Mtanzanias
JF-Expert Member
- Jul 30, 2021
- 1,747
- 3,725
Yanga sio wenzenu wanacheza mechi zao kimkakati na kwa mahesabu makali sana, Mzunguko huu wa kwanza yanga anacheza mechi nyingi ugenini kwenye viwanja vibovu na anakusanya point, Simba mzunguko huu wa kwanza anacheza mechi nyingi kwa mkapa na kafunga goli 14 kwa mkapa na mechi 2 za mikoani kafunga goli 2 tu nafikiri utaona ugumu atakaokutana nao mzunguko wa pili atakapoanza kucheza mechi nyingi mikoani na wakati huo yanga atakuwa kwa mkapa kwa mechi nyingi, hivyo mtihani mkubwa upo kwa simba ambae tiyali keshadondosha point 2 kwa singida ktk mechi 2 alizocheza mikoani na yanga kaokota alama 9 zote alizocheza mikoani na kesho ataokota alama kwa kagera sugar licha ya uchovu walionao kutokana na ratibaNaomba nipewe hilo jukumu na niwe na watu hawa Idi Kajuna (mtani wangu wa Kihaya), mafia mwenzangu Kassim Dewji (KD), Mandanje mzee wa kujilipua na mvaa mabomu na poti wangu kutoka kwetu mkoani Mara (Musoma), msomi na tajiri Crescentius Magori ili Yanga SC walie katika mechi zao hizi tatu zijazo.
Ya Kagera Sugar FC tunataka watoke sare (waangushe alama mbili), ya Singida Big Stars FC (japo ni ndugu zao kupitia Waziri wa Fedha Nchemba) tunataka nayo watoke sare (waangushe alama mbili tena), na ile ya Namungo FC (ambao ni ndugu zetu kabisa) tunataka Yanga SC wafungwe ili waangushe jumla ya alama (points) saba (7) tu kisha kazi imalizike.
Simba SC nitafuteni haraka GENTAMYCINE na mniwekee kabisa na mzigo (hela) wangu ili nizicheze hizi mechi zao kubwa na muhimu tatu tu sawa?
Nawaonya kama Simba SC tusipozicheza hizi mechi zao tatu na sisi leo dhidi ya Ihefu FC tukatoka sare au hata kufungwa na ile ya Namungo FC wiki ijayo nayo tukafungwa au kutoka sare basi GENTAMYCINE nasema wazi na hapa hapa JamiiForums kuwa Ubingwa wa NBC Premier League kwa msimu huu tena tuusahau na Yanga SC wataubeba (watauchukua) tena.