Simba SC wamechea kikubwa na kimkakati

Simba SC wamechea kikubwa na kimkakati

Kweli ndugu yangu umeongea jambo lenyewe kabisa lakini kama Kocha unakuwa na Game Plan yako kwahiyo hata mchezaji akikosea mara mbili mara tatu ndani ya uda mfupi huwezi tu kumfanyia mabadiliko lazima uwe na subra na umuelekeze ili arudi mchezoni na kukupa ile faida uliyoikusudia.Mie namuelewa Fadlu kwanini alichelewa kufanya sub japo kuna watu walikuwa wako ovyo kimchezo lakini bado timu ilikuwa kwenye shape nzuri kiufundi na bado haikuruhusu goli.
Kuna watu wangekuwa makocha wangekuwa wanafanya sub zote dakika 20 za kwanza za mchezo. Naamini kuna mipango ya kumuendeleza mchezaji kama Balua pamoja na kwamba wengi wetu hatuna uvumilivu naye kutokana na mapungufu yake ya sasa ila kuna kitu wamekiona ndiyo maana unaona anapewa dakika nyingi akiwa na Simba na hata timu ya taifa.

Jana nilisema, ile mechi inaenda kuwabatiza kwa moto madogo wote wa Simba wasio na uzoefu hasa kama wasingefungwa na ile sare nakwambia itawapa confidence kubwa sana.

Nakumbuka game ya Simba vs Wydad kule Morocco, nilimsema Baleke kutokana na mapungufu yake, nimetoka kupost tu haikupita sekunde 15 akafunga bonge la goli.
 
Yote kwa yote benchi la ufundi la Simba likumbuke kujiandaa kwa penati na "counter attack". Kwa penati hilo watajua wenyewe maana ni suala la kiufundi zaidi. Kwenye "counter attack" Simba hawajaweza kuzitumia vizuri japo wana wachezaji wenye kasi. Ni muhimu sana wakalifanyia kazi mazoezini pale kwenye mechi huwa ni hitimisho tu. Hata kwenye ligi ya ndani Simba wanashindwa kutumia vizuri "counter attack" zinapotokea. Ni muhimu sana wakafanyia kazi ili iwe rahisi kwao kupata ushindi maana kwenye hizi mechi kubwa nafasi za magoli huwa ni chache sana kwa hiyo ikitokea inabidi itumike vizuri.
 
Kama huo utumbo waliocheza ndio ulifanya tukatoka suluhu ugenini basi ninaomba waendelee kucheza utumbo huo huo kila wakiwa ugenini ili tuendelee kupata suluhu ugenini.
Endelea kuangalia mpira hivyo hivyo ila wengine tunaangalia tofauti kwahiyo na maoni lazima yawe tofauti cha msingi tu jifunze kuheshimu hoja na maoni ya wenzako ili nawe maoni n ahoja zako ziheshimiwe.
Suluhu mmeipata mkiwa wangapi nyuma ya Mpira na bado walipata nafasi ya kufunga endapo wangekuwa vizuri kwenye eneo lao la mwisho, kwaiyo kupata suluhu sio sifa ya kujisifu kwa timu kama Simba dhidi ya timu kama Ile!
 
Mpira wa kushindwa kupiga hata pasi 7 kwa usahihi?
Mpira wa kushambuliwa mwanzo mwisho?
Mpira wa kushindwa hata kutengeneza nafasi?
Mpira wa kushindwa kupata hata on target moja?
Wachezaji hata unyumbulivu hawana?
Msimu uliopita,Yanga alicheza vzr sana Tunisia akapigwa counter za uhakika 4, 3 zikawa magoli kumbuka alitawala mpk possession,kocha wa Yanga ni toka Argentina na mpira wa nchi ile ni wa kihispania means unamtawala mwenzako.
Kocha wa Simba anatoka SĄ but mbinu nyingi amezipata kwa makocha wakijerumani,angalia Klop wa liver alivyokua anafanya sometimes haitakiwi mpira uonekane bali kutafuta matokeo na hata game ya Taifa hutaona mpira biriani utakua mchezo wa kimkakati zaidi
 
Hahah. Nimeliona dongo lako eti "nimeanza kuelewa mpira" 🤣😂🤣

Wale mechi ya marudiano wanaenda kukutana na Simba tofauti kabisa na waliyocheza nayo jana. Tahadhari za ulinzi zitaendelea kuwepo ila tutafika saaana golini kwao. Hawajakutana na Awesu, Chasambi, Mukwala na hata silent killer Karabaka. Wanajua wana shughuli pevu ndiyo maana walipagawa.
Sio dongo ndugu yangu bali ni nakusifia maana umetoka kwenye ushabiki umehamia kwenye kuuzungumzia mchezo
 
Jana Al ahly kacheza na bingwa wa kenya Gor mahia.

Mechi imechezwa Kenya ila Al ahly kashinda goli 3 kwa 0.

Simba kacheza na timu ambayo sio bingwa wa Libya.. na simba hajapiga shot on target hata moja.

Halafu unasema simba anacheza kama Al ahly
Gor Mahia ni timu ya kawaida sana haiwezi kumsumbua Al AHLY lakini kama wewe ni mtu wa boli unajua ninachozungumzia wala sio ishu ya mechi moja ya Gor Mahia ambapo pia AL aHLY kimkakati hata magoli aliyoyafunga yalikuwa ni turn overs zilizotokana na makosa ya Gor Mahia wenyewe.
 
Msimu uliopita,Yanga alicheza vzr sana Tunisia akapigwa counter za uhakika 4, 3 zikawa magoli kumbuka alitawala mpk possession,kocha wa Yanga ni toka Argentina na mpira wa nchi ile ni wa kihispania means unamtawala mwenzako.
Kocha wa Simba anatoka SĄ but mbinu nyingi amezipata kwa makocha wakijerumani,angalia Klop wa liver alivyokua anafanya sometimes haitakiwi mpira uonekane bali kutafuta matokeo na hata game ya Taifa hutaona mpira biriani utakua mchezo wa kimkakati zaidi
Ni Mechi ya kutafuta matokeo tu wala hamna kuremba yaani na sie watu wa boli tunaelewa hilo na tuko tayari kwenda kuipa support Simba Sports Club
 
Simba Sports Club pamoja nakuwa na kundi kubwa la wachezaji wapya pamoja na benchi la ufundi jipya kabisa lakini bado wameonyesha kuwa wao ni timu namba moja kwa ukanda wa Afrika Mashariki na Kati na Namba 6 kwa ubora kwa vilabu Afrika nzima.Yaani ule mpira waliocheza jana ndio huwa unampa ubingwa Al Ahly ya Misri,Unacheza kwa malengo sio tu ilimradi na kiwango kile naiona Simba ikifika mbali sana tena ikiwezekana hata kombe watachukua.

Halafu mnaombeza Fadlu Davis kwa kumuacha nje Mukwala na kumuingiza Valentino Mashaka naomba niwaambie ukocha ni taaluma na watu wanasomea kwahiyo muacheni Mtaalamu Fadlu afanye majukumu yake kwa taaluma yake.
Kwamba malengo ya makolo yalikua asipate short on target hata moja?
 
Sasa magoli yatapatikana kwa kupiga shot off target?
Basi ongelea magoli, siyo issue ya shot on target. Simba imepata sare na imeondoka imefurahi, hizo shots on target zimeongeza nini kama zisingekuwa magoli?

Hakuna anayekataa kupata goli ingekuwa ni jambo zuri ila malengo yamefikiwa hayajafikiwa?
 
Msimu uliopita,Yanga alicheza vzr sana Tunisia akapigwa counter za uhakika 4, 3 zikawa magoli kumbuka alitawala mpk possession,kocha wa Yanga ni toka Argentina na mpira wa nchi ile ni wa kihispania means unamtawala mwenzako.
Kocha wa Simba anatoka SĄ but mbinu nyingi amezipata kwa makocha wakijerumani,angalia Klop wa liver alivyokua anafanya sometimes haitakiwi mpira uonekane bali kutafuta matokeo na hata game ya Taifa hutaona mpira biriani utakua mchezo wa kimkakati zaidi
Mechi ya Tunisia dhidi ya Belouizdad Kipa akiwa mdaka panzi Metacha mnata, enhe vipi mechi dhidi ya Medeama kule Mali ambayo mshika kibendera ndiye aliyewanusuru? vipi mechi dhidi ya Monastir kule Tunisia? Vipi mechi dhidi ya Tp Mazembe kule Congo? Vipi mechi dhidi ya USMA kule Algeria? Vipi mechi dhidi ya Mamelodi kule Afrika Kusini ambapo Yanga ndiye aliyeongoza kwa kufanya mashambulizi ya hatari? Na VAR ikashindwa kutumika ipasavyo kuamua goli la Aziz Ki?
Mpira wa malengo ni kucheza kwa tahadhari huku ukitafuta goli la ugenini sio kushindwa hata kutengeneza hata nafasi moja.
 
Simba Sports Club pamoja nakuwa na kundi kubwa la wachezaji wapya pamoja na benchi la ufundi jipya kabisa lakini bado wameonyesha kuwa wao ni timu namba moja kwa ukanda wa Afrika Mashariki na Kati na Namba 6 kwa ubora kwa vilabu Afrika nzima.Yaani ule mpira waliocheza jana ndio huwa unampa ubingwa Al Ahly ya Misri,Unacheza kwa malengo sio tu ilimradi na kiwango kile naiona Simba ikifika mbali sana tena ikiwezekana hata kombe watachukua.

Halafu mnaombeza Fadlu Davis kwa kumuacha nje Mukwala na kumuingiza Valentino Mashaka naomba niwaambie ukocha ni taaluma na watu wanasomea kwahiyo muacheni Mtaalamu Fadlu afanye majukumu yake kwa taaluma yake.
Hamna timu pale acheni kudanganywa. Wachezaji wanapiga pasi mbili mpira unapotea eti kikubwa. Wangekua wanamiliki mpira au kutopoteza kizembe labda ila sio kwa pira matope kama la jana.
 
Nikuulize wewe unayekazania shots on target. Kesho Simba ikishinda, mtakuja kusema lakini imepata kona 4 tu. Hamna jema na hamna hoja, mnabwabwaja tu.
Mtashindia wapi? fanyeni mazoezi mengi sana ya kupiga penati kwa sababu ndani ya dakika 90 hamna timu ya kuwafunga wale waarabu, mkikoswa basi sare.
 
Back
Top Bottom