Simba SC yalaani upangaji wa matokeo, yaahidi kutoa ushirikiano kwa mamlaka

Kila siku nasema na Narudia Simba na Yanga ni mradi wa ccm kuwapumbaza watu ,makosa ya timu yanapelekwa kwenye chama cha soka cha nchi husika sasa inapotokea binadamu akapeleka mpira kwa polisi hasa Tanzania hapo hakuna mpira kuna kupoteza muda na pesa zenu ,poleni sana wanazi wa Simba na Yanga
 
Mwanzo Simba waliepuka kuweka hadharani, wakaipeleka kesi polisi kimya kimya. Wengi tulikuja kujua baada ya kusikia kuna watu wanaitwa Polisi kuhojiwa. Ulivyoona hii taarifa imetoka hadharani, kuna kitu kitakuwa kimebainika kwenye tuhuma hizo
 
Rushwa ni jinai haiwezi pelekwa tff
 
Aliyekua kocha wa Simba Patrik phili aliwahi kukiri Simba kuchukua ubingwa bila kufungwa Ila walihonga sana, Akiyewahi kua Mchezaji wa Simba Ulimboka Mwakingwe alisha wahi shikiliwa na polisi baada ya kipa shaabani kado wa Mtibwa kukataa pesa aliyopelekewa na Ulimboka iliawaisaidie Simba iifunge Mtibwa, kipa wa Yanga Shaabani kabwili aliwahi kuweka bayana njama za Viongozi wa Simba kumtaka afanye mipango apewe kadi ili asiweze kudaka Mechi ya Simba na Yanga.
Simba ina utamaduni wa kuhonga Marefa na wachezaji wa timu pinzani kwa muda mrefu, Vitendo hivyo hushindwa kuvifanya kwenye michuano mikubwa mwishoe hupigwa Goli tanotano.
 
Rushwa inachunguzwa wapi?
Hivi wewe utakua unajua mpira na taratibu zake kuliko kina Magori?
 
Mtajitetea kwenye Vyombo vya dola
 
Mapovu ya nini?
 
Mikia Mnatapatapa Sana Na Hapo Mmepoteza Mechi Mbili Ndio Mmejua Kuna Upangaji Wa Matokeo.

Subirini Kipigo Bado Kinaendelea. Mnasahau Wachezaji Wenu Wengi Wameanza Kuchoka.

Kina Wawa, Onyango huyo ni Uchochoro Akina Mkude Akina Kaata, Bocco Accuracy Imepungua Sana Bwalya Ndio Hamna Kabisa Bado.

Mnang'ang'ania Kutafuta Mchawi Nje Ya Team Wakati Mchawi Ni Kikosi.
Subirini Mjionee Hao Wa-Nigeria Watakavyofanya Mnaelewa Nini.

Sijui Mtamtafuta Mpangaji Wa Matokeo CAF.
 
JINAI HAINA KIKOMO KAFUNGUENI JALADA YASIISHIE MANENO TU,KAFUNGUENI KESI PHIRI BADO YUPO HAI HUKO ZAMBIA ATAKUJA KUTOA USHAHIDI
 
Yanga tarehe 7 November alihonga refa akapewa penati ya maelekezo

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…