Simba SC kwanini mnazubaa na kuwa wazembe hivi?

Simba SC kwanini mnazubaa na kuwa wazembe hivi?

Akina Zamoyoni huyo alikuwa hajazaliwa. Muulize Mrisho Ngasa hakucheza simba? Muulize anamjua athuman Chuji je hakucheza simba? Muulize anamjua kelvin yondani na je hakucheza simba? Muulize anamjua kaseja? Je hakucheza Yanga? Muulize anamjua boban na je hakucheza yanga?
Ongezea na Sanifu Lazaro
 
Ngoja nikufahamishe kama ulikuwa haujui

Management ya Yanga ilimfata Manzoki kutaka kumsajiri lakini Manzoki alikataa.

Alikataa kwasababu Club yake anayoipenda ni Simba, ni kama ilivyotokea owa Chama Yanga walipojaribu kumfuata.

Manzoki anaikibali Simba na ndio maana aliweka ahadi ya kuwa asipokuwa top scorer atarudisha pesa za usajili.

Na sasa watu tunafatilia ligi ya china, Manzoki mechi nne sasa hajacheza, hafurahii kuwa kule, ni muda tu unasubiriwa aje dirisha dogo.
We ulisikia wapi hayo mambo yaani mtu aache hela kisa mapenzi ya timu?
 
Ngoja nikufahamishe kama ulikuwa haujui

Management ya Yanga ilimfata Manzoki kutaka kumsajiri lakini Manzoki alikataa.

Alikataa kwasababu Club yake anayoipenda ni Simba, ni kama ilivyotokea owa Chama Yanga walipojaribu kumfuata.

Manzoki anaikibali Simba na ndio maana aliweka ahadi ya kuwa asipokuwa top scorer atarudisha pesa za usajili.

Na sasa watu tunafatilia ligi ya china, Manzoki mechi nne sasa hajacheza, hafurahii kuwa kule, ni muda tu unasubiriwa aje dirisha dogo.
Acha porojo wewe! Huyo Manzoki alikuambia hivyo, au na wewe umeshakuwa popoma kama mtoa mada?
 
Feisal anatakiwa na azam kwa mapesa mengi,unahisi ataenda azam??
Kwa nini asiende iwapo hao Azam wamefuata taratibu zote za kumsajili! Mbona Fei Toto huyo huyo alipotoka timu yake ya JKU kule Zanzibar ili kuja kutafuta malisho bora huku Bara, kituo cha kwanza kilikuwa ni Msimbazi!! (Na hii ni kwa mujibu wa mahojiano yake mwenyewe aliyofanya na Azam Tv)!!

Baada ya kushindwana na Simba kwenye maslahi, ndipo Singida United ya wakati huo ikamsajili! Na ndani ya muda mfupi, yalifanyika makubaliano; akasajiliwa Yanga, kama ilivyotokea kwa Habibu Kiyombo msimu huu, pale aliposajiliwa na simba kutoka Singida Big Stars.
 
Wewe una matatizo ya akili siyo bure, wachezaji wazawa ambao ni wapenzi wa kuzaliwa wa Simba na Yanga wameshacheza timu tofauti na anayoipenda.

Kwa uchache tu Zamoyoni Mogela alikwenda Yanga, na Thomas Kipese alicheza Yanga, hawa wote ni Simba damu.

Ukiandika ushuzi huu siku nyingine kwa watu wenye akili utachekwa. mazoki na Simba au Yanga wapi na wapi, hao wanatafuta pesa tu.

Mtu kama Chama akienda Yanga atacheza namba ya nani? Kama Aziz Ki anaanzia benchi mtu kama Chama si hata jezi atakuwa havai?
Mogela alienda yanga Kwa sababu baadhi ya viongozi wa Simba walimkataa na Wala sio sababu ya pesa.
Halafu nashangaa kusikia yanga wanamtaka Chama wakati wanaye feitoto na Aziz K ambao wamemzidi uwezo Chama.
 
hapo mwanzo kabla charismatic fela hajajulikana,nimecheka sana
IMG_20221206_121245.jpg
 
Wewe umekaririshwa eti, Nani kakwambia mbele ya pesa unatanguliza mapenzi? Uyo Manzoki unaemsema anaipenda Simba tu alizaliwa nayo? Mnaokoteza habari za udaku uko mitaani na propaganda za mitandaoni mnaleta hapa jukwaani, Sasa akisajiliwa yanga utasemaje labda kwa mfano, Eti yanga walimfata akakataa yani mashabiki wa umbumbuni mnalishwa matango pori na nyie mnaingia mazima matokeo yake akisajiliwa yanga ndio wengine mnaanza maandamano kumtaka babra ajiuzulu akiwauliza ni nani aliwaambia wanamsajili manzoki mnaleta reference za mitandaoni🤣🤣
Post nzima unajichekesha nashindwa hata nikujibu vipi
 
Wewe una matatizo ya akili siyo bure, wachezaji wazawa ambao ni wapenzi wa kuzaliwa wa Simba na Yanga wameshacheza timu tofauti na anayoipenda.

Kwa uchache tu Zamoyoni Mogela alikwenda Yanga, na Thomas Kipese alicheza Yanga, hawa wote ni Simba damu.

Ukiandika ushuzi huu siku nyingine kwa watu wenye akili utachekwa. mazoki na Simba au Yanga wapi na wapi, hao wanatafuta pesa tu.

Mtu kama Chama akienda Yanga atacheza namba ya nani? Kama Aziz Ki anaanzia benchi mtu kama Chama si hata jezi atakuwa havai?
Nilitaka nikujibu nikajua upo serious ila paragraph yako ya mwisho imeonesha post yako yote umeiandika kiutani
 
Back
Top Bottom