitatu kwa raisi huyo huyo mliyekuwa mnasema anawaonea na ni simba siku mkikosa ubingwa naona mtaenda ikulu kama mlivyotaka kufanya awali.
 
Reactions: BRN
Nimekubali mashabiki wa simba tunaongea sana, mafanikio walionayo yanga misimu ya hivi karibuni ingekuwa ni simba kuna watu wasingekunywa maji, hapo ni michezo 2 tu ya ligi kuu lakini tambo zake km wamefika fainali ya club bingwa, ovyo kabisa
 
Mwanzo wa ligi mlishasema simba ni timu mbovu. Ila bado mnaiongelea, unaiongeleaje timu mbovu? Iacheni simba mbovu icheze.
Iongeleeni yanga timu bora duniani kwa sasa.
Kuna uwezekano nimeanza kuwa shabiki wa simba kabla hujazaliwa, usinipangie cha kuandika
 
Hamna timu mle.
 
Nimekubali mashabiki wa simba tunaongea sana, mafanikio walionayo yanga misimu ya hivi karibuni ingekuwa ni simba kuna watu wasingekunywa maji, hapo ni michezo 2 tu ya ligi kuu lakini tambo zake km wamefika fainali ya club bingwa, ovyo kabisa
Yanga wanaokunywa Hadi supu ya vibudu?. Ulishawahi kuona timu gani imeweka mabango ya magoli?. Hakuna timu ya wastaarabu na wasomi kama Simba.
 
Waacheni nao wafurahi. Maana muda wa kumkataa Mangungu ukifika, furaha yote itayeyuka kama barafu iyeyukavyo kwenye joto.
 
Raha ya goli lishangiliwe likiwa bado la moto moto, sio unasubiri hadi mechi imalizike ndio uanze kushangilia magoli
 
Vital O nao nealicheza wachezaji 9
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…