Simba na Kocha wao Fadlu Davis wapigwa faini ya milioni 7

Simba na Kocha wao Fadlu Davis wapigwa faini ya milioni 7

Mkalukungone Mwamba

JF-Expert Member
Joined
Aug 29, 2022
Posts
3,141
Reaction score
7,205
Klabu ya Simba imeadhibiwa kwa kutozwa faini ya Sh. 5,000,000 (milioni tano) kwa kosa la mashabiki wake kurusha chupa za maji uwanjani wakati wa mchezo tajwa hapo juu kwenye uwanja wa KMC Complex Mei 28, 2025.

Adhabu hii ni kwa mujibu wa kanuni ya 47:1 ya Ligi Kuu kuhusu Udhibiti wa Klabu.
Kocha wa klabu ya Simba, Fadlu Davis
ametozwa faini ya Sh. 2,000,000 (milioni mbili) kwa kosa la kuishutumu Bodi ya Ligi Kuu Tanzania kuwa ina ajenda tofauti kuhusiana na ratiba ya michezo ya klabu hiyo kwenye Ligi Kuu ya NBC. Fadlu alizungumza hayo alipokuwa anafanya mahojiano na Azam TV baada ya kumalizika kwa mchezo tajwa hapo juu, akionyesha kutoridhishwa na ratiba ya michezo ya Ligi ya klabu yake.

Adhabu hiyo ni kwa mujibu wa Kanuni ya 45:2(2.9) ya Ligi Kuu kuhusu Udhibiti kwa Makocha.

snapins-ai_3647665552156505508.jpeg
 
Kocha Mkuu wa Klabu ya Simba, Fadlu Davids, amepigwa faini ya Sh2 milioni na Bodi ya Ligi Kuu Tanzania kwa kosa la kutoa kauli zenye kuipotosha jamii kuhusu ratiba ya michezo ya klabu yake katika Ligi Kuu ya NBC.

Kwa mujibu wa taarifa rasmi ya Bodi ya Ligi, Fadlu alitoa matamshi hayo wakati akifanya mahojiano na Azam TV mara baada ya kumalizika kwa mchezo kati ya Simba na KMC uliofanyika Mei 28, 2025, katika Uwanja wa KMC Complex.

Katika mahojiano hayo, Fadlu alidai kuwa kuna ajenda tofauti zinazohusiana na upangaji wa ratiba ya michezo ya klabu yake, akionyesha kutoridhishwa na namna ratiba ya Ligi ilivyopangwa.

IMG_5063.jpeg
 
Mashabiki wa simba wanaifilisi tu timu yao kwa kufanya mambo ya kitoto na yasiyo ya kiungwana. Sijui shida iko wapi!! Huwezi kusikia mashabiki wa Yanga wameng'oa viti au kuwatupia watu chupa za maji.
 
Fadlu alikuwa sahihi tatizo viongozi wa Simba wapowapo haiwezekani siku sita unacheza mechi tatu?
Ukifatilia Simba misimu mitatu inatolewa nusu fainali sababu ya ratiba.
 
Fadlu alikuwa sahihi tatizo viongozi wa Simba wapowapo haiwezekani siku sita unacheza mechi tatu?
Ukifatilia Simba misimu mitatu inatolewa nusu fainali sababu ya ratiba.
Acha kubwabwaja. Kila siku mnajinasibu na kikosi kipana leo mnalia lia kwa sababu ya ratiba? Mlipokuwa mnalimbikiza 'viporo' huku mkikenua meno hamkujua kwamba lazima mje mmalizane na viporo vyenu?

Kila ilipokuwa inafika mchezo wa kimataifa mnajikuta wa kishua mnaahirisha mechi kwa kisingizio cha safari halafu leo mnalialia nini?

Mlitaka mechi zenu ziishe mwezi wa saba?

Nikukumbushe tu... Kikanuni kikosi kinatuhusiwa kushuka dimbani kila baada ya masaa 72. Kama walishuka dimbani chini ya hapo mnayo haki kulalamika
 
Siku 6 ni masaa 144 gawanya na mechi 3 ni saa 48 Rudi darasani ukatoe ujinga nahisi mwalimu wako alipata shida Sana.
 
Mashabiki wa simba wanaifilisi tu timu yao kwa kufanya mambo ya kitoto na yasiyo ya kiungwana. Sijui shida iko wapi!! Huwezi kusikia mashabiki wa Yanga wameng'oa viti au kuwatupia watu chupa za maji.
Wee nae mbona huwa wanapata adhabu au kwa sbb ni mechi za zamani unajisahaulisha...
Mashabiki wenu wao ni hatuchezii hatuchezii...
Mpka huyo msemaji wenu juzi tuu akatandikwa faini ya milioni 5 kwa kuropoka ropoka hivyo
 
Umeshawahi kusikia mashabiki wa Yanga wameng'oa viti uwanjani, au kuwatupia waamuzi makopo ya maji?
 
Back
Top Bottom