Habari ya asubuhi wana Simba. Nina mawili ya kusema:
- Hivi ni kweli Simba imepokonywa bus na wale wawekezaji? Kama ni kweli hii ni aibu kubwa kwa timu kubwa kama Simba kukosa bus la mil 200. Hebu imagine unamkataba na Azam, unamtangaza MO kwenye jezi za Simba, una mkataba na M-bet wa 26B. Mechi tu ya Simba vs Yanga mgao wake unatosha kununua bus lake kabisa bila kutumia mtu. Viongozi liangalieni hilo.
- Kama MO anataka kutoka Simba,. Viongozi wakijipanga Simba inaweza kujiendesha kupitia wawekezaji wengine kumuweka mtu mwekezaji kwenye jezi pale mbele ni hela ya maana. Simba ni kubwa, itabaki kuwa Simba hata kama MO anaondoka.