Simba SC yatangaza haitacheza mechi dhidi ya Yanga, Wakidai vitendo visivyo vya kiungwana dhidi yao

Simba SC yatangaza haitacheza mechi dhidi ya Yanga, Wakidai vitendo visivyo vya kiungwana dhidi yao

Acha uongo simba wamefika uwanjani saa 7:00 tena yanga ndo wanatoka
Bora mkuu umesema ukweli, mashabiki wenye mihemko mkubwa na Hoya Hoya wanasema kua timu ya Simba imefika saa tatu usiku tena ikiwa na basi limejaa wazee ,, Sasa najiuliza na kipindi huku Kuna simu za kila aina walishindwa nini kudhibitisha hata Kwa video na picha kuonesha basi linaingia saa 3 usiku na picha nyingine waipige ndani ya Basi tukioneshwa hao wazee,,tena tunaambiwa kwa mihemko mkubwa kua walikua wamevaa nguo nyekundu ..kumbe basi linaondoka saa 3 wao ndio wanasema ndio muda walioingia, ujinga mzigo.
 
Katika taarifa kwa Umma waliyoitoa saa 7 na dakika 46 usiku wa 8/3/2025 klabu hiyo imesema haitoshiriki mchezo huo wa Derby uliopangwa kufanyika majira ya saa 1 usiku 8/3/2025 kutokana na kuzuiliwa kufanya mazoezi uwanja wa Benjamin Mkapa na Wanaojiita Makomandoo wa Yanga

Nini maoni yako?

soma zaidiView attachment 3263095

Pia soma:
Wengine ndio tunaingia Dar Jamani kwa ajili ya hii game!
Gharama Zetu zinarudije?
 
Ni ujinga na ushamba.
Sio kwamba nyinyi yanga na mashabiki wa aina yako ndio wajinga na washamba? Kwani nyinyi ni nani nchi hii Hadi kwanza mruhusiwe nyinyi pekee kufanya mazoezi kwenye uwanja halafu mkiondoka mzuie wengine wasifanye. Acheni mambo ya kichawi na Imani potofu za kipumbavu, kama uchawi ungekua unafanya kazi mmngechukus ubingwa wa shirikisho wakati ule mko fainali, mmewafikiria hata watu kutoka nchi mbalimbali waliotoa pesa kununua tiketi kuja kuangalia mechi kwa upumbavu mliofanya, nyinyi si mmeonekana na Mheshimiwa Awesu kua mko huko pangani mko mnazungukia waganga tena viongozi wakubwa na tai zao , Sasa mnawaogopa Simba pamoja na uchawi wenu na makafara mnayofanya..utter nonsense.
 
Kihoro kinawasumbua simba; wameogopa kichapo. Pamoja na kuwa Uwanja wa mkapa unatumiwa na Yanga pamoja na Simba kama uwanja wa nyumbani, wao siyo wamiliki wa uwanja huo. Mmiliki ni serikali ya tanzania.

Kusema walikuwa mabaunsa wa yanga, ni kisingizioa kischo na mashiko yoyote kisheria.

Woga wa kichapo unawasumbua sana Simba wakati huu..
Ujinga wa watanzania aina yako ni mtaji mkubwa sana wa chama tawala
 
Kwa wanaojua kanuni endapo Simba isipocheza huo mchezo itaadhibiwaje? Faini, kukatwa point, kushushwa daraja

Na vipi kuhusu Yanga nao?
Hapo akuna mjadala kanuni zipo wazi Simba asipotokea uwanjani ni yanga kupewa point 3 na magoli 3, Akuna kanuni inayosema ukizuiwa kufanya mazoezi ya mwisho basi ugomee kucheza mechi,,kama ni adhabu zipo kikanuni ambapo ingethibitika ivyo yanga angepewa onyo ama kupigwa faini ya milioni Moja au mbili na sio timu kugomea mechi!
 
Simba hawezi kukatwa pointi kwenye tatizo ambalo ametengenezewa.

Anakatwa point akiwa yeye ndio amevunja kanuni. Hawezi kuwajibika kwenye makosa yaliyofanywa na mtu mwingine.

And by records Simba wapo vizuri kwenye sheria na wanajitahidi sana kuheshimu taratibu za kimpira.

Sitaki kuamini kama wamekuwa wazembe wasione hili uliloliona wewe.
Usiwe mbishi nenda kasome kanuni za ligi zinasemaje kukataliwa kufanya mazoezi ya mwisho sio kigezo cha timu kugombea mechi Kuna kanuni zinaelekeza adhabu zipi zitatolewa but sio timu kugomea mechi ilo ni jambo jingine kabisa
 
Tff itakuwa ndiyo imetoa hayo maelekezo,kwa nini hao makomandoo wa yanga wanaingilia taratibu za kimichezo dhidi ya Simba,Kule mwanza mambo yalikuwa hivi hivi ili kuihujumu Simba
Kwa jinsi ambavyo Simba inauongozi makini kwenye masuala ya kisheria especially CEO Zubeda pale hakuna mtu atawatikisa Simba
 
Kwani lazima wafanye mazoezi hapo? Si wana uwanja wao Bunju? Yanga nendeni uwanjani wasipokuja chukueni Pointi 3 na magoli matatu ili iwe fundisho.
 
Mjinga kama wewe utawezaje kujadili mambo ya maana na watu wenye akili? Tunaongea mpira kati ya Yanga na Simba wewe unaongea Chama tawala. hapo ndipo ujue kuwa akili zako ni finyu sana. Inawezekana leo hujala.
Kuna watu humu wameingia kwa bahati mbaya ujue yan wana tabia flani ivi za Facebook
 
Simba hawezi kukatwa pointi kwenye tatizo ambalo ametengenezewa.

Anakatwa point akiwa yeye ndio amevunja kanuni. Hawezi kuwajibika kwenye makosa yaliyofanywa na mtu mwingine.

And by records Simba wapo vizuri kwenye sheria na wanajitahidi sana kuheshimu taratibu za kimpira.

Sitaki kuamini kama wamekuwa wazembe wasione hili uliloliona wewe.
Naunga mkono hoja hakuna kucheza na Yanga huu upuuzi ukifumbiwa macho tunatakuwa na mpira wa kihuni,wapelekeni hata FIFA hawa Yanga kule kuna rungu kali sio hawa FFF
 
Kwa wanaojua kanuni endapo Simba isipocheza huo mchezo itaadhibiwaje? Faini, kukatwa point, kushushwa daraja
Vyote kwa pamoja ila watacheza tu hizo mbwembwe za kuwatoa watu mchezo nje ya uwanja usizizingatie ni planned events
 
Back
Top Bottom