Simba SC 0-0 Young Africans SC | Ligi kuu NBC | Benjamin Mkapa

Simba SC 0-0 Young Africans SC | Ligi kuu NBC | Benjamin Mkapa

Nachoomba leo mechi isiharibiwe na refa , matukio ya penati yawe ya foul za uhakika .
 
Dah! Nimecheka. Nchi hii tushakubali kutoendelea. Yaani mtu anakaa anawaza igonge saa sita kamili usiku aachie thread. Noma.
halaf wanailaumu serikali kwa umasikini, watu wanaingia uwanjani saa 3 asubuhi michi saa 11!
 
Uliza makolo wenzako amefunga free kick ngapi mpk sasa na sio kwenye hii ligi tu ila ni mpk kwa timu yake ya Taifa

Mkifanya makosa karibu na box tambueni hiyo ni goal la bure
Kwahyo yeye uchezaji wake ili afanye kuonekana ni mpk itokee faulo tenaa karib na goli ? Basi kumbe ni topolo tuu kama matopolo menzake.
 
Kikosi changu cha leo
1Manula
2 Israel mwenda
3 zimbwe jr
4 Inonga Baka
5 Onyango Joash
6 Jonas mkude
7 Hassan Dilunga
8 Muzamiru Yassin
9 Madie kagere
10 Rally Bwalya
11Kibu Denis

Subs
Kakolanya, Kennedy, kapombe, Morrison, Boko, Banda, E nyoni, Sahko, Kanoute.

Marrison namuweka nje kama game changer wangu kutokana hali ya mchezo itakavyokuwa kipindi cha pili nikiangalia kati ya Dilunga na Kibu yupi anaufanisi mzuri ampishe Morrison lakini pia nitamtazama Bwalya kwa jicho la karibu ikiwa mechi itakuwa ngumu kwake na Yanga wanashambulia sana basi atatoka na nafasi yake Ataingia E nyoni kisha nitakuwa na viungo 3 katikati ya kiwanja yaani MUZAMIRU, E NYONI NA MKUDE wote hao wana uwezo mzuri sana wa kukaba hasa ukizingatia kwa upande wa Yanga watakuwa na watu wagumu sana katikati ya kiwanja yaani AUCHO, BANGALA NA FEISAL.

Kama Bwalya atatoka na kuingia Nyoni basi Kibu Denis atapanda juu kucheza 10 nyuma ya Kagere kisha 11 Ataingia Morrison nafasi ya Dilunga hapo itakuwa ni 4.4.2 Diamond yaani Kuna wakati timu ikiwa na mpira MUZAMIRU ama NYONI watapanda juu nyuma ya Kagere kama namba 10 huku KIBU DENIS kicheza kutokea pembeni kulia kama namba 7 hivyo basi nitakuwa na watu sita kwenye eneo la box la timu pinzani. Na timu ikipoteza mpira nitakuwa na watu wanne katikati ya kiwanja na wanne kwenye eneo la ulinzi na ikitokea shambulizi la kushitukiza nitakuwa hatari zaidi sababu nitakuwa na KIBU NA MORRISON watu wenye kasi kubwa Huku juu yao Kuna mtu hatari KAGERE.

Wakati huo huo nje nitakuwa na Sadio Kanoute kama back up ikiwa Muzamiru ama mkude wakiumia.

Kwanini Onyanyo na Inonga wanaanza ni kwasababu ya mipira ya juu yaani cross, Kona na faulo ambazo Yanga wanaweza kuzitumia vizuri lakini pia Kuna Ntibazonkiza ambaye ni fundi sana kwenye mipira iliyo kufa hivyo nitawahitaji sana INONGA NA ONYANGO kucheza tena kwa kiwango chao Bora kabisaa.

Kwanini Morrison anaanzia bench ni kwasababu nataka kupima kwanza ufanisi wa Moloko ama Ntibazonkiza kwenye zile winga za kushoto na kulia kwasababu Morrison sio mwepesi wa kurudi nyuma haraka kukaba ikiwa timu haina mipira hivyo Zimbwe anaweza kuzidiwa sana lakini KIBU NA DILUNGA ni wazuri sana kwenye kukaba timu inapokuwa haina mpira hivyo basi Morrison nitamuhitaji kipindi cha pili wakati ambayo Yanga kasi yao imepungua tayari.

Naanza na Israel mwenda kwasababu ya kupungua kwa kasi na kiwango cha kapombe kwa michezo ya hivi karibuni japo Mwenda sio mzuri sana kwenye kushambulia lakini atanipa uhakika wa kukaba lakini pia anaweza kufukia mashimo yanayoachwa na mabeki wa kati na pia ni mzuri sana hewani kuliko kapombe.

Binafsi nitaenda hivi.
umeongea vyema asee inabidi tukuweke bench la ufundi
 
Nafikiria tu hapa

Kama morison hakufunga goli na akavua bukta akawaoneshea yanga chupi

Walahi leo huyu jamaa akifunga anaweza kuwaonyeshea ubo kabisa
 
Yan kwa mawazo hayo....Yanga tujiandae kuhama hii dunia leo
Nafikiria tu hapa

Kama morison hakufunga goli na akavua bukta akawaoneshea yanga chupi

Walahi leo huyu jamaa akifunga anaweza kuwaonyeshea ubo kabisa
 
Tatizo simba akishinda kelele zinakuwa nyingi sana kuanzia mtandaoni mpk mtaani ila Yanga akishinda ni kawaida tu na mitaa inakuwa imepoa
 
Back
Top Bottom