Simba Sc 4-0 Us Gendarmerie | CAF Confederation Cup | Benjamin Mkapa Stadium

Simba Sc 4-0 Us Gendarmerie | CAF Confederation Cup | Benjamin Mkapa Stadium

Yule Adebayor mnayemtaka Mikia mbona simuoni au kwasababu aliwafunga tu...... mchezaji mkubwa ndiyo mechi zake hizi

Dk 27 nyau nyau
 
Wawakilishi wa Tanzania katika michuano ya CAF Confedaration Cup, Simba Sc itashuka dimbani dhidi ya Us Gendarmerie katika dimba la Benjamin Mkapa majira ya saa 4:00 usiku.

Hiyo itakuwa mechi ya mwisho ya kundi D na Simba wanahitaji ushindi wa aina yoyote ili waweze kufuzu hatua ya robo fainali.

Endapo Simba itashinda watafuzu kwa hatua ya robo fainali huku pia wakisikilizia matokeo ya Rs Berkane Vs Asec Mimosas mechi ambayo nayo itapigwa saa 4:00 usiku Kwa saa za Afrika ya Mashariki.

Hii itakuwa mara ya kwanza Simba kucheza mechi saa 4:00 usiku jambo ambalo linatia mashaka kama mashabiki watajitokeza kwa wingi kulinganisha na hali ya usalama.

Je Simba wataweza kufuzu robo fainali? Majibu ni saa 4:00 usiku kupitia ZBC2
Mbona umeutelekeza uzi wako hauuwekei updates?
 
Yule Adebayor mnayemtaka Mikia mbona simuoni,au kwasababu aliwafunga tu......mchezaji mkubwa ndiyo mechi zake hizi

Dk 27 nyau nyau
Ni wa kawaida tu ila akiwa kwenye team nzuri ni hatari zaidi, hii simba inavyocheza hii mechi laiti kama Adebayor angekuwa Simba Sc asingeacha kutupia.
 
Ni wa kawaida tu ila akiwa kwenye team nzuri ni hatari zaidi, hii simba inavyocheza hii mechi laiti kama Adebayor angekuwa Simba Sc asingeacha kutupia.
Kwanini timu zetu mpaka mchezaji azifunge ndiyo wanamuhitaji.......?? Scouting yetu ni ndogo sana
 
Bwalya anawachelewesha sana wenzie, yupo slow mpaka anapoteza mipira.
 
Berkane keshatangulia

Screenshot_2022-04-03-22-30-42.png
 
Back
Top Bottom