Simba SC tusipozicheza 'Kimkakati' na 'Kimafia' hizi Mechi Tatu za Yanga SC tusahau 'Ubingwa' tena na Msimu huu

Yanga sio wenzenu wanacheza mechi zao kimkakati na kwa mahesabu makali sana, Mzunguko huu wa kwanza yanga anacheza mechi nyingi ugenini kwenye viwanja vibovu na anakusanya point, Simba mzunguko huu wa kwanza anacheza mechi nyingi kwa mkapa na kafunga goli 14 kwa mkapa na mechi 2 za mikoani kafunga goli 2 tu nafikiri utaona ugumu atakaokutana nao mzunguko wa pili atakapoanza kucheza mechi nyingi mikoani na wakati huo yanga atakuwa kwa mkapa kwa mechi nyingi, hivyo mtihani mkubwa upo kwa simba ambae tiyali keshadondosha point 2 kwa singida ktk mechi 2 alizocheza mikoani na yanga kaokota alama 9 zote alizocheza mikoani na kesho ataokota alama kwa kagera sugar licha ya uchovu walionao kutokana na ratiba
 
Yanga wakiwa na Utulivu kama ilivyo Sasa ningumu Simba kuchukua kikombe chochote. Yanga Wana network kubwa sana na kwasasa wanakikosi imara na dirisha dogo wataongeza watu.
Na kwa taarifa yao ni kwamba inachukua zaidi ya mechi 45 Yanga kupoteza mechi moja na kwa sasa ili Simba awe bingwa inatakiwa Yanga apoteze mechi mbili kwa hesabu za haraka ni misimu miwili ijayo huu umeisha !
 
Ubingwa wa msimu huu bado sana mkuu narudia bado sanaaaa,hata azam anaweza kuwa kwenye mbio za ubingwa
 

Kwani timu gani inaongoza kwa magoli mkuu?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…