Simba SC yaitisha mkutano na Waandishi wa Habari hivi punde

Simba SC yaitisha mkutano na Waandishi wa Habari hivi punde

wanawaadaa washabiki wao kukwepa bakora, mpira kutiana ujinga, hata arsenal mashabiki wake wametiwa ujinga kuna arsenal mpya, manji kawaambia mashabiki kuwa yanga ya level ya tp mazembe inakuja, ukiwa shabiki wa mpira ujiandae kufanywa mjinga saa zote!
 
Che che cheche! Wanapenda vitu vya che. Wanapenda dezo dezo ebwanae mnatuchosha
 
Yaani huyu Simba wa mbereko amekuwa mpole huyu! Unaweza kumshika sharubu kabisa!!
 
Ushauri wa Bure tff ligi ya 2017/2018 ondoeni hiyo kanuni ya kukata rufaa,wekeni kanuni mtu akifungwa uwanjani imetoka hy..

Pia zengwe hili limegubikwa na uchaguzi wa tff wa agost 12,watu wanahofia nafasi zao za kamati tendaji na kamati za ulaji
Sasa bila sheria mpira utachezwaje? Ikiwa hivyo hakuna haja ya kadi masna mtu akipigwa red card leo, mechi ya kesho yuko uwanjani kusadia timu ishinde.

Vv
 
Fakhi ana miguu mingapi hadi aizuie simba kushinda? Na je kama simba wangeshinda haya yangetokea? Na kama yangetokea je wangeongezewa point 3 na goli 3 au wasingekata rufaa maana wameshinda???? Ushauri kwa viongozi wa simba semeni Fakhi aliwaathiri nini hadi mkashindwa kupata ushindi kagera?? Na kadi ya fakhi iliwaongezea nguvu gani kagera kwenye mechi yenu?? Mjitathmini kabla Toto hawajakata rufaa maana mlichezesha wachezaji 6 wa kigeni dhid ya Toto na kanuni inaruhusu wachezaji watano tu. Mtakoma mwaka huu. Kombe sio hotpot hadi mchukulie mezani
 
Baada ya kuonenaka kuwa TFF ya Malinzi, wana Kagera wenzie ( Wahaya ) na Yanga FC wanataka kuiangamiza Klabu ya Simba juu ya points zake na tayari kukiwa na tetesi kuwa huenda leo mchana maamuzi rasmi yakatolewa na Simba SC kupokwa points Uongozi wa Simba umeitisha mkutano wa haraka sana na Waandishi wa Habari katika wanachosema kuwa TFF, wana Kagera ( Wahaya ) na Yanga FC wameamua kumwaga Ugali sasa Simba SC wao wanaenda kumwaga Mboga, Maji ya kunawa, Chumvi, Pilipili ile tuheshimiane hapa mjini kama siyo nchini.

Mpira wa Bongo umeshaharibika leo ndiyo FIFA na CAF watayajua madudu yote ya Malinzi na Watu wake wa TFF.

Hongereni sana Simba SC kwa kuamua Kukinukisha na leo ndiyo leo!
Mimi sielewi ni kwa nini timu yangu Simba haikutumia mbinu za Mbao FC ili kuimaliza Kagera Sugar. Kaburu alitusawazishia mabao mawili na kuongeza la tatu. Kwa nini hakufanya hivi huko bukoba? Badala yake akaishia kufungua matawi tu.
 
Kiukweli huu mzozo mimi umenisononesha sana.TFF nilianza kuilaumu tangu Tenga alipotoka.Imekuwa ni TFF ya simba na yanga.Kiukweli sijui kama itatokea tukapata wawakilishi halali wa kimataifa. Singida united tunahofia sana uhuni huu.
 
Huyu Malinzi ni wa kumuondoa hapo TFF, kashageuza ka ofisi ka hapo nyumbani kwake.
 
Point ni za kagera alietafuta ndani ya uwanja kwa dakika 90 ila huyo ombaomba fc sijui alikuwa wapi maana hili povu na nguvu nyingi anazotumia kupiga kelele zingetumika uwanjani nina imani wangeshinda kuliko point za kuomba mezani
 
Mpira unachezwa uwanjani na mashabiki wanaingia kushuhudia na kushangilia.
Mfungwe eti mnataka kupita njia za panya mpate ushindi!!! hakuna kitu kama hicho.
Mmekutana na paka anawasubiri nje ya tundu, hamtoki humo hata mmekwisha kutubu.
Wenzenu wacheze mpira uwanjani nyie mkae mtunge story za kadi eti mpewe ushindi.
Nyie vipi!!!
 
Jiunge na group la whatsap la betting lenye members zaidi ya watu 130 upate mikeka ya uhakika na ushauri mzuri kuhusu mechi na company za betting. Kujiunga ni bure na ushauri na mikeka yote ni bure. Linki iyo hapo chini.<br /><br /><br /><br />Betting only
 
Back
Top Bottom