Simba SC 0-0 Young Africans SC | Ligi kuu NBC | Benjamin Mkapa

Lile goli halikuingia......? Mpira wenyewe nime angalia kwa kuchungulia tena nieanzaia dk 60,ila yote kwa yote kwa dk nilizo ziona Simba walikuwa bora, Yanga walikosa mechi fitness sijajua kipindi cha kwanza ilikuwaje.
Game Simba amezidiwa sema watu wanashangilia kwakuwa nafasi kubwa ya ushindi alipewa Yanga. Mtaani wanaofurahia SARE ni SIMBA na sio YANGA.
 
Sema refa kawapa utopolo sare wewe. Waamuzi ndio wameipa utopwinyo sara maana goli la halali limefungwa kabsa hali shida. Na filimbi ya ajabu hatukujua ya nn
Simba imebakia kwenye mitandao, pale hakuna timu.
 
Unajipa moyo tu ila kwa mpira huna cha ajabu umekimbizwa kama mtoto kipindi cha 2 ndo kdg umezinduka

Huyo Al ahly utamweza wap?
 
Nimeangalia mpira kwa umakini sana. Simba walikuwa wanapoteza mipira hovyo kuliko Yanga, hata kipindi cha pili Simba bado hawakufanya shambulizi lolote la maana golini kwa Yanga zaidi ya Shuti moja la Kanoute, nadhani watu wameona ameperform kisa tu kupiga shuti lile, ila katikati Simba hawakuwa vizuri na hata Kanuote amepoteza mipira mingi sana. Simba wamecheza rafu nyingi zaidi ya Yanga hii inaonesha ni jinsi gani walikuwa wanajihami dhidi ya mashambulizi.
Onyango amefanya kazi nzuri sana kwa kumdhibiti Mayele na sio INONGA.

Next game Simba isirudie makosa kuwaanzisha MORRISON, KIBU, DILUNGA NA KAGERE kwa pamoja, walikuwa mzigo mzito kwa viungo wakabaji wa Simba maana hawawezi kukaba pindi mpira unakuwa kwa YANGA.
Kwa ujumla mechi ilikuwa nzuri tena sana, refa kachezesha vizuri, makosa yaliyopo ni ya kibinadamu tu.
 
Mkuu unapokutana na mshindani wako ni muhimu sana kumshinda ili kutengeneza gap, Usitegemee wapinzani wengine wamshushe kama ww umeshindwa.

Maisha yamebadilika sana, sasa SIMBA inafurahia SARE.
 
Simba mwenyewe anajijua underdog ndo maana amefurahia draw
Tunawacheka tu kwa dharau, hakuna anaye shangilia draw, we are one of the giants wa soka la afrika nyie endeleeni na ligi yenu ya mchangani [emoji23]
 
Kwani kwenye ngao ya jamii alifungwa nani?

Saa nyingine ni kama kichwani hazikutoshi.
Tulifungwa sisi ila kwa kubahatishwa na ndio maana tulikua na uhakika kua mayele ni zari tu kama ilivyokua kwa balama mapinduzi naye mlimpa promo lakini yuko wapi saizi?

Hao ni wachezaji wa msimu saizi mtakua na mchezaji gani wa kutamba naye kwenye marudiano ya derby kwa kiwango hiki cha leo?
 
Sawa, unazungumziaje goli alilokosa mayele kipindi cha kwanza kwa kutaka kupiga ki star, mayele ni mzigo kwa yanga muda utaongea. [emoji23]
 
Acha kujifariji, ulichokiona pale ndo uwezo halisi wa yanga achana na maneno ya manara nyie bado sana [emoji23]
Kwa upande wangu matokeo yamekua kawaida sana,kwa maana hata haya pia niliyatarajia.

Kingine me sio shabiki 'oya oya',Kitu chochote anachoongeaga Manara huwaga nakichuja kwanza,Me huwaga sifati mkumbo.

All in all nakupa hongera mzee maana haya matokeo kwako ni favorite.
 
Game Simba amezidiwa sema watu wanashangilia kwakuwa nafasi kubwa ya ushindi alipewa Yanga. Mtaani wanaofurahia SARE ni SIMBA na sio YANGA.
Hakuna Simba anayefurahi sare, tulikuwa tunatamani muda usiishe tupate goli but Yanga mkaanza kupoteza
 
Hujaona mashambulizi ya Simba? Na hukuona hata ile Mwamnyeto akatoa mpira nje kidogo ajifunge
 
Kilichoongezeka yanga ni kelele tu, lakini kimpira bado sana.
 
Sawa, unazungumziaje goli alilokosa mayele kipindi cha kwanza kwa kutaka kupiga ki star, mayele ni mzigo kwa yanga muda utaongea. [emoji23]
Hahahahah binafsi nimehisi yule aliona kama ni offside, lkn pia mpira ulikatika tu, amejitahidi sana leo ila alikabwa mno.
Hata hivyo yule KIBU naye anahitaji mshauri mzuri ili utimamu wa akili uwe sawa, hayuko makini hata kidogo.
 
Hujaona mashambulizi ya Simba?na hukuona hata ile Mwamnyeto akatoa mpira nje kidogo ajifunge
Mkuu sasa kama hizo clearance mbona mabeki wa Simba wamefanya sana. Lile shambulizi kwako wewe?? Ushabiki wa ajabu sana huu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…