Simba SC yampa mapumziko Bernard Morrison hadi mwisho wa msimu huu 2021/ 2022

Simba SC yampa mapumziko Bernard Morrison hadi mwisho wa msimu huu 2021/ 2022

Simba mbumbumbu sana yaani semeni mmemuacha.

Anyway welcome back homeboy
Hapa aziz ki,adebayor pale halafu kati mayele pembeni kabisa anasimama mzee mzima moses phiri.😂😂
 
Kumbe GSM kashafanya yake tayari ndio maana Simba wameondoa kirusi mapema ndani ya kambi yao.

Ni maamuzi mazuri kwa Morson maana msimu ujao kaona hata benchi hatakuwepo Kutokana na ujio wa Luis, Tau na Adebayo
Hakuna club Tanzania inaweza kumsajili Percy Tau, haipo
 
Sasa bila Morison itakuwaje? Nani ata cover nafasi yake na kwa kiwango kama chake?
 
lamda kama Morison mwenyewe ndiye aliyeamua kuondoka lakini kama ni simba imeamua kumuacha hapa tumekosea sana kumuachia Morison kisa nidhamu yake.
Mchezaji asipokuwa na nidhamu ataiharibu timu....wachezaji wengine wataiga .
 
Huyu Morisson Yanga wakimrudisha na mpira wa Tanzania naacha kufatilia kabisa, utakuwa ni upumbavu wa kiwango cha juu
 
Uzuri anaondoka kwa amani kwa makubaliano ya pande zote mbili yaani yeye kama mchezaji na Simba kama Club. Sio kama wanavyo ondokaga wa Yanga
 
Huyo jamaa ni bonge la mchezaji. Narudia tena ni bonge la mchezaji. Ila kichwani kwake anajua mwenyewe kuna nini. Nidhamu mbovu ni hatari sana kwa timu. Nafikiri Simba wameona kuwa:-
1. Anaweza kuambukiza tabia yake mbaya kwa wachezaji wengine.
2. Akiadhibiwa na timu maana yake timu inapungiwa wachezaji hasa ikitokea kuwa wachezaji wanaocheza nafasi yake ni majeruhi au wana kadi.
3. Akifanya utovu wa nidhamu asipoadhibiwa maana yake mchezaji mwingine akifanya kosa kama lake hataadhibiwa mwisho wa siku timu nzima inakuwa na nidhamu mbovu.
4. Akifanya kosa asipoadhibiwa anapunguza morali kwa wenzake na kuona kuwa anapendelewa.
5. .......................................
 
Vita ya kukataa wahuni mliipuuza mkamsajili muhuni ona sasa alivyowafanyia uhuni
 
Hii nayo ni chai. Hakuna mshahara huu hapa Tanzania.
Pole sana, Gomez alikuwa analipwa milioni 29 kwa mwezi. Muwe mnafatilia vyombo vya habari jamani.

Unajua mkurugenzi wa NHC au TANESCO analipwa milioni 30 na zaidi kwa mwezi? Na ni hapa hapa Tanzania? Ulimsikia JPM alivyotoa hiyo Siri?
 
Huyo jamaa ni bonge la mchezaji. Narudia tena ni bonge la mchezaji. Ila kichwani kwake anajua mwenyewe kuna nini. Nidhamu mbovu ni hatari sana kwa timu. Nafikiri Simba wameona kuwa:-
1. Anaweza kuambukiza tabia yake mbaya kwa wachezaji wengine.
2. Akiadhibiwa na timu maana yake timu inapungiwa wachezaji hasa ikitokea kuwa wachezaji wanaocheza nafasi yake ni majeruhi au wana kadi.
3. Akifanya utovu wa nidhamu asipoadhibiwa maana yake mchezaji mwingine akifanya kosa kama lake hataadhibiwa mwisho wa siku timu nzima inakuwa na nidhamu mbovu.
4. Akifanya kosa asipoadhibiwa anapunguza morali kwa wenzake na kuona kuwa anapendelewa.
5. .......................................

Nimekupa like mkuu.
 
Back
Top Bottom