Simba SC yamtambulisha rasmi Afisa Mtendaji Mkuu (CEO) mpya, Senzo Mazingiza kutoka Afrika Kusini

Simba SC yamtambulisha rasmi Afisa Mtendaji Mkuu (CEO) mpya, Senzo Mazingiza kutoka Afrika Kusini

Aisee why not Saad Kawemba or Patrick Kahemele?

Kwanini wasingetafuta mzungu from UK ambao football culture yetu ni kama copy and paste ya UK ?
Unaanza kumkosoa mtu hata majikimu hajaanza, pili mazingira ya ulaya tofauti na hapa Africa
 
Aisee why not Saad Kawemba or Patrick Kahemele?

Kwanini wasingetafuta mzungu from UK ambao football culture yetu ni kama copy and paste ya UK ?
Hujui maana ya ushindani?ajira imetangazwa international invitation. Tuambie kama Saad na Kahemele waliomba wakakidhi vigezo na bado wakaachwa. Wabongo mtaacha lini longolongo?
 
Ajira ilitangazwa world wide je kuna mmbongo alifikia vigezo? Cv ya huyo jamaa umeipitia?
Ina maana hakuna Mtanzania mwenye sifa za kuwa CEO wa klabu kama Simba? Au ni ugonjwa mpya wa kuamini wageni zaidi. Tumeanza wachezaji, makocha, leo ma CEO, kesho?
Ikiwa ni kweli hakuna, nina watakia SSC kila la kheri.
 
Aisee why not Saad Kawemba or Patrick Kahemele?

Kwanini wasingetafuta mzungu from UK ambao football culture yetu ni kama copy and paste ya UK ?
Waliapply? Nafasi zilitangazwa watu wakaaply mwenye vigezo vilivyokidhi kapata! Afterall ni mwafrika so kufanya kazi na Watanzania haitakuwa ngumu kama ungechukua mtu kutoka Uingereza
 
Hivi hivi viongozi wa club nao wanatoka nje.

Watawapoteza washabiki bure na haji manara aanze kulia mbona uwanja haujai.
Kwahiyo Liverpool wakiajiri boss kutoka Spain wanapoteza mashabiki???
 
Kila Mwaafrika sasa hivi anatakiwa awagomee Afrika Kusini mpaka wajirekebishe. Hii siyo mara ya kwanza wao kuuwaa na kupora wageni.
Simba wangeonesha mshikamano na Waafrika wengine kipindi hiki.
Si kila jambo lazima litolewe tamko au zuio.
Kuna Watanzania wameuliwa kule.
Nigeria ndio wameonyesha kitu.. hata wasouth waliopo kwa Buhar wameipata ya moto.
Huku kwetu nini kinaendelea..? Au simba ndio wabebe sura ya taifa?
 
Nigeria ndio wameonyesha kitu.. hata wasouth waliopo kwa Buhar wameipata ya moto.
Huku kwetu nini kinaendelea..? Au simba ndio wabebe sura ya taifa?
Simba haijaanza leo kubeba bendera ya taifa.
 
Watu wanakufa hapa Tanzania kwa kupotezwa na hakutolewi tamko itakuwa Afrika kusini.
Kila Mwaafrika sasa hivi anatakiwa awagomee Afrika Kusini mpaka wajirekebishe. Hii siyo mara ya kwanza wao kuuwaa na kupora wageni.

Simba wangeonesha mshikamano na Waafrika wengine kipindi hiki.

Si kila jambo lazima litolewe tamko au zuio.

Kuna Watanzania wameuliwa kule.
 
Hawa sindio wanalalamika kule kwao kwamba wageni wanachukua nafasi zao mpk wanafanya vurugu?
Aisee. Kama ingalikuwa kule kwao au Nigeria au Congo tungesikia mengine. Wangemmarehemu fasta. Hata hivyo sioni kama kulikosekana Mtanzania wa kujaza hiyo nafasi (lengo sio ubaguzi) natumai kuna vigezo mahsusi za ajira za wageni kwa kila nafasi. Hebu tujiulize vilifutwa? Isije ikawa kama ndani ya kampuni za Mo, kila nafasi yupo Kanjibai, waswahili wapo nafasi fulani zisizo na umuhimu!!
 
Watu wanakufa hapa Tanzania kwa kupotezwa na hakutolewi tamko itakuwa Afrika kusini.
Yanayotokea Afrika Kusini sijayaona hapa kwetu. Au huelewi kinachoendelea huko?

Sijaona Watanzania kuua na kupora mali za Waafrika wenzao wageni kwa maandamano.

Kama umewahi kuona hayo naomba nioneshe.
 
Klabu ya Simba leo Septemba 7, 2019, imemtambulisha rasmi Senzo Mazingiza kutoka Afrika Kusini kuwa Afisa Mtendaji Mkuu (CEO), wa klabu hiyo, akichukua nafasi ya Crescentius Magori ambaye amemaliza muda wake.

Akizungumza wakati wa utambulisho huo uliofanyika leo kwenye Hoteli ya Serena Jijini Dar es salaam, Senzo ambaye amewahi kufanya kazi katika Klabu ya Orlando Pirates, Platinum Stars FC pamoja na Chama cha Soka cha Afrika Kusini, ameahidi kuifanya klabu ya Simba kuwa klabu kubwa zaidi barani Afrika.

"Simba ni timu kubwa sana, nimekuwa nikiifuatilia kwa muda sasa. Nimejifunza kuwa ni timu kubwa, na tunaweza kuifanya kubwa zaidi, sio tu ukanda wa Afrika Mashariki bali kuwa klabu kubwa zaidi Afrika" amesema Senzo

Kwa upande wake CEO ambaye amemaliza muda wake Crescentius Magori, amewashukuru Wanasimba kwa ushirikiano waliompa muda wote kwa kipindi chake hadi kumalizika.

"Kuanzia wiki ijayo nitakuwa CEO mstaafu, nawashukuru sana kwa ushirikiano mlionipa. Nawashukuru sana Wanasimba. Kwa wale ambao tumekwazana niombe radhi ilikuwa sababu ya kazi yangu" alisema Magori.

SimbaSCNguvuMoja

View attachment 1200719View attachment 1200720
Manara nae lini kibarua chake? Ataweza wasiliana na msauzi kizungu?
 
Acheni visingizio, gemu ilikuwa ngumu kwenu wala si kutokana na kuwadharau, ni uwezo uliishia pale.
Kati ya simba na yanga nani huwa anaongoza kwa kutafuta visingizio vya kulia lia akifungwa.....kuna timu sikuhizi imekuwa kikundi cha waliajiwaliaji wakifungwa...mara utasikia sjui tumefungwa sababu ya tff,mara utaskia sjui tumefungwa sababu tff wanawabeba simba,mara tumefungwa sababu sjui marefa,mara utaskia tumefungwa sababu uwanja mbaya,mara tumefungwa sababu timu imecheza saa nane...juzi wamepigwa goli la pili clear na jkt ruvu refa anakataa ingekuwa wamefunga wao sasa refa akagoma or kafungwa simba ilo goli alafu refa kagoma ungeona msururu wa mapovu humu jf but kwa kuwa ni wao walitulia kimya kama hakijatokea kitu
 
Back
Top Bottom