Simba Sc yaendelea kuingiza timu 4 mashindano ya CAF

Simba Sc yaendelea kuingiza timu 4 mashindano ya CAF

Hujajibu swali nanukuu "kubwa jinga miaka yote hiyo kina point 1tu" hii ndiyo hoja ya msingi
Kwani mantiki ya hizo timu nne ina mashiko gani Kwa timu kama Yanga ambayo Kila mwaka inapata nafasi ya kushiriki mashindano ya Kimataifa, baada kuchukua Ubingwa wa Ligi kuu au ule wa Shirikisho?

Hii ndiyo hoja yangu. Yanga itashiriki tu hata timu zikibakia kuwa mbili! Sasa shida iko wapi? Kwani lazima izibebe timu nyingine?
 
Kwani mantiki ya hizo timu nne ina mashiko gani Kwa timu kama Yanga ambayo Kila mwaka inapata nafasi ya kushiriki mashindano ya Kimataifa, baada kuchukua Ubingwa wa Ligi kuu au ule wa Shirikisho?

Hii ndiyo hoja yangu. Yanga itashiriki tu hata timu zikibakia kuwa mbili! Sasa shida iko wapi? Kwani lazina izibebe timu nyingine?
Hata ibaki nafasi moja tutaenda sisi
 
CAF hawataki kabisa kuiachia Simba SC kuitaja yaani, mara nafasi ya 10 kwa ubora, mara wachezaji watatu wanaunda kikosi cha wiki, hatujakaa vizuri mara Chama mchezaji bora wa wiki wa CAF.
Yaani CAF ina mahaba na Mnyama ?
 
SIMBA imeshaipa neema Tanzania 🇹🇿 baada ya kuingiza timu nne kwenye mashindano ya klabu Afrika msimu huu na msimu ujao kwa mara ya tatu mfululizo.

Kitendo cha Simba kuwepo katika hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika hadi sasa kimeihakikishia Tanzania pointi moja.

Aidha Yanga kuwepo kwenye hatua ya makundi ya Kombe la Shirikisho Afrika kimeihakikishia Tanzania pointi 0.5.

Timu hizo mbili zimefanya Tanzania iwe na pointi 29 na kushika nafasi ya tisa katika viwango vya mafanikio ya nchi kutokana na ushiriki kwenye mashindano ya klabu Afrika ambavyo nchi 12 zilizo juu ndizo kila moja inapata nafasi nne za uwakilishi kwenye mashindano ya Afrika.

Yanga watakuwa wamejipatia point 1 yaani 0.5 ya mwaka huu na ile ya 2018 walioshika mkia kwenye kundi
Mkuu njoo tupe msimamo wa point za Yanga vs Simba kwenye CAF, uzi una mwaka mmoja tu lakini yaliyojiri yanafurahisha. Embu tambeni sasa na rank basi
 
Back
Top Bottom