Simba Sc 1-0 RS Berkane | CAF Confederation Cup | Benjamin Mkapa Stadium

Simba Sc 1-0 RS Berkane | CAF Confederation Cup | Benjamin Mkapa Stadium

Tujifunze wapinzani wakija kwa MKAPA wanacheza open game...
Tofauti na timu zetu zikienda ugenini
Unaangalia mpira lakini? hiyo open game iko wapi?? Possesion 68 kwa 32[emoji23]
 
Leo ni sikukuu kwa wapenda kandanda nchini Tanzania.

Mnyama Mkubwa mwituni, Simba Sc atashuka katika dimba la Benjamin Mkapa kucheza dhidibya RS Berkane ya Morocco majira ya saa 10:00 jioni kwa saa za Afrika Mashariki.

Simba itaingia dimbani huku ikiwakaribisha nyota wake waliotoka majeruhi kama Chris Mugalu, Kibu Denis, Jonas Mkude, Tadeo Lwanga, Bwalya huku ikiwakosa Hassan Dilunga na Chama (ambaye sheria zinambana)

Simba itahitaji ushindi wa hali kwa mali ili kujiwekq katika nafasi nzuri ya kufuzu kwenda robo fainali ya michuano hiyo.

RS Berkane wakiwa ugenini wamekuwa na tabia ya kuruhusu magoli hivyo Simba ikitulia vizuri leo wanaweza wakavuna alama 3 muhimu.

Mechi ni saa 10:00 kupitia Utv ya Azam Tv.

Mijadala, updates na yote kuhusu mechi hii utapata dondoo kupitia uzi huu...karibuni sana

Simba nguvu moja!!
Simba ashinde ndilo la kuomba
 
Back
Top Bottom