GENTAMYCINE
JF-Expert Member
- Jul 13, 2013
- 60,660
- 121,325
Kitendo tu cha Mahakama ya Usuluhishi wa Michezo duniani ( CAS ) kutupilia mbali Ombi la Mchezaji Bernard Morrison kuwa Wasiisikilize Kesi yake ni ' wake up call ' kwa Simba SC kuwa kuna ' HATARI ' inaenda Kutuangukia na huenda tusiamini na tukaja Kujuta pia.
Tafadhali upesi sana Simba SC iandae Jopo lake la Wanasheria Nguli wakiongozwa na mwana Simba SC Mwenzetu Mzee Said El Maamry na imjumuishe na ' Bingwa ' wa Kuzijua na Kuzitafsiri vyema Sheria za Soka Mzee Ismail Aden Rage waweze Kulikabili hili.
Yanga SC siyo Wajinga ( Ngumbaru ) wala Wapumbavu ( Popoma ) kulishikilia ' Bango ' hili na wala ' tusiwadharau ' kwani yawezekana Kiushahidi na Kihoja wana sehemu wenye uhakika nayo na ambayo itaenda Kutuumbua na Kutugaragaza Simba SC ' Kisheria ' kisha tukaja kuanza kutafutana mbele ya Safari.
Imenibidi taratibu GENTAMYCINE nianze Kufuatilia Rekodi za Mchezaji husika Bernard Morrison ( hasa Kitabia kote alikocheza na nimegundua kuwa ni Samjo Samjo ( Mjanja Mjanja ) sana na si Mtu wa Kumuamini 100% japo nakiri ni Mchezaji mwenye Kipaji kikubwa cha Soka na ni Msaada kwa Timu yoyote ile inayojitambua na yenye Malengo.
Nimeambiwa kuwa kumbe hata kule Afrika Kusini ambapo Simba SC ilienda Kucheza na Kaizer Chiefs FC Mchezaji Bernard Morrison alikuwa anaishi kwa wasiwasi kama ' Digidigi ' kwakuwa kumbe kuna ' Msala ' aliufanya hivyo anatafutwa na Mahakama za huko ili akajibu Mashtaka yake. Na sijui ni kwanini Klabu ya Simba imeamua kulificha hili wakati ' Wafukunyuzi ' wa Taarifa Ngumu, za Hatari na Nyeti akina GENTAMYCINE tumeshazipata.
Naomba Wanasheria wa Simba SC waanze ' Kujinoa ' vilivyo juu ya hili Sakata la Yanga SC na Mchezaji wetu Mghana Bernard Morrison kwani kwa dalili ninazoziona ninaanza Kuogopa kwani kama ni Mpambano wa Ndondi nawaona Yanga SC wanaenda Kutupiga Ngumi Moja ' takatifu ' ya TKO ambayo itatuumiza na Kutugharimu sana na hata kuiharibu ' Brand ' yetu Kimataifa.
Kama tukishinda hii Kesi na Mchezaji wetu Bernard Morrison kuwa hana ' Hatia ' nami pia GENTAMYCINE nitafurahi na ndiyo naliombea litokee hilo ila nisiwafiche Moyo wangu na Roho yangu kwa pamoja vimeanza kuwa na ' Hofu ' ya hili Suala Yanga SC kuibuka Washindi na CAS kuamua Haki kuwa Kwao 100%.