Simba SC yatangaza haitacheza mechi dhidi ya Yanga, Wakidai vitendo visivyo vya kiungwana dhidi yao

Simba SC yatangaza haitacheza mechi dhidi ya Yanga, Wakidai vitendo visivyo vya kiungwana dhidi yao

Sio tetesi tena, Its Official

Simba Sports Club imesikitishwa na vitendo visivyo vya kiungwana dhidi ya timu yetu kuelekea Mchezo wa Ligi Kuu NBC dhidi ya Yanga, Simba ikiwa timu mgeni.

Kwa Mujibu wa Kanuni 17(45) ya Kanuni za Ligi Kuu Bara, Timu Mgeni ina haki ya kufanya mazoezi kwenye uwanja wa mechi angalau mara moja kabla ya siku ya mechi katika muda tarajiwa wa mchezo husika. Kwa makusudi Simba imenyimwa haki hiyo licha ya kufika uwanjani katika muda husika.

Katika Sintofahamu hiyo, Simba iliarifiwa na Meneja wa Uwanja kuwa hana maelekezo ya kuruhusu mazoezi kufanyika bila maelekezo ya kamishna wa Mchezo. Pamoja na Kamishna wa mchezo husika kufika, Mabaunsa wa Klabu ya Yanga walivamia Msafara wa Simba huku wakiendelea na vurugu na wakizua Msafara wa simba kuingia uwanjani kufanya mazoezi. Jitihada za Simba kupata ufumbuzi wa changamoto hiyo hazikuzaa matunda kwa zaidi ya Masaa Mawili kabla ya Simba kuondoka eneo la nje ya uwanja kwa sababu za kiusalama ambazo zimerekodiwa kwa gjili ya ushahidi.

Kufuatia ukiukwaji huo wa Taratibu za Mchezo, Simba haitoshiriki Mchezo husika na haki zote zimehifadhiwa. Simba inahimiza kuchukuliwa kwa hatua stahidi dhidi ya wahusika wote wa sakata hili.

View attachment 3263098
Kwa nini simba alitaka aingie na mbuzi na bundi mzoga uwanjani?
 
Hatari kubwa hii, kamati ya masaa 72 mezani tena.
20250308_025246.jpg
 
Katika taarifa kwa Umma waliyoitoa saa 7 na dakika 46 usiku wa 8/3/2025 klabu hiyo imesema haitoshiriki mchezo huo wa Derby uliopangwa kufanyika majira ya saa 1 usiku 8/3/2025 kutokana na kuzuiliwa kufanya mazoezi uwanja wa Benjamin Mkapa na Wanaojiita Makomandoo wa Yanga

Nini maoni yako?

soma zaidiView attachment 3263095

Pia soma:
Hakuna Kususa hapa
 
Haki itendeke.

Source ya haya yote ni imani za kishirikina kitu ambacho ni upuuzi kabisa. Ushirikina ulioshindwa kuwapa kombe la CAF hadi leo bado mnauendekeza hadi leo.

Sijui hili jambo limekaae kisheria ila kama Yanga wanamakosa waadhibiwe iwe fundisho kwa hawa makomandoo uchwara.

Mwisho wa siku nawalaumu TFF wao ndio wanaolea upuuzi wa hizi timu mbili matokeo yake ndio haya sasa.

Soka la Tanzania limejikita zaidi kwenye masuala ya kutegemea 'Ndumba na Vibuyu' badala ya kutegemea Sayansi ya Kufanya Mazoezi ili kuweza kujiimarisha vizuri zaidi kwa ajili ya Soka la Ushindani.

Wahusika wanashindwa kuelewa kwamba Soka ni Sayansi, ambapo ukifuata Kanuni basi Matokeo Chanya lazima utayapata na usipofuata Kanuni Matokeo Hasi lazima utayapata.
 
Hili tatizo linatengenezwa na TFF wenyewe kwasababu ya wepesi wa adhabu wanayotoa kwa wakosaji.

Sasa kama sheria ya adhabu inasema faini ni milioni 1 hadi 5.

Kwa Club hizi ambazo mchezaji analipwa zaidi ya milioni 20 basi milion 5 haiwezi kuwa kikwazo wala adhabu ya kuwafanya wajiulize mara mbili pindi wanapofikiria kufanya huu ujinga.
Wangekuwa wanakatwa points haya mambo yangeisha.
 
Katika taarifa kwa Umma waliyoitoa saa 7 na dakika 46 usiku wa 8/3/2025 klabu hiyo imesema haitoshiriki mchezo huo wa Derby uliopangwa kufanyika majira ya saa 1 usiku 8/3/2025 kutokana na kuzuiliwa kufanya mazoezi uwanja wa Benjamin Mkapa na Wanaojiita Makomandoo wa Yanga

Nini maoni yako?

soma zaidiView attachment 3263095

Pia soma:
Meneja wa uwanja ni nani?
Hana boss wake?
Je anapaswa kuambiwa na nani kwamba kikanuni Simba alitakiwa kufanya mazoezi kwenye uwanja kabla ya mechi na muda mechi itakapochezwa?

Baada ya kukataa,hakuna aliyechukua hatua za kumtaarifu?au boss wake naye hajui mpira?

Hao makomandoo wa yanga,wana nguvu kuliko polisi?Kana watu wanaleta vurugu,kwa nini wasikamatwe na kuwekwa ndani?

Hii yanga mnaiendekeza sana,na hawa watu wa siasa wanaolazimisha club iwe ya serikali wanaonyesha upuuzi wa hali ya juu.Wana timu za majeshi lakini hawazipi upendeleo kama huu wanaoipa yanga.

Yanga ni kama vile vikundi vya mazombi kule Zanzibar wakipiga wapinzani halafu serikali nayo inachekelea tu

Sent from my Infinix X626 using JamiiForums mobile app
 
Soka la Tanzania limejikita zaidi kwenye masuala ya kutegemea 'Ndumba na Vibuyu' badala ya kutegemea Sayansi ya Kufanya Mazoezi ili kuweza kujiimarisha vizuri zaidi kwa ajili ya Soka la Ushindani.

Wahusika wanashindwa kuelewa kwamba Soka ni Sayansi, ambapo ukifuata Kanuni basi Matokeo Chanya lazima utayapata na usipofuata Kanuni Matokeo Hasi lazima utayapata.
Ni kweli mkuu. Basi angalau kututhibitishia uchawi unasaidia basi wamroge Al Ahly wawe wanabeba wao kombe la CAF.
 
Simba hawezi kukatwa pointi kwenye tatizo ambalo ametengenezewa.

Anakatwa point akiwa yeye ndio amevunja kanuni. Hawezi kuwajibika kwenye makosa yaliyofanywa na mtu mwingine.

And by records Simba wapo vizuri kwenye sheria na wanajitahidi sana kuheshimu taratibu za kimpira.

Sitaki kuamini kama wamekuwa wazembe wasione hili uliloliona wewe.
Kanuni haisemi timu ngeni ikinyimwa kufanya mazoezi iginee
Simba hawezi kukatwa pointi kwenye tatizo ambalo ametengenezewa.

Anakatwa point akiwa yeye ndio amevunja kanuni. Hawezi kuwajibika kwenye makosa yaliyofanywa na mtu mwingine.

And by records Simba wapo vizuri kwenye sheria na wanajitahidi sana kuheshimu taratibu za kimpira.

Sitaki kuamini kama wamekuwa wazembe wasione hili uliloliona wewe.
Kanuni haisemi timu ikizuiwa kufanya mazoezi igomee match husika,kanuni ipo wazi Yanga atapigwa faini ya hela au onyo Kali na aliegomea match atakatwa point 3 na magoli matatu.
 
Meneja wa uwanja ni nani?
Hana boss wake?
Je anapaswa kuambiwa na nani kwamba kikanuni Simba alitakiwa kufanya mazoezi kwenye uwanja kabla ya mechi na muda mechi itakapochezwa?

Baada ya kukataa,hakuna aliyechukua hatua za kumtaarifu?au boss wake naye hajui mpira?

Hao makomandoo wa yanga,wana nguvu kuliko polisi?Kana watu wanaleta vurugu,kwa nini wasikamatwe na kuwekwa ndani?

Hii yanga mnaiendekeza sana,na hawa watu wa siasa wanaolazimisha club iwe ya serikali wanaonyesha upuuzi wa hali ya juu.Wana timu za majeshi lakini hawazipi upendeleo kama huu wanaoipa yanga.

Yanga ni kama vile vikundi vya mazombi kule Zanzibar wakipiga wapinzani halafu serikali nayo inachekelea tu

Sent from my Infinix X626 using JamiiForums mobile app
Tulieni dawa iwaingie,hii ndio maana halisi ya Ubaya Ubwela.
 
Ni ujinga na ushamba.
Hahahaha,hili nalijua na ndio maaana siuelewagi

Mfn.. kesho pre match meeting itakuwepo ? Au imefanyika ?

Vipi marefarii ,kamisaa na timu pinzani zikafika uwanjani na Simba wasiwepo watatoa points

Wataishuisha daraja au ?

Ila NAJUA MECHI ITAHAALISHWA NAKUPANGWA SIKU NYINGINE...KESHO PRESS YA TPLB
 
Back
Top Bottom