Simba SC kwanini mnazubaa na kuwa wazembe hivi?

Ongezea na Sanifu Lazaro
 
We ulisikia wapi hayo mambo yaani mtu aache hela kisa mapenzi ya timu?
 
Acha porojo wewe! Huyo Manzoki alikuambia hivyo, au na wewe umeshakuwa popoma kama mtoa mada?
 
Feisal anatakiwa na azam kwa mapesa mengi,unahisi ataenda azam??
Kwa nini asiende iwapo hao Azam wamefuata taratibu zote za kumsajili! Mbona Fei Toto huyo huyo alipotoka timu yake ya JKU kule Zanzibar ili kuja kutafuta malisho bora huku Bara, kituo cha kwanza kilikuwa ni Msimbazi!! (Na hii ni kwa mujibu wa mahojiano yake mwenyewe aliyofanya na Azam Tv)!!

Baada ya kushindwana na Simba kwenye maslahi, ndipo Singida United ya wakati huo ikamsajili! Na ndani ya muda mfupi, yalifanyika makubaliano; akasajiliwa Yanga, kama ilivyotokea kwa Habibu Kiyombo msimu huu, pale aliposajiliwa na simba kutoka Singida Big Stars.
 
Mogela alienda yanga Kwa sababu baadhi ya viongozi wa Simba walimkataa na Wala sio sababu ya pesa.
Halafu nashangaa kusikia yanga wanamtaka Chama wakati wanaye feitoto na Aziz K ambao wamemzidi uwezo Chama.
 
Post nzima unajichekesha nashindwa hata nikujibu vipi
 
Nilitaka nikujibu nikajua upo serious ila paragraph yako ya mwisho imeonesha post yako yote umeiandika kiutani
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…