Simba mlichowafanyia biashara sio poa

technically

JF-Expert Member
Joined
Jul 3, 2016
Posts
12,706
Reaction score
52,355
Mmefanikiwa kuwahujumu wasisafiri kwenda Libya kisa waliwabana mkatoka droo.

Mna ushaidi gani yanga alitoa pesa kwamba Simba afungwe na biashara?

Kwa kuwatumia watu wa kushughulikia vibari mmechomeka rushwa ili wakwamishe vibari vya kusafiri?

Mtu wa Kwanza aliyeihujumu Biashara Ni Rais wa TFF ambaye Ni Simba damu.

Yaani inakuwaje mlezi wa timu zote anakuwa na chuki kwa timu iliyopiga hatua hivi.

Nina ushaidi wa kutosha kwamba Rais wa TFF pamoja na viongozi wandamizi wa Simba na baadhi wa serikali wameihujumu biashara ili isisafiri kisa ilitoa droo na Simba.

Kwa syle hi soka letu litasubiri Sana ikiwa timu zinahujumiwa na viongozi wa mpira.

Takukuru na Serikali naomba ichunguze sakata hili Kuna hujuma kubwa imefanywa na Simba ili kuwakomoa biashara.
 
"Nina ushaidi wa kutosha kwamba Rais wa TFF pamoja na viongozi wandamizi wa Simba na baadhi wa serikali wameihujumu" uko wapi sasa mbona sio kitu kinachoweza ku back up unachosema.

Anyway maji masafi yamepungua bei kwa lita, kwahiyo jitahidi sana upate ya kutosha yana msaada katika nyakati kama hizi
 
Mmefanikiwa kuwahujumu wasisafiri kwenda Libya kisa waliwabana mkatoka droo.

Mna ushaidi gani yanga alitoa pesa kwamba Simba afungwe na biashara?....
Acha Kimbelembele....Hao Biashara Wenyewe Ukiwauliza karibu Siku 10 Zimepita toka mmalize Mechi Yenu ya Tz, nini Kimewasibu mkashindwa Kukata tiketi ili Msafiri Mapema?

Hawana majibu...! Wewe hicho Kihoro Umekitoa Wapi?

Vita Ya Mpira Asìkwambie Mtu..ni Uwanjani tu.
 
Nimefurahi Biashara United kutolewa kwa ukata.

Simba tulijitahidi kuwawezesha kimataifa hata shukrani hawakutoa.

Walipaswa kutupigia makofi siku ya mechi nao.

Kitendo cha kukamia kutuumizia wachezaji wetu kimewagharimu.

Malipo ni hapa hapa.
 
Kwa Uyanga wangu ninazidi kuwakumbusha mashabiki na wanachama wenzangu tumthamini sana GSM....hata wale wa Simba pia wamthamini sana MO DEWJI....

Furaha yetu mashabiki ni kuona BURUDANI ya mpira tu.....

#DaimaMbeleNyumaMwiko
#1935ForEver
 
Wee jamaa kumbe sometime akili zako ni za hovyo hivyo? Huo ushahidi ulionao kwa nini usiuweke kwenye andiko lako?

Unasema hakuna ushahidi kuwa "
Mna ushaidi gani yanga alitoa pesa kwamba Simba afungwe na biashara?

Halafu unasema pia "Nina ushaidi wa kutosha kwamba Rais wa TFF pamoja na viongozi wandamizi wa Simba na baadhi wa serikali wameihujumu biashara ili isisafiri kisa ilitoa droo na Simba.

Sasa ili tuende sawa na isiwe kuwa hii ni porojo na kwamba akili zako siyo za hovyo, anika wazi huo ushahidi ulionao ili hatua stahili zichukuliwe!

Lakini pia nikuulize, Biashara ilikwama kusafiri kuelekea Djibouti mara mbili mfululizo kwenye hatua ya awali ilipocheza na FC Dikhil hali iliyoilazimu kuchelewa kusafiri siku ya mechi baada ya jitihada kufanyika na ukumbuke ilikuwa ni kabla ya kucheza na Simba, je hapo napo ilikuwa inahujumiwa na Simba pamoja na viongozi wa TFF?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…