Simba SC yatangaza haitacheza mechi dhidi ya Yanga, Wakidai vitendo visivyo vya kiungwana dhidi yao

Joseverest

JF-Expert Member
Joined
Sep 25, 2013
Posts
52,812
Reaction score
71,392
Katika taarifa kwa Umma waliyoitoa saa 7 na dakika 46 usiku wa 8/3/2025 klabu hiyo imesema haitoshiriki mchezo huo wa Derby uliopangwa kufanyika majira ya saa 1 usiku 8/3/2025 kutokana na kuzuiliwa kufanya mazoezi uwanja wa Benjamin Mkapa na Wanaojiita Makomandoo wa Yanga

Nini maoni yako?

soma zaidi

Pia soma:
 
Sio tetesi tena, Its Official

Simba Sports Club imesikitishwa na vitendo visivyo vya kiungwana dhidi ya timu yetu kuelekea Mchezo wa Ligi Kuu NBC dhidi ya Yanga, Simba ikiwa timu mgeni.

Kwa Mujibu wa Kanuni 17(45) ya Kanuni za Ligi Kuu Bara, Timu Mgeni ina haki ya kufanya mazoezi kwenye uwanja wa mechi angalau mara moja kabla ya siku ya mechi katika muda tarajiwa wa mchezo husika. Kwa makusudi Simba imenyimwa haki hiyo licha ya kufika uwanjani katika muda husika.

Katika Sintofahamu hiyo, Simba iliarifiwa na Meneja wa Uwanja kuwa hana maelekezo ya kuruhusu mazoezi kufanyika bila maelekezo ya kamishna wa Mchezo. Pamoja na Kamishna wa mchezo husika kufika, Mabaunsa wa Klabu ya Yanga walivamia Msafara wa Simba huku wakiendelea na vurugu na wakizua Msafara wa simba kuingia uwanjani kufanya mazoezi. Jitihada za Simba kupata ufumbuzi wa changamoto hiyo hazikuzaa matunda kwa zaidi ya Masaa Mawili kabla ya Simba kuondoka eneo la nje ya uwanja kwa sababu za kiusalama ambazo zimerekodiwa kwa gjili ya ushahidi.

Kufuatia ukiukwaji huo wa Taratibu za Mchezo, Simba haitoshiriki Mchezo husika na haki zote zimehifadhiwa. Simba inahimiza kuchukuliwa kwa hatua stahidi dhidi ya wahusika wote wa sakata hili.


 
Watu wamelala wakiamka watakutana na hii

Inanikumbusha Mei 8 mwaka 2021 Yanga alisusia mechi tena kwa sababu ambazo ilikuwa ni mabadiliko ya ratiba ya mechi.

Let's see kitachoenda kufanyika.
 
Haki itendeke.

Source ya haya yote ni imani za kishirikina kitu ambacho ni upuuzi kabisa. Ushirikina ulioshindwa kuwapa kombe la CAF hadi leo bado mnauendekeza hadi leo.

Sijui hili jambo limekaae kisheria ila kama Yanga wanamakosa waadhibiwe iwe fundisho kwa hawa makomandoo uchwara.

Mwisho wa siku nawalaumu TFF wao ndio wanaolea upuuzi wa hizi timu mbili matokeo yake ndio haya sasa.
 
Hili tatizo linatengenezwa na TFF wenyewe kwasababu ya wepesi wa adhabu wanayotoa kwa wakosaji.

Sasa kama sheria ya adhabu inasema faini ni milioni 1 hadi 5.

Kwa Club hizi ambazo mchezaji analipwa zaidi ya milioni 20 basi milion 5 haiwezi kuwa kikwazo wala adhabu ya kuwafanya wajiulize mara mbili pindi wanapofikiria kufanya huu ujinga.
 
Anakatwa point tatu na magoli matatu
Simba hawezi kukatwa pointi kwenye tatizo ambalo ametengenezewa.

Anakatwa point akiwa yeye ndio amevunja kanuni. Hawezi kuwajibika kwenye makosa yaliyofanywa na mtu mwingine.

And for the records Simba wapo vizuri kwenye sheria na wanajitahidi sana kuheshimu taratibu za kimpira.

Sitaki kuamini kama wamekuwa wazembe wasione hili uliloliona wewe.
 
Watu wamelala wakiamka watakutana na hii

Inanikumbusha Mei 8 mwaka 2021 Yanga alisusia mechi tena kwa sababu ambazo ilikuwa ni mabadiliko ya ratiba ya mechi.

Let's see kitachoenda kufanyika.

Timu za Yanga na Simba jinsi wanavyofanya mambo yao kwa kuhujumiana utafikiri ni kama vile Wanasiasa wa CCM na wa Vyama vya Upinzani wanavyofanya Siasa zao wakati wa Kampeni za Chaguzi za kisiasa.
Hakuna tofaufi kabisa.
 
Kwani wanatakiwa kutoa taarifa muda gani kabla ya mechi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…