SAYVILLE
JF-Expert Member
- Mar 25, 2010
- 7,895
- 12,975
Kuna watu wangekuwa makocha wangekuwa wanafanya sub zote dakika 20 za kwanza za mchezo. Naamini kuna mipango ya kumuendeleza mchezaji kama Balua pamoja na kwamba wengi wetu hatuna uvumilivu naye kutokana na mapungufu yake ya sasa ila kuna kitu wamekiona ndiyo maana unaona anapewa dakika nyingi akiwa na Simba na hata timu ya taifa.Kweli ndugu yangu umeongea jambo lenyewe kabisa lakini kama Kocha unakuwa na Game Plan yako kwahiyo hata mchezaji akikosea mara mbili mara tatu ndani ya uda mfupi huwezi tu kumfanyia mabadiliko lazima uwe na subra na umuelekeze ili arudi mchezoni na kukupa ile faida uliyoikusudia.Mie namuelewa Fadlu kwanini alichelewa kufanya sub japo kuna watu walikuwa wako ovyo kimchezo lakini bado timu ilikuwa kwenye shape nzuri kiufundi na bado haikuruhusu goli.
Jana nilisema, ile mechi inaenda kuwabatiza kwa moto madogo wote wa Simba wasio na uzoefu hasa kama wasingefungwa na ile sare nakwambia itawapa confidence kubwa sana.
Nakumbuka game ya Simba vs Wydad kule Morocco, nilimsema Baleke kutokana na mapungufu yake, nimetoka kupost tu haikupita sekunde 15 akafunga bonge la goli.