"Simba nguvu moja." Tujadiliane namna ya kuwaua Waarabu na kuongoza Kundi D

"Simba nguvu moja." Tujadiliane namna ya kuwaua Waarabu na kuongoza Kundi D

huyu jamaa huwaga ni mburura sana aseeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeehhhhhhhh mkuu,na mods wameona kathread kakikolo ndio maana wamekiunganisha huku wameshamstukia huyu bichwabox kama ni empty set
Huyu kolo ni pimbi [emoji817], anaongea as if Mpira unachezwa kitandani badala ya uwanjani!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kama kawaida wa Kimaitaifa leo tumeshapangiwa group letu lenye timu kutoka Uarabuni moja na Congo moja.

Toa ushauri wako tufanyaje tuweze songa mbele katika hatua ya robo fainali na nusu na kisha kulichukua kombe zima tulilete Msimbazi

Karibuni wana SIMBA


Sent using Jamii Forums mobile app
Ongezeni nguvu back four na mpeni muda wa kucheza salamba maana Boko anawacheleweshea ushindi, japo mi Yanga ila nimeona nafasi nyingi kama leo pasi nzuri Boko alipewa za kufunga akapoteza.
Mashindano ya kimataifa nafasi ni chache sana,so zinahitaji mtu awe shapu sana kama Babu Kagere
 
Ongezeni nguvu back four na mpeni muda wa kucheza salamba maana Boko anawacheleweshea ushindi, japo mi Yanga ila nimeona nafasi nyingi kama leo pasi nzuri Boko alipewa za kufunga akapoteza.
Mashindano ya kimataifa nafasi ni chache sana,so zinahitaji mtu awe shapu sana kama Babu Kagere
Hapa umeacha mzaha na umekuwa mwenye busara na hekima.
Yanga daima mbele.
Simba ushindi daima


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ni Popoma / Mpumbavu tu ndiye atabisha na kujifanya anajitutumua kwa kusema kuwa Simba SC itafanya vizuri mbele ya Wapinzani wake katika Makundi Klabu Bingwa Afrika akina JS Saoura ya Algeria, AS Vita Club ya DRC na Al Ahly ya Misri ambalo Kwangu Mimi ndiyo naliona kama Kundi la Kifo ( au la Mauwaji kabisa )

Mtanisamehe wana Simba SC wenzangu najua ukweli wangu huu utakuwa mchungu Kwenu na utawaumeni mno ila mnivumilie tu na muupokee kama ambavyo huko nyuma nilikuwa nawapeni ukweli na matumaini katika mechi za ndani na hata ile ya Nkana Red Devil.

Hapa hatuna chetu tena kwa 100% ila nawaomba Simba SC waitumie hii michezo na hizo Timu kama sehemu ya Kuwatangaza vyema Wachezaji wetu ili basi waanze Kuonekana na Vilabu vikubwa ama vya Afrika hapa hapa au vile vya Ulaya kusudi tuwauze, tuingize Pesa na tusajili Wachezaji wapya wakubwa na wazuri.

Kwa sasa hivi hii Michuano tuichukulie kama sehemu yetu ya Kujifunza mambo mbalimbali na hasa kupata Uzoefu zaidi ili basi kama na Msimu huu tutabahatika Kuchukua Kombe la Ligi basi Michuano ijayo ya Klabu Bingwa tuingie huku tukiwa tumeshajikamilisha na kujiandaa kwa kila Kitu.

Tusidanganyane Simba SC ya sasa haina ubavu wa Kupambana na hizo Timu zote hapo juu hasa kutokana na sababu Kuu za Kiufundi. Kwa Simba SC ya Beki Pascal Serge Wawa, kwa Simba SC iliyokurupuka Kumsajili Beki Zana Coulibaly, kwa Simba SC yenye Kiungo kama James Kotei ambaye huwa anakata Upepo ( anaishiwa Pumzi ) haraka, kwa Simba SC ambayo ina Kipa Aishi Manula ambaye anafungwa aina ile ile ya Magoli ya Kizembe kabisa kama si ya Kitoto, kwa Simba SC ambayo Kipa wake wa akiba Deogratius Munishi ambaye hajielewi anafanya au anataka nini, kwa Simba SC ambayo ina Winga Shiza Kichuya ambaye Siku hizi Ushamba wote wa Morogoro umemtoka na Kumbi zote za Starehe za Dar anazijua, kwa Simba SC ya Mshambuliaji kama John Boko ambaye kama Mshambuliaji akikabwa tu njiani huwa hana Plan B na kwa Simba SC ambayo hadi hivi leo Kocha Patrick Aussems hana bado First Eleven yake na wala Msaidizi wake kamwe tusitegemee kufanya vyema katika Makundi.

Tunaoujua mpira vyema, Watoto wa mjini, Wazee wa Fitna na tuliocheza mpira kidogo hata kama huko Ligi Kuu hatukufika kwakuwa tulikuwa na Majukumu mengine ya Kimaisha na Kimtazamo kwa CAF kutupangia hizo Timu Nne ( 4 ) tusidanganyane wala kupeana Moyo ' Kingumbaru / Kijinga ' bali hapo ni rasmi Mbuzi ( SSC ) kafia kwa Wauza Supu Watatu mmoja wa Algeria ( Mwarabu ) , mwingine Mkongo na mwingine Mmisri ( Mwarabu )

Akili zetu sasa tuzielekeze mno katika Ligi Kuu ambayo nayo kwa jinsi ninavyoona kama tusipokuwa makini basi Yanga SC au Azam FC watachukua Kombe kwani Kimpira, Kimbinu, Kimkakati na hadi Kisaikolojia wapo vizuri sana kuliko Sisi Simba SC ambao muda mwingi tunakuwa tupo tu katika Presha na tusipotulia Msimu ujao kama kuna Kombe ambalo tutashiriki basi litakuwa ni la MBUZI MAPINDUZI CUP na UPUUZI SPORTS PESA CUP.

Yangu GENTAMYCINE ni hayo tu na mtanisamehe kwa wale ambao ukweli wangu huu utawaumiza ila muuchukue tu!

Nawasilisha.
Acha ujuaji bro simba ni team ngum na tunaenda kuonesha hilo



team yenye uhakika wa kupata zaid ya goli 3 kwenye game 1 unasema haifiki popote



kuna team ilipewa team zote za ukanda huu na mwarabu mchovu mmoja tena kwenye federation...lakin hii team ilikua kibonde kundi zima sijui angekua kapewa kundi letu angefanyaje...nahis angechangisha wanachama wake hadi wa huku kwetu umarila

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mungu zibariki timu za waarabu zisonge mbele kama kawa, SIMBA nawaombea mpigwe nyingi sana mrudi kuvuna pamba.
 
Back
Top Bottom