Simba SC imemtangaza Mshambuliaji Kivuli (False number nine) Willy Essomba Onana (23) Raia wa Cameroon kutokea Club ya Rayon Sports ya Rwanda

Simba SC imemtangaza Mshambuliaji Kivuli (False number nine) Willy Essomba Onana (23) Raia wa Cameroon kutokea Club ya Rayon Sports ya Rwanda

View attachment 2679212

Simba SC imekamilisha usajili wa Mshambuliaji Kivuli (False number nine) Willy Essomba Onana (23) Raia wa Cameroon kutokea Club ya Rayon Sports ya Rwanda.

Onana amesaini Mkataba wa miaka miwili kuitumikia Simba SC na ana uwezo wa kucheza namba zaidi ya tatu uwanjani, winga zote mbili na kucheza nyuma ya mshambuliaji namba 10.

Msimu uliopita Onana aliibuka mfungaji bora wa Ligi Kuu ya Rwanda akiwa na magoli 16 na assist 5 lakini ni Mshindi wa tuzo ya Mchezaji bora wa Msimu nchini Rwanda yaani MVP
Miaka 23, huyo kibabu? Ukisema 30 sawa
 
Kwa ufupi hakuna mchezaji mzuri west Africa akaja kucheza chini huku na hapa naongelea wote siongelei team moja ni team zote. mchezaji wa kiwango W.A haju huku ni simple tu, hao ni wachezaji wa kawaida tu kama tulionao tofauti majina yao na wanatumia profile ya nchi zao kuongeza thamani....
Naungana nawee kabisaa, kila nikimuangalia kipre Jr yaan ndo napata majibu sasa.
 
Nimejuliza hii kutambulisha mchezaji akiwa kavalia jezi ya msimu uliopita nafikiri ni bongo tu bado tuna safari ndefu..
By the way Onana ni mwamba sana.

Hahaha bongo ukitambulisha jezi mapema kabla ya sijui Simba Day au Wananchi Day, kuna wakali wa kuzifyatua kopi raiti halafu timu ikaingia hasara isiuze jezi OG kwa wingi...
 
Sidhani kwa wachezaji hao kama wataweza kuwasaidia kufika hata robo fainal ya caf baada ya kusajili wachezaji wenye experience kutoka alhaly au raja mnatoa wachezaji kweli ligi ambayo hata haijulikani soka letu kimataifa litabaki kuwa nyuma always kwa sababu ya ubahili na kusajili kwa kubahatisha kama mlivyobahatisha mickson
 
Simfahamu kiuchezaji, hivyo sitoweka neno angle hiyo.

Ninachoomba kujua, icho kibaba ni kweli kina miaka 23??
Mimi pia nilitaka kutia neno hapo kwenye kipengele cha umri. Hivi kweli hatujui kutofautisha kinda la miaka 23 na huyu kikongwe kweli jamani?
 
Haya mshambuliaji wa hela kubwa.Haya tutarudi baada ya mechi tano.
Screenshot_20230705_145422_Instagram.jpg
 
Hii ni mali aisee huyu ni ntu na nusu.

Alikua kapanda ngege anaenda kukipiga Liver viongozi wa Simba wakampigia simu rubani ndege akapiga uturn chuma kikatua bongo.

Mashabiki woyoooooo,,,chapa ilaleeee!
DP world bye,,,bye.
 
Haya mshambuliaji wa hela kubwa.Haya tutarudi baada ya mechi tano.
View attachment 2679252
$200k kwa huyu mchezaji? mbona kama wameongeza sifuri moja mbele hawa jamaa?[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]

mshahara $8k? mchezaji mwenyewe toka rwanda! ngoja msimu uanze mbivu na mbichi zitajulikana!
 
Hizo takwimu za mfungaji bora sijui mche,aji bora mmezitoa kwenye Ligi ya Sudan au? 😄

Screenshot_20230705-212520_Chrome.jpg
 
Wakati huo huo kuna timu jana imemtambulisha kibabage,mchezaji kistuli[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]dunia piga honiii nikwepeeeee
 
Hivi mtu kua na Miaka 23 anakuaje kwa mfano, tafuta nduguzo wenye 23 uwaone walivokomaa mkuu, hua tunalaumu Bure tu kumbe hata wengine hawadanganyi.
We muulize tu kwani mwapunyeto ana miaka 23 kweli???
 
Back
Top Bottom