Simba SC Vs Coastal Union (2-0)| Simba yatwaa Ubingwa msimu wa 2020/21

Simba SC Vs Coastal Union (2-0)| Simba yatwaa Ubingwa msimu wa 2020/21

Sema hawa coastal union wameamua kula pesa ya simba, huku wameshajua wanashuka daraja, hivi simba sports club wataacha lini kununua hizi game
 
Kaingie basi we uwanjani Kama unaona uchungu coastal kufungwa
Ahaaa nilikuwa nimesahau, hawa si ndio small branch wa simba Ila zamani hawa coastal Walikuwa wanaitwa small simba
 
Patashika ya Ligi Kuu Tanzania Bara Vodacom Premier League VPL, Kuendelea kupigwa leo July 11, 2021 ambapo Mnyama Mkali, Simba SC, wanawakabili Wagosi wa Kaya, Coastal Union, kunako Dimba la Mkapa Jiji Dar es salaam.

Mchezo ni mgumu kwa pande zote mbili, kwani Simba SC inasaka alama tatu au sare ili kuweza kutangaza Ubingwa wa (VPL) 2020/21 kwa mara ya Nne Mfululizo huku Coastal Union wakihitaji alama tatu muhimu ili kuweza kujiweka sehemu salama kuepuka mstari wa kushuka daraja.

Simba SC yenye alama 76, kama itashinda mchezo wa leo itafikisha alama 79 na kama itatoka sare itakuwa na alama 77 ambazo haziwezi kufikiwa na timu yoyote ikiwemo Yanga SC iliyopo nafasi ya pili kwa alama 70 ambapo kama itashinda mechi zao mbili zilizobaki watafikisha alama 76.

Kocha Msaidizi wa Simba SC, Suleiman Matola, amesema kuwa wajiandaa vizuri kwa ajili ya kupata ushindi.

"Tumejiandaa vizuri kwa ajili ya kupata ushindi. Tunawaheshimu Coastal Union ni timu nzuri lakini tumejipanga kesho (leo), kutangazwa kuwa mabingwa". Amesema Matola

Naye Kocha Msaidizi wa Coastal Union Joseph Lazaro, amesema kuwa wamekuja kwa tofauti kabisa kwenye mchezo wa leo ili kujinusuru na kushuka daraja.

"Tumekuja kivingine tofauti na mechi nyingine, tumekuja kupambana dhidi ya Simba SC ili kujinusuru kutoka sehemu mbaya tulizopo". Amesema Lazaro

Nani kuibuka kidedea? Dakika 90 za jasho na damu kuamua. Kumbuka mchezo ni kuanzia saa 1:00 Usiku. Usikose Ukasimuliwa.

Kulitaka Mwana Kulipewa Mwana

....... Ghazwat....Na Jopo la JF.....


==========

Mwamuzi yupo katikati ya dimba tayari kupuliza kipyenga kuashiria kuanza kwa mchezo.

00' Naaaam mpira umeanza ni dakika 90 za Wanaume hawa kupambana | Simba SC 0-0 Coastal Union.

05' Simba SC wanajipinga kujaribu kupata nafasi huku wakiusoma mchezo wa Coastal.

13' Bocco Goooooooooooooaaal Goooooooooaaal.
John Bocco anaipatia Simba SC bao la kwanza kwa Free Kick | Simba SC 1-0 Coastal Union.

18' Shuti la mbali la Abushehe linatoka nje ya lango la Simba SC huku Umiliki wa mpira uko upande wa Simba.

23' Mugalu Goooooooooaaal Goooooooaaal

Kope Mutshimba Mugalu anaipatia Simba SC bao la pili, akimzunguka golikipa wa Coastal | Simba SC 2-0 Coastal Union.

Coastal wanafanya jaribu, lakini Defense ya Simba chini Ame wanaokoa hatari ile.

35' Simba SC wapo mbele kwa mabao mawili, huku Coastal wakijaribu kutafuta bao la kwanza, huku mashambulizi yakiendelea.

40' Coastal mbinu zao za kupenya gome ya Simba SC inadunda huku Simba kupitia kwa Mugalu na Miquissone wakipoteza nafasi bomba za kufunga.

45+1' Kuelekea kuwa mapumziko Dimba la Mkapa

Naaaam mpira ni mapumziko ambapo Simba SC wanaongoza kwa mabao mawili kwa bila dhidi ya Coastal Union. | HT, VPL: Simba SC 2-0 Coastal Union.
Line men's wamekula pesa kabisaa
 
Back
Top Bottom