Kikosi changu cha leo
1Manula
2 Israel mwenda
3 zimbwe jr
4 Inonga Baka
5 Onyango Joash
6 Jonas mkude
7 Hassan Dilunga
8 Muzamiru Yassin
9 Madie kagere
10 Rally Bwalya
11Kibu Denis
Subs
Kakolanya, Kennedy, kapombe, Morrison, Boko, Banda, E nyoni, Sahko, Kanoute.
Marrison namuweka nje kama game changer wangu kutokana hali ya mchezo itakavyokuwa kipindi cha pili nikiangalia kati ya Dilunga na Kibu yupi anaufanisi mzuri ampishe Morrison lakini pia nitamtazama Bwalya kwa jicho la karibu ikiwa mechi itakuwa ngumu kwake na Yanga wanashambulia sana basi atatoka na nafasi yake Ataingia E nyoni kisha nitakuwa na viungo 3 katikati ya kiwanja yaani MUZAMIRU, E NYONI NA MKUDE wote hao wana uwezo mzuri sana wa kukaba hasa ukizingatia kwa upande wa Yanga watakuwa na watu wagumu sana katikati ya kiwanja yaani AUCHO, BANGALA NA FEISAL.
Kama Bwalya atatoka na kuingia Nyoni basi Kibu Denis atapanda juu kucheza 10 nyuma ya Kagere kisha 11 Ataingia Morrison nafasi ya Dilunga hapo itakuwa ni 4.4.2 Diamond yaani Kuna wakati timu ikiwa na mpira MUZAMIRU ama NYONI watapanda juu nyuma ya Kagere kama namba 10 huku KIBU DENIS kicheza kutokea pembeni kama kulia kama namba 7 hivyo basi nitakuwa na watu sita kwenye eneo la box la timu pinzani. Na timu ikipoteza mpira nitakuwa na watu wanne katikati ya kiwanja na wanne kwenye eneo la ulinzi na ikitokea shambulizi la kushitukiwa nitakuwa hatari zaidi sababu nitakuwa na KIBU NA MORRISON watu wenye kasi kubwa Huku juu yao Kuna mtu hatari KAGERE.
Wakati huo huo nje nitakuwa na Sadio Kanoute kama back up ikiwa Muzamiru ama mkude wakiumia.
Kwanini Onyanyo na Inonga wanaanza ni kwasababu ya mipira ya juu yaani cross, Kona na faulo ambazo Yanga wanaweza kuzitumia vizuri lakini pia Kuna Ntibazonkiza ambaye ni fundi sana kwenye mipira iliyo kufa hivyo nitawahitaji sana INONGA NA ONYANGO kucheza tena kwa kiwango chao Bora kabisaa.
Kwanini Morrison anaanzia bench ni kwasababu nataka kupima kwanza ufanisi wa Moloko ama Ntibazonkiza kwenye zile winga za kushoto na kulia kwasasa Morrison sio mwepesi wa kurudi nyuma haraka kukaba ikiwa timu haina mipira hivyo Zimbwe anaweza kuzidiwa sana lakini KIBU NA DILUNGA ni wazuri sana kwenye kukaba timu inapokuwa haina mpira hivyo basi Morrison nitamuhitaji kipindi cha pili wakati ambayo Yanga kasi yao imepungua tayari.
Naanza na Israel mwenda kwasababu ya kupungua kwa kasi ya kapombe kwa michezo ya hivi karibuni japo Mwenda sio mzuri sana kwenye kushambulia lakini atanipa uhakika wa kukaba lakini pia anaweza kufukia mashimo yanayoachwa na mabeki wa kati na pia ni mzuri sana hewani kuliko kapombe.
Binafsi nitaenda hivi.