Simba SC kwanini mnazubaa na kuwa wazembe hivi?

Simba SC kwanini mnazubaa na kuwa wazembe hivi?

Akina Zamoyoni huyo alikuwa hajazaliwa. Muulize Mrisho Ngasa hakucheza simba? Muulize anamjua athuman Chuji je hakucheza simba? Muulize anamjua kelvin yondani na je hakucheza simba? Muulize anamjua kaseja? Je hakucheza Yanga? Muulize anamjua boban na je hakucheza yanga?
Zamoyoni sijui zaFigo hakusaidii chochote kujibu hoja yangu, wala swala la kutanguliana kuzaliwa sio issue hususani kwenye karne yenye ukuaji wa tehama ambayo hata mtoto wa miaka 9 anaweza kumprove wrong mzee wa miaka 60 kwenye habari ambayo inazungumzia tukio la miaka 30 iliyopita

Hao wachezaji uliowataja kama references ukiangalia wote hao hawakua kwenye competition ya kuwaniwa na hizo timu uliziozitaja, wengine hapo walitolewa kwa mikopo na timu zao kwenda kwenye timu zingine means mchezaji hakuwa na option
 
Cristiano Ronaldo pamoja na pesa aliyonayo hawezi cheza kwa mapenzi ijekua huku kwetu tunaopambana kujitoa kwenye umasikini! be serious please
Ulifatilia interview yake aliyoifanya juzi kati hapo mpaka kusababisha kuvunjiwa mkataba na Man?

Ulimsikia alivyokuwa akijibu hoja kuwa sio kweli kuwa hakuna timu ambayo inamtaka maana mpaka sasa amepokea offer za mikatab minono kutoka mataifa tofauti tofauti lakini amezikaa?

Wachezaji wangapi wamewahi kupewa deal za maana kwenda kucheza ligi za China huko lakini mwisho wa siku wakazipiga chini

Fabregas alipiga chini mkataba ambao alitakiwa kulipwa zaidi ya Euro 560K kwa wiki
 
Vikwazo, au mlishindwa kufikia dau lake la usajili? Stephano Aziz Kii mwenyewe mlishindwa kumsajili kutokana na ukata!
Manzoki mwenyewe alikuwa yuko tayari ila kwasababu mkataba ulikuwaumebakiza miezi michache kukamiliki so hakuwa na maamuzi akatuambia malizaneni na management, management ndio ikatufelisha kwa kututajia kiwango kikubwa cha pesa

Azizi Ki ilikuwa ni ishu ya pesa of course tulikuwa tukithaminisha pesa na kiwango cha mchezaji tunaona kabisa hesabu zinakataa
 
Ulifatilia interview yake aliyoifanya juzi kati hapo mpaka kusababisha kuvunjiwa mkataba na Man?

Ulimsikia alivyokuwa akijibu hoja kuwa sio kweli kuwa hakuna timu ambayo inamtaka maana mpaka sasa amepokea offer za mikatab minono kutoka mataifa tofauti tofauti lakini amezikaa?

Wachezaji wangapi wamewahi kupewa deal za maana kwenda kucheza ligi za China huko lakini mwisho wa siku wakazipiga chini

Fabregas alipiga chini mkataba ambao alitakiwa kulipwa zaidi ya Euro 560K kwa wiki
Angekataa ku sign China aende Simba sasa kwenye mapenzi yake
 
Yanga mnawasingia, wakumuhofia ni Yusuph Bakheresa msimu huu hana masihala upande wa usajili. Chama mkataba unaisha June 2023 anzeni naye mazungumzo, huyo Feisal nae yupo kwenye rada zake.
Chama alishawakataa tangu mwanzo, hawezi kwenda Uto labda Simba waachane naye awe free bila timu

Wachezaji wengi wa Uto wanacheza kwa kujituma ili kuishawishi management ya Simba iwasajiri

Kucheza Simba ni ndoto ya kila mchezaji wa Africa mashariki na kati
 
Ngoja nikufahamishe kama ulikuwa haujui

Management ya Yanga ilimfata Manzoki kutaka kumsajiri lakini Manzoki alikataa.

Alikataa kwasababu Club yake anayoipenda ni Simba, ni kama ilivyotokea kwa Chama Yanga walipojaribu kumfuata.

Manzoki anaikibali Simba na ndio maana aliweka ahadi ya kuwa asipokuwa top scorer atarudisha pesa za usajili.

Na sasa watu tunafatilia ligi ya China, Manzoki mechi nne sasa hajacheza, hafurahii kuwa kule, ni muda tu unasubiriwa aje dirisha dogo.
Eti Manzoki anaipenda simba🤣🤣🤣 hivi ulifikiria sawa sawa kabla ya kuandika hayo mashudu!!! Yaan mlishindwa hata kuvunja mkataba wake ili mumsajili alafu aje tu kijinga tu
 
Kama nilivyokuambia, management yake ndio iliyo fucked up na sasa huko aliko hana furaha. Dirisha dogo anatua msimbazi wait and see
Analipwa sh ngapi akose furaha? hio pesa mtampa nyie? Signing fee 200M mlikula kona jamaa wakaweka 900M sasa hivi value yake ni sh ngapi?
 
Bora shule zifunguliwe maana mna utoto sana kichwani.

Yaani mtu aache hela kisa anapenda timu fulani?
Manzoki ana akaunti feki nyingi sana twiter na instagram.. na simba walivyo mbumbumbu wanaamini kila kinachoandikwa na makolo wenzao wanaotafuta followers..
 
Ronaldo alikataa ofa ya kwenda kujiunga na Club ya uarabuni huko ambayo ilikuwa ni billions of money

Lakini alikuwa tayari aende kucheza Madrid hata kwa mkopo

Frank Libery alipewa ofa ya kujiunga na Chelsea kwa mkataba wa zaidi ya euro milion 64 lakini alikataa

Manzoki ye nani?

Hata Chama tu huyo naye si mlimtaka au umesahau? Chama aliwakataa sio kwasababu hamkutoa pesa anayoitaka, aliwakataa kwasababu mapenzi yake kwa Simba yana worth zaidi ya hiyo pesa ya vigodoro
Juzi chama aliulizwa akasema MAISHA HAYA, anaweza kucheza popote as long as pochi limenona.. acha umbumbumbu.. hawa wachezaji ni professional its difficult to let their heart rule their head
 
Chama alishawakataa tangu mwanzo, hawezi kwenda Uto labda Simba waachane naye awe free bila timu

Wachezaji wengi wa Uto wanacheza kwa kujituma ili kuishawishi management ya Simba iwasajiri

Kucheza Simba ni ndoto ya kila mchezaji wa Africa mashariki na kati
Kwa hiki ulichokiandika nimeng'amua tunajibishana na mtu wa aina gani, Yani wachezaji wawe na ndoto ya kwenda kucheza kwa wabwia unga na walozi? Uko sawa sawa kweli wewe kichwani? Akuna mchezaji mwenye akili timamu anayeweza kutoka Yanga kwenye maisha bomba eti aende kusajiliwa simba labda uyo awe ajielewi, Utoke kwenye timu inayoendeshwa kiuwazi uende kwenye timu inayoendeshwa kama timu za mitaani utakuwa una akili
 
Timu jezi zinauzwa duka moja kama zama za maduka ya ushirika[emoji1787].. juzi nimefuata jezi 300 za simba vunja bei sinza.. naambiwa zipo blue na white red hakuna nisubiri mpaka mzigo uingie wiki ijayo. Na hili swala limejirudia ni mwezi wa tatu sasa.. they are not serious..
 
Kama haujawahi kufanya biashara na wachina na kampuni za shipping inabidi utulie tu hujui wanaume tunakumbana na changamoto gani
 
Yaani mtu aache hela kisa anapenda timu fulani?
We ulisikia wapi hayo mambo yaani mtu aache hela kisa mapenzi ya timu?

Mbona Ngassa aliacha hela za El Merreikh, siku ambayo alitakiwa asaini mkataba akazima simu na kujificha ili aendelee kuitumikia klabu anayoipenda ya Yanga mwiko nyuma?

1670330260882.png
 
Chama alishawakataa tangu mwanzo, hawezi kwenda Uto labda Simba waachane naye awe free bila timu

Wachezaji wengi wa Uto wanacheza kwa kujituma ili kuishawishi management ya Simba iwasajiri

Kucheza Simba ni ndoto ya kila mchezaji wa Africa mashariki na kati
Ukita kupata kichekesho hiki ubonyeze namba ngapi.

Msijidanganye hamna mchezaji wa kutoka nje ,eatakaye acha kupenda fedha then apende Simba na Yanga hamna.

Huyo Manzoki unajipa moyo ,hela aliyopewa Manzoki na Wachina ,hawezi kuipata hapo Simba hata acheze kwa miaka kumi.

Nyie msimu huu hela hamna na mtaendelea kuchemka kwenye battle za kusajili wachezaji, yule Ndala wa Azam mlichemka sababu hela hamna,Sopu huyu ndie mmefanyiwa umafia na Yusuph, kamchomoa mchezaji kambini mbele ya viongozi wenu,nyie mlienda mikono mitupu mwanaume kaenda na kitabu chake cha cheki.
 
Back
Top Bottom