Simba SC 'mdhibitini' upesi sana Zackaria Hanspope na huu 'Uzushi' wake hukusu akina Chama, Miquissone na Bwalya atatuharibia

GENTAMYCINE

JF-Expert Member
Joined
Jul 13, 2013
Posts
60,660
Reaction score
121,325
Nimesikitika sana kama siyo mno Kumsikia leo mchana kupitia Kipindi cha Michezo cha Clouds FM Jumapili Mchana 'akiwashutumu' wazi wazi Wachezaji akina Clatous Chama, Luis Miquisonne na Larry Bwalwa kuwa Jana walicheza chini ya Kiwango na kwamba wanatakiwa 'Wahojiwe' kwani kuna uwezekano 'Wameihujumu' Klabu kwa 'Kuhongwa' na Yanga SC.

Nilikuwa sijui kuwa kumbe Mzee Hanspoppe ni 'mtupu' hivi Kichwani kwani ameshindwa tu kujua kuwa jana Chama amecheza akiwa na Majeraha ya Mechi ya Kagera Sugar, Luis Miquissone ndiyo aliyepiga Kona iliyozaa Goli lililotuokoa na 'Aibu' na Larry Bwalya jana ilikuwa ndiyo 'Derby' yake ya Kwanza hapa Tanzania.

Simba SC henu mfungeni 'Speed Governor' ya Mdomo huyu Hanspoppe kwani siyo 'Siri' ni 'Mvurugaji' na atatuharibia Klabu yetu. Amenikera sana.
 
analalamika bure,mechi ipi ya yanga chama amewahi onekana. huyu anatamba kwenye vitimu vidogo.

hao wengine mtatafuta sababu tu mara ndo derby ya kwanza kwani T.K,Mukoko, sarpong ni ya ngapi kwao hao wenu ni uwezo mdg wa mechi za kibwege bwege

yanga ahongi anakukimbiza kibabe sio kama mlivyo muhonga morrison mkashinda kibwege jana babu onyango anakamata miguu mnakataa sio penati mbumbumbu bwana
 
Naunga mkonyo ....japo yawezekana jana aliongea sababu ya gadhabu ya marefa....
 
Sasa kama unasema kuwa tumetoka 'Sare' na nyie 'tumefarakana' ,wengine mnasema 'tumefurahia' kwanini kama mna uwezo hamkutufunga Jana?
Mpira una matokeo matatu [emoji3][emoji3][emoji3]
 
Japo Mimi ni mwana Simba SC na Wewe ni Mwana Yanga SC ila hapa Mkuu umeandika ukweli mtupu na nitamshangaa Mtu wa Simba SC akipinga.
 
Naunga mkonyo ....japo yawezekana jana aliongea sababu ya gadhabu ya marefa....
Namkubali na namuheshimu mno Hanspoppe ila naona sasa amezidi na ikiwezekana sasa Yeye ndiyo awaombe Radhi upesi hawa Wachezaji Wetu.
 
Namkubali na namuheshimu mno Hanspoppe ila naona sasa amezidi na ikiwezekana sasa Yeye ndiyo awaombe Radhi upesi hawa Wachezaji Wetu.
Yeye anaamini simba haipo kwa ajili ya kufungwa
 
Nina miaka kama 25 tangu nimeangalia game kati ya timu hizi 2 (iwe live uwanjani ama kwenye runinga). Jana nimeangalia runingani nimekuwa extremely disappointed na sitakuja kurudia tena kupoteza time yangu kuangali hii game.

Kwa kelele ninazoziona na kuzisikia kwenye media kuhusu vilabu hivi siku hizi nilidhani zinapiga mpira fulani babu kubwa.... lakini jana nime confirm kwamba hivi vilabu 2 ni kama roho fulani ya kishetani imewaingia watu kuvishabikia blindly kama misukule.

Ndiyo mpira gani ule?
 
Ulitaka wachezeje we nae?
 
Ujue Simba ikicheza nataman sana nione maoni yako uwaga nafarijika unaongea ukweli japo mengine kiushabiki Ila sio mengi ya kiushabiki ubarikiwe Kwa hilo kuhusu kauli alioongea jamaa sio nzuri atasababisha chama aende yanga na yanga wataona kama wametafutiwa njia Kwa kweli
 
Sijui kwa nini, zinapocheza Simba na Yanga kuna mambo mengi ya ajabu ajabu...




Cc: mahondaw
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…