Simba SC yaachana na Kocha Mkuu Abdelhak Benchikha

Hongera kocha kuliko kushusha heshima na CV Yako Bora umeachana na haya mabumunda. Hata wamlete Pep Gurdiola hatakaa pale Simba bila kuondoa matatizo ya msingi ambayo ni MO, Mangungu, Try Again na Kajula bila kusahau billion 20
 
Sio kila kitu utakikuta official page ya Ya Team
Misharavya wachezaji ushawahi ikuta official page ya Team hata pale Madrid?
Tulia shirikisha ubongo..unaongelea mishahara inafanana na termination? Wkt anakuja tuliona kwny official page ya club kama taarifa kwa umma kuwa ni kocha mpya wa Simba na kuondoka vivyo hivyo tunataka kuona kama ambavyo tumeona tayari...
 
Kwahiyo Kocha Mkuu akiuguliwa na Mkewe ndiyo analazimka kuondoka na Wasaidizi wake Wawili ili waende nae kumsaidia Kumtibia huyo Mkewe Mgonjwa? Nachukia sana Watu Wapumbavu na Waongo. Koaha Benchika mmeshindwana nae baada ya Kumtukuna Kiongozi Mmoja mkubwa tu Kikaoni kuwa kamletea Wachezaji wabovu hivyo hataki Kuharibu CV yake kaomba Kuondoka.
 
Naunga mkono hoja
 
Hakika Jombaa. Binafsi nilihisi makubaliano ya Benchika na Simba yalikuwa nusu fainali klabu bingwa, haingii akilini umlipe kocha mkuu na wasaidizi wake zaidi ya $40,000 kwa mwezi kucheza NBC premier league ambayo hata Juma Mgunda anaweza kufanya kwa ufasaha pamoja na wasaidizi wake chini ya $10,000 kwa mwezi.
 
Viongozi wasipokuwa wakweli bado hawajatibu tatizo!yaani ugonjwa wa mke usababishe kocha avuje mkataba na wasaidizi wake?
 
Jana nilimcheki try again na mangungu yanavyokenua kubeba muungano nikakasirika mpaka nikawaza ndio maana kuna watu huua bila kukusudia!simba haijawahi kuwa na viongozi wapuuzi na mbumbumbu kwa hawa wawili!
Weka limit ya hisia, hasira za kiwango cha kufikiria kuua usiruhusu, si salama kwa afya ya akili. Unaitwa mchezo wa mpira wa miguu na wewe ni shabiki.
 
Simba sc msipo aknowledge tatizo maali lilipo na kulifanyia kazi , hata kocha atoke mbinguni kwa kikosi hiko ataondoka tu.

Mme rudi kule kule alipotoka yanga, kuendeshwa kiswahili

Fitina na majungu ya kumtoa Barbra zinawatafuna
 
Tatizo Mo yupo tayari kurisk pesa yake? Miezi 10 ya kukaa na Ben gharama ni almost B, bado anahitaji wachezaji watakaohitaji mishahara mikubwa, kurudisha hizo fedha na faida ni kupitia AFL na Champion league, asipovuka ni hasara, Mo na wenzie wanaona bora ukiokota okota wachezaji wa kulipwa M5, 10 na mmoja au wawili wa bei juu wa M20,25 na kocha asiye na gharama sana halafu ukafika robo fainali Champion league na AFL ukavuka hata hatua ya pili kuliko kurisk.
 
Huwa sielewi watu wanavyosema Mo ndiyo sijui analipa mishahara huku hamna taarifa rasmi ya klabu imewahi kusema hivyo. Ukiangalia bajeti ya timu mfano ya mwaka jana imejumuisha mishahara kwa maana hiyo inatoka kwenye vyanzo rasmi vya klabu na si hisani za pembeni za watu binafsi. Katika mkutano ule sikusikia wakisema kuna gharama za nyongeza zilizolipwa na Mo nje ya bajeti.

Kabla klabu haijamuajiri mtu yoyote, iwe mfanyakazi wa kawaida, kocha au mchezaji kwanza inajiridhisha itaweza kumudu kumhudumia na kumlipa kwa kipindi chote cha mkataba. Kutumia makocha wa milioni 20 halafu ukiwa unakaribia malengo unawatoa unaleta kocha wa milioni 80 halafu unampa miezi 2 afikie lengo ni kukosa maarifa ya kiuongozi, kimpira na kuishi kimaskini.

Kama gharama ya kocha unayemtaka ni Bilion 1 kwa mwaka, itafute hiyo hela, weka kwenye bajeti mpe miaka 3 na mahitaji yake yote mengine ili afikie hayo malengo. Bilioni 3 kwa miaka 3 ni pesa kiduchu sana kama lengo la kuchukua Ubingwa wa CAF linafikiwa.
 
Reactions: Tsh
Mkuu, mkataba pesa anazotakiwa kutoa Mo ni za shughuli gani? Kwanini anahitajika?
 
Mkuu, mkataba pesa anazotakiwa kutoa Mo ni za shughuli gani? Kwanini anahitajika?
Pesa ya Mo haina tofauti na vyanzo vingine vyote vya mapato vya Klabu. Kama kuna pesa ambazo Mo anatakiwa kutoa kila mwaka hazijaspecify kazi ya hizo pesa zake moja kwa moja. Bajeti ndiyo inaamua pesa iliyokusanywa itatumikaje. Ni sawa na kuuliza pesa wanazotoa M-Bet au Sandaland ni za shughuli gani au kusema pesa ya Sandaland inalipa mshahara wa Babacar Sarr.
 
Bado ujanijibu swali mkuu. Kwanini Mo au hata akija mwingine anahitajika sana pale Simba iwapo pesa yake ni vyanzo vingine vya mapato na Simba ina vyanzo vikuu ambavyo vinaweza kuendesha timu?
 
Bado ujanijibu swali mkuu. Kwanini Mo au hata akija mwingine anahitajika sana pale Simba iwapo pesa yake ni vyanzo vingine vya mapato na Simba ina vyanzo vikuu ambavyo vinaweza kuendesha timu?
Sijaelewa msingi wa swali lako. Pesa anayotoa mwekezaji kwa mujibu wa mikataba yake na klabu ni sehemu ya hivyo vyanzo vikuu lakini hauwezi kusema hiyo pesa anayotoa imefanya kitu fulani specific kwa sababu inaingia katika mfuko wa klabu na huko ndiyo inaenda kupelekwa katika matumizi mbalimbali.

Kama Mo angekuwa anatoa pesa nje ya inayotakiwa kwenye mkataba wake na Simba, hiyo pesa ingeonekana katika ripoti ya mapato na matumizi iliyowasilishwa. Kama unakumbuka ripoti ya Simba ilionyesha mapato yamezidi matumizi, sasa pesa ya Mo ya ziada ya kazi gani?

Kama Mo au viongozi wanataja malipo anayotoa Mo mfano ya matangazo ya kwenye jezi kama pesa iliyomlipa Benchikha au usajili wa wachezaji hapo kuna udanganyifu na ulaghai unafanyika. Katika utaratibu wa uendeshaji wa klabu hii siyo sahihi. Inabidi waseme analipa kiasi gani kwa matangazo, na klabu ndiyo ipewe credit kwa kulipa hiyo mishahara.
 
Sijaelewa msingi wa swali lako. Pesa anayotoa mwekezaji kwa mujibu wa mikataba yake na klabu ni sehemu ya hivyo vyanzo vikuu.
Twende taratibu boss. Tumekubaliana pesa ya mwekezaji ni sehemu ya vyanzo vikuu vya mapato.

Sasa twende kwenye swali la pili, mishahara ya wafanyakazi ambayo ndo msingi wa hoja yetu, ni matumizi ya msingi au matumizi ya ziada?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn moreโ€ฆ