Kama ulikuwa unaniheshimu endelea kuniheshimu, heshima haiwezi kuvunjika kwa kutofautiana mitizamo.
Usinifanye niwe mtumwa wako wa kuandika kile unachokipenda wewe ili tu nikuridhishe kwa lengo la kuidumisha heshima yako kwangu
Maoni binafsi ambayo siyatoi kwa kum disrespect mtu hayawezi kuwa na indications ya kushusha heshima mbele ya rational thinker yeyote yule.
Pengine naweza nikafikiria kuwa busara sahihi kwa mtu anayekuheshimu ilikuwa sio kusema "kumbe nilikuwa nakuheshimu bure" (this sounds like ridiculous to me) bali busara ya kiuadilifu ilikuwa ni kukaa kimya
Unasema Africa mchezaji hawezi kuacha hela?
Hassan Bumbuli aliwahi kusema kuwa Yanga haiwezi kumsajiri Ibrahim Ajibu, kwakua aliondoka Yanga kutimkia Simba kwasababu yeye mwenyewe mchezaji alisema ana mapenzi na Club ya Simba, hafurahii kuchezea Yanga.
Hayo ni maneno aliyoyasema Bumbuli mwenyewe kipindi hicho bado ni Afisa habari
Huyo huyo Ajibu kama utakumbuka aliwahi kuitajika na Tp Mazembe, mkwanja kibao uliwekwa mezani huku Zahera akiwa ndio middle man lakini mwisho wa siku hakuenda Tp Mazembe akatimkia Simba ambako alipewa kandarasi ya miaka 2 akitanguliziwa M20. Na Zahera mpaka leo bado analaumu