Simba SC Tanzania yamtambulisha kocha mpya Robertinho

Simba SC Tanzania yamtambulisha kocha mpya Robertinho

Kwanini tunamdharau Mgunda? Kaikuta timu katikati ya Ligi kaipeleka mpaka makundi ya CAF viongozi wetu wapuuzi sana
Wewe. Mashindano ya kimataifa sio Ligi ya NBC kule kuna hitajika mbinu na sio maneno.

Juma mgunda ni kocha mzuri ila Anahitaji MTU Ambaye Watasaidiana Mwenye Mbinu zaidi.

Kwa hili Nawapongeza sana Simba wameona Mbali. Ukiangalia mkataba wa miaka 2 kwa coach ni kuonyesha Simba wana Malengo ya Muda Mrefu.

Kwenye Malengo kuna hitaji Subira Leo Arsenal wasingekua wanapata matokeo mazuri kama wangemfukuza coach wao. Lakini hawakuangalia matokeo waliangalia project ya coach na kumpa sapoti na sasa wanakula matunda ya uvumilivu.

Niwito Wangu kwa Simba tukubali kuvumilia. Mambo mazuri yanahitaji uvumilivu sana.
 
Aliyewafikisha makundi ni Nani? Mgunda kashinda mechi mbili away CV ya Mgunda ni nzuri. Lakini tunataka mpaka aje mzungu ndio tuamini tuna kocha!!! Shame
 
Simba SC imemtambulisha aliyekuwa kocha wa Vipers SC ya Uganda, Roberto Oliveira kuwa kocha mkuu mpya wa klabu hiyo kwa kandarasi ya miaka miwili.

Oliveira amechukua nafasi ya Juma Mgunda.

#KitengeSports
 
Kwanini tunamdharau Mgunda? Kaikuta timu katikati ya Ligi kaipeleka mpaka makundi ya CAF viongozi wetu wapuuzi sana
Ni kweli nimesikitishwa na akili mbovu za viongozi wa Simba.Tutarajie kikosi kuanza kufanyiwa majaribio tena na sasa nadhani kwa bara Simba ameshajitoa kwenye ubingwa.Natabiri kuwa na mechi yake na uto atapigwa kama amesimama.Upuuzi sana huu

Sent from my Infinix X626 using JamiiForums mobile app
 
Azam wa mchukue Mgunda. Simba nao wakubali kuwa wavumilivu mpaka kocha awazoee wachezaji na atengeneze mfumo wake na hizo ndizo changamoto za kocha mpya.

Hapo wanampa mzigo wa Target ya ubingwa,ndipo ujue kuwa kocha bongo ni kazi.
 
Wanachofeli Simba ni uvumilivu kwa makocha wao tu. Kocha mpya amekuja katikati ya msimu, asipewe malengo makubwa kwa wachezaji finyu waliopo, mpira sio tu Mbinu pia VIPAJI vilivyopo vinaamua mechi.
Wenzao Yanga kocha Nabi YUKO MSIMU WA 3 huu, alikuja YANGA msimu wa 2020/2021, akamaliza nafasi ya Pili.
2021/2022 akawa bingwa
2022/2023 hadi muda huu bado game 11 anaongoza ligi.

Simba wamvumilie kidogo, afanye Sajili muhimu kisha awape mafanikio.
 
Du Mgunda pole sana, ulikuwa na Takwimu nzuri sana. Ila ndio asili ya mtu mweusi ungekuwa kocha wa rangi nyeupe kwa Takwimu hizo wala usingefukuzwa Bali wangeweka nguvu kusajili wachezaji wazuri.
 
Binafsi nilikuwa namuona Mgunda kama anatosha ila nadhani management ilifika angle hiyo thats why ikaona umuhimu wa kuleta kocha mpya.

Manzoki moja ya ahadi yake alisema akiwa na kocha wake (ambaye ndio huyu) asipokuwa top scorer kwenye ligi yetu basi atarudisha pesa zote za usajili

Ni swala la muda tu Manzoki anatua unyamani.
YIKPE alisema anaweza kufunga Magoli 40, Sserunkuma alisema atafunga si chini ya kamba 30, Mavugo nae alisema hivyo, Balinya alisema asipofikisha goli 35 aulizwe yeye.

Mpira ni Zaidi ya maneno.
 
Na Matola? Hao watakua kina nani?
Mtola toka ameenda kusoma aliporudi alivadirishiwa majukumu. Hata kwenda mwanza kusaidiana na Mgunda alienda kama emergence tu
 
Sababu zipi zimepelekea apewe boss mpya? Unafikiri kufuzu makundi ya CAF ni jambo dogo? Kocha aliyekuja ni mzuri lakini tatizo letu ni kukurupuka hatutulii na kocha mmoja,Mgunda angeaminiwa na kupewa wachezaji wazuri

Ndo maana nasemaga vijana wekezi muda na nguvu zenu katika kujiimarisha nyie wenyewe binafsi acheni ushabiki maandazi.

Lini Mgunda aliwahi kuwa KOCHA MKUU???

Toka mwanzo analetwa Simba na kwa kipindi chote alichohudumu pale Simba alikuja kama KAIMU KOCHA MKUU!! kwa maana hiyo ilikuwa lazima aletwe kocha mkuu.
 
Kaimu anaweza kupewa madaraka! Mpaka anakaimu alionekana ana uwezo,
 
Du Mgunda pole sana, ulikuwa na Takwimu nzuri sana. Ila ndio asili ya mtu mweusi ungekuwa kocha wa rangi nyeupe kwa Takwimu hizo wala usingefukuzwa Bali wangeweka nguvu kusajili wachezaji wazuri.
Acha kupotosha watu wewe.. Mgunda yupo kwa makubaliano na SSC ya kaimu kocha mkuu, na wakati ukifika hana budi kukubaliana na hali halisi.
 
Back
Top Bottom