Simba SC yakamilisha usajili wa beki wa dimba la kati Mohamed Ouattara raia wa Burkina Faso

Simba SC yakamilisha usajili wa beki wa dimba la kati Mohamed Ouattara raia wa Burkina Faso

Pablo alimfukuzisha Nabi mwaka gani??
Sorry..Kocha Gomez da Rosa ndo alimfungisha virago Nabi akiwa Al Merreikh ya Sudan March 6, 2021 baada ya hapo ndo akaja Yanga
 
Katika kuendelea kuimarisha kikosi chake kwa msimu ujao wa 2022/ 2023 kwa michuano ya Ligi Kuu na michuano ya Kimataifa, Simba SC leo Julai 22, 2022 imekamikisha usajili wa beki wa dimba la katikati (Dinfensore Centrale) Mohamed Ouattara raia wa Ivory Coast kwa mkataba wa miaka miwili akitokea Al Hilal ya Sudan.

Beki huyu Ouattara ni changuo la Kocha mpya wa miamba ya viunga vya Msimbazi Zaron Maki ambaye anaamini kuwa ukuta wake chini ya beki Ouattara mwenye experience kubwa na soka la Afrika utakuwa imara sana.

"Beki kisiki, beki wa kuzuia mipira ya juu na chini, beki bora na mwenye uwezo wa kucheza kwenye kikosi chetu, Mohamed Ouattara ni Mnyama". Imeeleza kwa ufupi taarifa kutoka klabu ya Simba SC.

Ouattara wa Ivory Coast anaungana na Moses Phiri, wa Zambia, Victor Akpan wa Nigeria, na Augustine Okrah kutoka Ghana, ambao ni wachezaji wa Kimataifa waliosajiliwa msimu huu, ambapo Klabu imepanga kufanya vizuri kwenye michuano mbalimbali wanaoshiriki.

View attachment 2299766
Raia wa Ivory Coast
 
Nadhani pale simba kuna majitu kama lwanga,boko,akpan,mugalu ila hili ni jitu haswaa
 
Back
Top Bottom