Simba SC yapokwa pointi 3 dhidi ya Kagera Sukari

Kadi tatu,hazijaguswa kabisa?Hiki ni kichekesho.
 
Kwa akili hizi eti tutafanikiwa Tanzania! Mimi huwa nasema maendeleo ya aina yoyote Tanzania hayataletwa na kizazi chetu hiki wala kijacho. Ni mpaka itakapotokea struggle ya nguvu, watakaokuwepo baada ya hiyo "struggle" watakuja na akili mpya.
 
Serengeti boys walitolewa na wale waCongo lakini CAF wamewarudisha mashindanoni. Fair play kwenye soccer ni pamoja na kuzingatia vigezo na masharti.
Vigezo Na masharti ndiyo rufaa ya Simba haikukidhi, sasa unalialia nini?
 
Hivi ilikuaje kamati ya Masaa 72 ikatoa uamuzi mkubwa kama ule wa kuipa pont 3 na magoli 3 Simba kama rufaa ya Simba ilikua nje ya muda na haikulipiwa ada.....
Hiki mbona ni kichekesho cha karne
 
Basi kulikuwa hakuna sababu ya kuwa na sheri 17za soka
Hakuna kati ya sheria 17 inayosema timu inaweza kupewa ushindi wa mezani, bali sheria 17 za soka zinasimamia mchezo ndani ya dakika 90.

Hivi umewahi kusikia Barcelona au Chelsea imepewa point tatu na magoli matatu mezani?only in Tanzania.

Na ndio sababu hatuendelei katika soka. Leo hii watu badala ya kuhangaika kushinda mechi uwanjani ndani ya dakika 90 eti wanahangaika kushinda mezani.
 
Real Madrid aliondolewa mwakajana kwenye kombe la Mfalme japo alishinda hyo mechi baada ya kumchezesha mchezaji mwenye kadi tatu za njano .Jipange ndugu kama hujui mpira na huna facts
 
Real Madrid aliondolewa mwakajana kwenye kombe la Mfalme japo alishinda hyo mechi baada ya kumchezesha mchezaji mwenye kadi tatu za njano .Jipange ndugu kama hujui mpira na huna facts
Yaani mnawasilisha rufaa nje ya muda uliopangwa kisheria then mnakataa hata kulipia ada ya rufaaa, alafu mnalia lia eti mmeonewaa????? aloo kweli nyie mko serious kweli? tena kosa lenu ni kubwa kuliko hao waliomchezesha mchezaji mwenye kadi 3
 
Real Madrid aliondolewa mwakajana kwenye kombe la Mfalme japo alishinda hyo mechi baada ya kumchezesha mchezaji mwenye kadi tatu za njano .Jipange ndugu kama hujui mpira na huna facts
Unajua ya real Madrid tofauti na hii ya Simba acha kukurupuka kijana,

Ishu ya Madrid ilikuwa hivi, Denis Cheryshev alikuwa kwa mkopo Villareal, alicheza mechi za cope del Rey na kupata card 3 za njano, msimu unafuata akarudi kwny timu yake Madrid, hivyo Madrid hawakujua km Denis alipata card 3 akiwa kwa mkopo Villarreal, basi wakamchezesha ndio wakapokonywa ushindi, huoni tofauti hapo
 
Kuna jambo ambalo wengi hamjaligundua hapa, ukweli ni kwamba yule mchezaji wa Kagera Sugar hakuwa na kadi 3. TFF wameamua tu kuwafichia Simba aibu, maana wangesema ukweli kuwa alikuwa na kadi 2 ingekuwa kashfa kubwa kwa Simba na Bodi ya ligi. Ni aibu kubwa kwa Club kubwa kama simba kuendekeza mambo ya kugushi.
 
Mambumbumbu chezeni mpira mnatia aibu meals laminal a lamina pointing tatu za mezani
 
Wewe utakuwa muhaya labda
 
Naomba nikukumbushe real Madrid miaka miwili iliyopita alitolewa kwenye kombe la mfalme licha ya kuwa alishinda kwa makosa hayo hayo ya card.

 
Kwa hiyo real Madrid alionewa!? Ndio maana ya vigezo na masharti kuzingatiwa. Ni kama Pogba alivyokosa mechi ya kwanza ya united. Kwa hiyo hapo unajichanganya mwenyewe kwa sababu umeonesha wazi kuwa mchezaji alikuwa na kadi.

 
Unachekesha sana. Hivi ni jukumu la klabu kuweka rekodi ya kadi za wachezaji pinzani!? Unajua man tiki ya hukumu hii ni nini!? Ni kuwa hivi sasa mtibwa sugar anaweza kumchezesha mchezaji mwenye kadi anapocheza na yanga ili mradi tu yanga wakubali kutopeleka malalamiko tff.

 
Kitu ambacho kinatakiwa kwa Kamati ya Katiba Sheria na Hadhi ya wachezaji ni kuwaambia watanzania kuwa Fakhi alikuwa na kadi tatu au la. Hii ndiyo inawafanya watanzania kushabikia Timu za Uingereza. Maana bingwa anayepewa kila mwaka akienda kwenye mashindano ya kimataifa ni mapema anarudi na kapu la magoli.
 
Sikuelewi mkuu. Hoja yangu wala haiko kwenye nani apewe au asipewe pointi za mezani. Nilichokuwa nimesisitiza ni kwamba kesi ya pointi tatu za Serengeti Boys na hizi zinazolalamikiwa na Simba ni vitu viwili tofauti. Moja inahusu mchezaji aliyedanganya umri, ambaye kumbukumbu zake haziwekwi hadharani wala si jukumu la waamuzi wa pambano husika. Nyengine inahusu madai ya mchezaji kuwa na kadi tatu za njano, ambazo zunahusiana moja kwa moja na waamuzi wa pambano husika kwa kuwa hupaswa kuonesha kadi hizo hadharani na kuzinakili kwenye kumbukumbu zao. Ya kwanza inahusu vipimo vya kitaalamu kwa mlalamikiwa, ambavyo vitabainisha umri halisi wa mchezaji. Ya pili haina njia yoyote ya kisayansi ya kuithibitisha bila ya kuwepo kumbukumbu za mchezo husika. La kwanza wahusika hawakutoa ushirikiano, lakini hawajalalamikia hukumu iliyotolewa na mamlaka husika. La pili kila upande ulitoa ushirikiano lakini bado utata ukabaki juu ya upande upi umesema kweli. Walioshindwa wamelalamikia hukumu iliyotolewa na mamlaka husika. Kichekesho siyo mimi Mkuu, ni hilo igizo lenyewe la kushindwa kuwa na Kumbukumbu za mchezo husika.
 
Je na faki alikuwa na kadi ngapi za Njano mbona wahaya hilo munajiumauma hamjibu mara hawajalipia sijui rufaa imechelewa kubebana huku ndio kunakolemaza soka la kibongo aibu kwenu wahaya wa tff
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…