Simba SC wamechea kikubwa na kimkakati

Kuna watu wangekuwa makocha wangekuwa wanafanya sub zote dakika 20 za kwanza za mchezo. Naamini kuna mipango ya kumuendeleza mchezaji kama Balua pamoja na kwamba wengi wetu hatuna uvumilivu naye kutokana na mapungufu yake ya sasa ila kuna kitu wamekiona ndiyo maana unaona anapewa dakika nyingi akiwa na Simba na hata timu ya taifa.

Jana nilisema, ile mechi inaenda kuwabatiza kwa moto madogo wote wa Simba wasio na uzoefu hasa kama wasingefungwa na ile sare nakwambia itawapa confidence kubwa sana.

Nakumbuka game ya Simba vs Wydad kule Morocco, nilimsema Baleke kutokana na mapungufu yake, nimetoka kupost tu haikupita sekunde 15 akafunga bonge la goli.
 
Yote kwa yote benchi la ufundi la Simba likumbuke kujiandaa kwa penati na "counter attack". Kwa penati hilo watajua wenyewe maana ni suala la kiufundi zaidi. Kwenye "counter attack" Simba hawajaweza kuzitumia vizuri japo wana wachezaji wenye kasi. Ni muhimu sana wakalifanyia kazi mazoezini pale kwenye mechi huwa ni hitimisho tu. Hata kwenye ligi ya ndani Simba wanashindwa kutumia vizuri "counter attack" zinapotokea. Ni muhimu sana wakafanyia kazi ili iwe rahisi kwao kupata ushindi maana kwenye hizi mechi kubwa nafasi za magoli huwa ni chache sana kwa hiyo ikitokea inabidi itumike vizuri.
 
Suluhu mmeipata mkiwa wangapi nyuma ya Mpira na bado walipata nafasi ya kufunga endapo wangekuwa vizuri kwenye eneo lao la mwisho, kwaiyo kupata suluhu sio sifa ya kujisifu kwa timu kama Simba dhidi ya timu kama Ile!
 
Mpira wa kushindwa kupiga hata pasi 7 kwa usahihi?
Mpira wa kushambuliwa mwanzo mwisho?
Mpira wa kushindwa hata kutengeneza nafasi?
Mpira wa kushindwa kupata hata on target moja?
Wachezaji hata unyumbulivu hawana?
Msimu uliopita,Yanga alicheza vzr sana Tunisia akapigwa counter za uhakika 4, 3 zikawa magoli kumbuka alitawala mpk possession,kocha wa Yanga ni toka Argentina na mpira wa nchi ile ni wa kihispania means unamtawala mwenzako.
Kocha wa Simba anatoka SĄ but mbinu nyingi amezipata kwa makocha wakijerumani,angalia Klop wa liver alivyokua anafanya sometimes haitakiwi mpira uonekane bali kutafuta matokeo na hata game ya Taifa hutaona mpira biriani utakua mchezo wa kimkakati zaidi
 
Sio dongo ndugu yangu bali ni nakusifia maana umetoka kwenye ushabiki umehamia kwenye kuuzungumzia mchezo
 
Jana Al ahly kacheza na bingwa wa kenya Gor mahia.

Mechi imechezwa Kenya ila Al ahly kashinda goli 3 kwa 0.

Simba kacheza na timu ambayo sio bingwa wa Libya.. na simba hajapiga shot on target hata moja.

Halafu unasema simba anacheza kama Al ahly
Gor Mahia ni timu ya kawaida sana haiwezi kumsumbua Al AHLY lakini kama wewe ni mtu wa boli unajua ninachozungumzia wala sio ishu ya mechi moja ya Gor Mahia ambapo pia AL aHLY kimkakati hata magoli aliyoyafunga yalikuwa ni turn overs zilizotokana na makosa ya Gor Mahia wenyewe.
 
Ni Mechi ya kutafuta matokeo tu wala hamna kuremba yaani na sie watu wa boli tunaelewa hilo na tuko tayari kwenda kuipa support Simba Sports Club
 
Kwamba malengo ya makolo yalikua asipate short on target hata moja?
 
Sasa magoli yatapatikana kwa kupiga shot off target?
Basi ongelea magoli, siyo issue ya shot on target. Simba imepata sare na imeondoka imefurahi, hizo shots on target zimeongeza nini kama zisingekuwa magoli?

Hakuna anayekataa kupata goli ingekuwa ni jambo zuri ila malengo yamefikiwa hayajafikiwa?
 
Basi ongelea magoli, siyo issue ya shot on target. Simba imepata sare na imeondoka imefurahi, hizo shots on target zimeongeza nini kama zisingekuwa magoli?
Sawa, kwaiyo mmefunga magoli mangapi?
 
Mechi ya Tunisia dhidi ya Belouizdad Kipa akiwa mdaka panzi Metacha mnata, enhe vipi mechi dhidi ya Medeama kule Mali ambayo mshika kibendera ndiye aliyewanusuru? vipi mechi dhidi ya Monastir kule Tunisia? Vipi mechi dhidi ya Tp Mazembe kule Congo? Vipi mechi dhidi ya USMA kule Algeria? Vipi mechi dhidi ya Mamelodi kule Afrika Kusini ambapo Yanga ndiye aliyeongoza kwa kufanya mashambulizi ya hatari? Na VAR ikashindwa kutumika ipasavyo kuamua goli la Aziz Ki?
Mpira wa malengo ni kucheza kwa tahadhari huku ukitafuta goli la ugenini sio kushindwa hata kutengeneza hata nafasi moja.
 
Hamna timu pale acheni kudanganywa. Wachezaji wanapiga pasi mbili mpira unapotea eti kikubwa. Wangekua wanamiliki mpira au kutopoteza kizembe labda ila sio kwa pira matope kama la jana.
 
Nikuulize wewe unayekazania shots on target. Kesho Simba ikishinda, mtakuja kusema lakini imepata kona 4 tu. Hamna jema na hamna hoja, mnabwabwaja tu.
Mtashindia wapi? fanyeni mazoezi mengi sana ya kupiga penati kwa sababu ndani ya dakika 90 hamna timu ya kuwafunga wale waarabu, mkikoswa basi sare.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…