SAGAI GALGANO
JF-Expert Member
- Nov 13, 2009
- 47,706
- 69,281
Hawa hapaSasa kwenye huu uzi nani anamuongelea mwingine?
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Hawa hapaSasa kwenye huu uzi nani anamuongelea mwingine?
Kuna nduguzo Nalia Ngwena,Demigod na Laban Og kwa siku kila mmoja anaanzisha threads zaidi ya 5 kuihusu Simba huwaonei huruma hawa? Hapa wana Simba wakianizsha thread zinahusu club,viongozi na wachezaji wao kuwakosoa ili Simba ifanye vizuri.Ni ajabu na kweli mashabiki na wanachama wa simba pamoja na viongozi wao wamebaki kuiongelea yanga muda wote na kusahau kabisa ya kuwa wanaitaji kuijenga timu yao ambayo imetoka kapa misimu 2 mfululizo,
Wamesahau kuwa wanaowasema wanaendelea na wataendelea kubeba makombe na kuvaa medali kwa kuwa wanao viongozi bora na makini wanaofanyya mipango yao bila presha ya aina yoyote ile,
Wanasahau wenzao wametuliza vichwa kuwashusha wachezaji wakubwa aina ya wakina makabi lilepo kutoka Al hilal na wao wamekimbilia kusainisha mchezaji kutoka ligi dhaifu ya Rwanda, kwa mwenye kumbukumbu nadhani anamkumbuka michael sarpong aliyesajiliwa na yanga kutoka ligi ya Rwanda,alisajiliwa akiwa top scorer na magoli yake 17 na asist 5 but alipofika bongo kila mwenye kumbu kumbu anajua alichokifanya!
Kwa miaka ya karibuni ligi ya Rwanda imeshuka sana akuna ushindani wa kusema unaweza kumjenga mchezaji kukabiliana na ligi ngumu ya Tanzania na ata kuwa msaada kwenye mechi za kimataifa!
Kwa maana iyo bado kauli za wakina Try again na wenzake kuwa inakuja simba mpya yenye nguvu zinaendelea kudhihirisha msamiati wa mzee Rage!
Ni muda sahihi kwenu kupaza sauti na kuushauri uongozi wenu kuacha propaganda na sio kukomaa na mambo ya yanga ambao wameshawaacha mbali kwa kuwa na timu bora, viongozi bora na mafanikio ya kupigiwa mfano wanayo, wanachokifanya wenzenu kwa sasa ni kuboresha kikosi kwenye mapungufu na sio kujenga kikosi mlijue hilo!
Kama nyumba yako inaungua alafu unakimbilia kuzima moto kwa jirani yako utakuwa na utindio wa ubongo!
Upo sahihi mkuuuWatu wajinga hupenda attention tu ndo maana anahisi uto wanaongelewa na wanachama wa mnyama.