Simba SC yamtambulisha rasmi Afisa Mtendaji Mkuu (CEO) mpya, Senzo Mazingiza kutoka Afrika Kusini

Simba SC yamtambulisha rasmi Afisa Mtendaji Mkuu (CEO) mpya, Senzo Mazingiza kutoka Afrika Kusini

Ghazwat

JF-Expert Member
Joined
Oct 4, 2015
Posts
23,718
Reaction score
66,267
Klabu ya Simba leo Septemba 7, 2019, imemtambulisha rasmi Senzo Mazingiza kutoka Afrika Kusini kuwa Afisa Mtendaji Mkuu (CEO), wa klabu hiyo, akichukua nafasi ya Crescentius Magori ambaye amemaliza muda wake.

Akizungumza wakati wa utambulisho huo uliofanyika leo kwenye Hoteli ya Serena Jijini Dar es salaam, Senzo ambaye amewahi kufanya kazi katika Klabu ya Orlando Pirates, Platinum Stars FC pamoja na Chama cha Soka cha Afrika Kusini, ameahidi kuifanya klabu ya Simba kuwa klabu kubwa zaidi barani Afrika.

"Simba ni timu kubwa sana, nimekuwa nikiifuatilia kwa muda sasa. Nimejifunza kuwa ni timu kubwa, na tunaweza kuifanya kubwa zaidi, sio tu ukanda wa Afrika Mashariki bali kuwa klabu kubwa zaidi Afrika" amesema Senzo

Kwa upande wake CEO ambaye amemaliza muda wake Crescentius Magori, amewashukuru Wanasimba kwa ushirikiano waliompa muda wote kwa kipindi chake hadi kumalizika.

"Kuanzia wiki ijayo nitakuwa CEO mstaafu, nawashukuru sana kwa ushirikiano mlionipa. Nawashukuru sana Wanasimba. Kwa wale ambao tumekwazana niombe radhi ilikuwa sababu ya kazi yangu" alisema Magori.

SimbaSCNguvuMoja

IMG_20190907_135418_064.jpeg
FB_IMG_1567853511879.jpeg
 
Ina maana hakuna Mtanzania mwenye sifa za kuwa CEO wa klabu kama Simba? Au ni ugonjwa mpya wa kuamini wageni zaidi. Tumeanza wachezaji, makocha, leo ma CEO, kesho?
Ikiwa ni kweli hakuna, nina watakia SSC kila la kheri.
 
Nani hapa nchini? mwenye cv ya kuendesha klabu kuitoa hapa kuipeleka juu zaidi katika mfumo wa kisasa
Ina maana hakuna Mtanzania mwenye sifa za kuwa CEO wa klabu kama Simba? Au ni ugonjwa mpya wa kuamini wageni zaidi. Tumeanza wachezaji, makocha, leo ma CEO, kesho?
Ikiwa ni kweli hakuna, nina watakia SSC kila la kheri.
 
Simba ndo mfalme,,wengine wote ni mboga ya mfalme
 
Nafasi ilitangazwa kwa wote, CEO mstaafu Crescentius Magori amesema waliomba ni Watanzania 6, Mmarekani 1, MSouth 1.. Ambaye amekidhi vigezo ni Senzo..!

Tuheshimu wenye taaluma zao ndipo tutasonga mbele..SimbaNguvuMoja
Ina maana hakuna Mtanzania mwenye sifa za kuwa CEO wa klabu kama Simba? Au ni ugonjwa mpya wa kuamini wageni zaidi. Tumeanza wachezaji, makocha, leo ma CEO, kesho?
Ikiwa ni kweli hakuna, nina watakia SSC kila la kheri.
 
simba ni timu ya watu tena wanaojitambua.. nafasi ikitangazwa inakuwa wazi kwa wote lengo ni kupata mshindani aliye sahihi... sisi sio timu ya wananchi wa jangwani wanaopeana vyeo kwa kuangalia mtu anayejua kuongea kiswahili tu. hiyo kazi ilitangazwana watu wakaomba bila kujali mipaka ya nchi. ilikuwa wazi kwa wotu wote wanaojitambua.

Back
Top Bottom