Kwa nini asiende iwapo hao Azam wamefuata taratibu zote za kumsajili! Mbona Fei Toto huyo huyo alipotoka timu yake ya JKU kule Zanzibar ili kuja kutafuta malisho bora huku Bara, kituo cha kwanza kilikuwa ni Msimbazi!! (Na hii ni kwa mujibu wa mahojiano yake mwenyewe aliyofanya na Azam Tv)!!
Baada ya kushindwana na Simba kwenye maslahi, ndipo Singida United ya wakati huo ikamsajili! Na ndani ya muda mfupi, yalifanyika makubaliano; akasajiliwa Yanga, kama ilivyotokea kwa Habibu Kiyombo msimu huu, pale aliposajiliwa na simba kutoka Singida Big Stars.