Simba SC 3-0 JKT Tanzania FC | Uwanja wa Benjamin Mkapa | Vodacom Premier League VPL

Simba SC 3-0 JKT Tanzania FC | Uwanja wa Benjamin Mkapa | Vodacom Premier League VPL

Patashika ya Ligi Kuu, Vodacom Premier League VPL' kuvurumishwa leo Machi 1, 2021 ambapo Mnyama Mkali, Simba SC wanapambana na JKT Tanzania FC kwenye uwanja wa Benjamin Mkapa.

Mchezo huu inatarajiwa kuwa kali na wa kusisimua kwa muda wote wa dakika 90 huku kila timu ikiwania kusaka ushindi wa alama tatu muhimu ili kuweza kujiweka sawa kwenye msimamo wa VPL.

Kwenye mchezo uliofanyika 4, 10, 2020 JK Tanzania walilala kwa jumla ya mabao nne kwa bila. Je leo JKT Tanzania watakubali kuwa wateja kwa Mnyama Mkali kwa mara nyingine?

Usikose Ukasimuliwa.. Kumbuka mtanange huu ni kuanzia saa 1: 00 Usiku.
======

08' Chris Mugalu anaipatia Simba SC bao la kwanza, baada ya krosiiiiiiii kutoka kwa Miquissone

37' Luis Miquissone anaipatia Simba SC bao la pili akipokea pasi safi kutoka kwa Nyoni.

45+1

HT, VPL Simba SC 2-0 JKT Tanzania



View attachment 1714883View attachment 1714884
Embu malizia kwanza na "KULITAKA MWANA, KULIPEWA MWANA" ndo tuendelee.
 
Kapombe anakwendaa, doooh anaangushwa ndani ya 18 na refa hakuna kituuu
Ingekuwa kidimbwi FC, kesho ungesikia maandamano...

Juzi niliongea na wachezaji wetu, nikawaambia hawawezi kuunga mkono juhudi za vyura. Tukipewa penalti wapige nje... Nyie wote ni mashahidi wangu ... mliona Kagere alivyopiga nje... Wajinga wanadhani alikosa kumbe alikuwa anafuata maagizo kutoka juu...
 
Back
Top Bottom