Simba na Yanga zitaweza ushindani wa Afrika? Al Ahly imemuajiri kocha wa Mamelodi, Mosimane kwa mshahara wa Dola za Kimarekani 120,000 kwa mwezi

Kama ilibahatisha kufika robo mbona utopolo hambahatishi mmfike
Bahati inategemea na muda. Kwani Simba imeanza kushiriki michuano msimu wa 2018/2019 pekee? Si ilishashiriki michuano hiyo mara nyingi hapo kabla je kwanini miaka ya nyuma haikuweza kupata hiyo bahati? Ni sawa sawa na kwa Yanga kuna nyakati ilibahatika kufika mpaka hatua ya makundi ikawa mwisho wao hivyo ipo siku inaweza kubahatisha kufika hatua zaidi ya hiyo.

Kinachothibitisha Simba ilibahatisha ni namna walivyotolewa hatua ya awali kabisa. Yaani unapanda mpaka karibia ngazi ya mwisho halafu unaporomoka ghafla tu. Wakati aliyembeba ameenda hatua ya mbele yake zaidi. Au kunasababu ipi iliyopelekea Simba kutoweza kufika tena hatua Kama waliyofikia msimu wa nyuma yake?
 
Na nyie bahatisheni tuwaone tumewabeba mpaka mkashiriki halafu mnatuletea upotolo wenu
Hamkuibeba Yanga bali mliibeba nchi kwa ujumla. Mafanikio ya klabu kimataifa hainufaishi timu moja bali huinufaisha nchi yao na timu yenyewe husika pia inapata mafanikio. Timu za Italy, Germany, England zinapata nafasi ya kuingiza timu nne kwenye champions league na timu mbili kwenye Europa kwasababu ya performance ya klabu zao kwenye michuano ya kimataifa (Uefa na Europa league) na huwezi kusikia kauli ya kusema timu fulani imebebwa.
 
simba ndiyo wanao haribu mpira wa nchi hii, yaani wao ni ujanja ujanja tuu, kununua marefa na tim pinzani, wakienda kimataifa wabutuliwa 5 bila, next season wanarudi wananunua mechi zao zote wanainunua na tff wanachukua tena ubingwa, wkienda kimataifa wanatolewa na kitim cha msumbiji, mwisho wa siku wanaivuruga adi tim ya taifa inafungwa na Lesotho na Burundi...…...........kazi kweli kweli,
 
Mkuu embu jaribu kuongea kimpira zaidi, jaribu kuweka ushabiki pembeni. Kwa aina ya wachezaji aliyonao Simba, pamoja na aina ya mpira anaocheza Simba, kwa Africa Mashariki hakuna timu inaweza kuifikia. Pamoja na madai uliyoleta yanayojawa na hisia zetu za kishabiki pasipo na uthibitisho, lakini ukiangalia namna timu inavyocheza unaona kabisa utofauti na timu zingine.
Umasikini mbaya Sana mkuu inaleta hali ya wivu, maana kila unayemuona kafanikiwa unamuona Kama vile kafanikiwa kwa ndumba au wizi wakati wewe kapuku. Tukubali kuzidiwa tujifunze kujitafakari sisi Kama sisi mapungufu yetu ili kufikia mafanikio kama wenzetu. Uswahili hauendeshi timu bali pesa na mifumo mzuri ndio unaoleta mafanikio kwenye mpira.
 
Umeongea ukweli mkuu.
Kwa mfano uwe na uongozi kama ule wa Yanga ambao Mwenyekiti wake anajiona yeye ndiye kocha na wakati huohuo ndiye mkurugenzi wa ufundi na pia ndiye Mwenyekiti wa Klabu, hata ukiwa kocha kama Klopp atashindwa tu
 
Hahaha.. ripoti yako inaangusha hadhi ya Ahly... huwezi fananisha AHLY na na timu yeyote hapa EA (afrika mashariki)
Tumeaminishwa kuwa KOCHA ndiyo mshindi...NO.. big NO mpira ni wale vijana 11 (wahezaji) !!
Na hao 11 lazima waujue mchezo w kandanda !!
Pole sana.... tuendeleee
 
Usipende kuharibu mazungumzo yamsingi kwa vitu vya kipuuzi
 
Muwe mnatumia akili. Unamleta huyo kocha kwa kushiriki ligi ambayo mshindi anapata milion 100 we utakuwa na akili kweli? Mambo mengine huhitaji kusoma sana kuyaelewa.
 
Majina ya watu na taasisi lazima yaanze na herufi kubwa. Acha dharau!
 
Tafuta historia ya Simba kwenye mashindano ya CAF, kumbe hujui lolote kuhusu Simba
 
Simba waliibeba nchi sawa.. Yanga akiwa nchi gani?
 
Na wewe utopolo tulikununua tulipokupiga 4
 
Tafuta historia ya Simba kwenye mashindano ya CAF, kumbe hujui lolote kuhusu Simba
Historia haiwezi kubadili uhalisia ya kutokubahatisha. Kwasababu kwa kila unapofikia hatua fulani, misimu inayofuata haufikii pale ulipoishia bali unaishia pa mwanzoni tu. Hiyo ni kubahatisha, ungekuwa umefika kwa malengo basi hayo hayo malengo yangekufanya upitilize pale ulipoishia au sio mbaya ukagotea pale pale ulipoishia mwanzoni.
 
Basi msifike hatua za juu (robo/nusu/au fainali) ili muikomoe Yanga. Kama mnaona mnufaika ni Yanga pekee.
KIMATAIFA hakuna kubwa mlilowahi kufanya kuwazidi Simba.. (kubali, kataa)

Ushindani wa YANGA NA SIMBA hao wengine usiwaweke sababu wanatambua mchango wa mkubwa wa Simba CAF, na ndio maana walitoa shukrani zao kwa mnyama.
 
Ndio maana hukuwahi kusikia kombe moja limebebwa na timu mbili.

Habari za kubahatisha mbona Azam fc na uwekezaji wote hajawahi kufanya lolote?

Simba amewahi kucheza fainal Shirikikisho CAF.., VIPI YANGA na hao unaowataja mnahistoria gani?
 
Kama sio bahati kwanini msimu uliofuata mkatoa hatua ya awali kabisa? Embu nipe sababu
We ulitaka nani atoke hiyo hatua..?
Mpira ni mistake ukikosea unaadhibiwa.. Ila haiondoi ubora wake nakusema ALIBAHATISHA
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…