OKW BOBAN SUNZU
Platinum Member
- Aug 24, 2011
- 53,868
- 121,001
Lazima tukiri kuwa tumepata mpinzani mgumu kwenye hatua ya Robo Fainali, na pengine ni mpinzani mgumu zaidi tangu tuanze kushiriki hatua hii.
Hapa unamzungumzia bingwa mtetezi, unamzungumzia mshiriki wa Club World Cup, unazungumzia timu yenye wachezaji waliotoka Nusu Fainali ya Kombe la Dunia.
Huu ni mlima mrefu kwetu lakini hatuna budi kuupanda na kufika kileleni. Ili uwe mkubwa Afrika ni lazima uwafunge wakubwa wa bara hili.
Inawezekana sana Simba kupata ushindi dhidi ya Wydad kama tuu kila idara ndani ya taasisi yetu itatimiza wajibu wake kwa asilimia 100
Kama tulivyomvua Ubingwa Zamalek mwaka 2003 ni wakati sasa kumvua Ubingwa Wydad.
Let’s goo wana Lunyasi, Let’s goo wana Simba let’s wana Msimbazi mapambano yanaanza sasa. ☄️☄️
Credit Tajiri Mo Dewji
Credit Semaji la CAF
My Take
Wote tumeshuhudia nguvu ya mashabiki kwa Simba. Majamaa ya Al Ahl yalitisha uwanja ukatanda mpaka Al Hilal wamabaki kutetemeka tu. Ule moto wa derby ya Raja Vs Waydad ilikuwa hatari sana.
Huu ni wakati wa mashabiki kuingia bure, labda ibaki VIP A na B. Maandalizi yabaki namna ya kupiga vibe la kufa mtu pale Lupaso.
Simba Nguvu Moja