Simba Sport Club yafungiwa kusajili kisa Pape Ousmane Sakho

Simba Sport Club yafungiwa kusajili kisa Pape Ousmane Sakho

Mwaka wa tabu, zimefika goli 7 sasa, 5 kutoka Yanga, goli la Jezi + goli la Fifa, hadi muimbe Haleluya mwaka huu
 
Jaman Tim zetu mbna Kama bado hazijajipambanua kimataifa zaid kwa kutokuhexhimu Sheria za FIFA
 
Kabla ya Kukutana na Yanga tulikuwa Unbeaten na furaha ilikuwepo..!!

Baada ya Kukutana na Yanga
-Tumekula Tano
-Tumefukuza Kocha
-Tume Draw Mechi Ya Leaue
- Now Tumefungiwa Kusajiri.

Yanga Ruined our Club, I hate Yanga Africa Official..[emoji24][emoji24]

Sent from my SM-N975U using JamiiForums mobile app
Pole sana mkuu yatapita tu

Sent from my TECNO BF7 using JamiiForums mobile app
 
Klabu ya ligi Kuu ya NBC YA Simba imefungiwa kusajili mpaka itakapolipa madai ya Klabu ya Teungueth ya Senegal kuhusu mchezaji Pape Ousmane Sakho.

Uamuzi huo umefanywa na Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA) baada ya klabu hiyo kushinda kesi ya madai dhidi ya Simba kutokana na mauzo ya Sakho. Kabla ya kujiunga na Simba, Sakho ambaye hivi sasa anacheza timu ya Quevilly Reuen Metropole ya Ufaransa alikuwa mchezaji wa Simba.

Klabu hiyo ilifungua kesi FIFA dhidi ya Simba ikidai sehemu ya malipo kutokana na mauzo ya Sakho. Simba ilitakiwa iwe imetekeleza uamuzi huo ndani ya siku 45 tangu ulipotolewa, lakini haikufanyika hivyo.

Wakati FIFA imeifungia klabu hiyo kufanya uhamisho wa wachezaji kimataifa, TTF limeifungia Simba kufanya uhamisho wa ndani.

TTF inazikumbusha klabu kuheshimu sheria, kanuni na taratibu za mpira wa miguu ili kuepusha adhabu mbalimbali, ikiwemo kufungiwa usajili wachezaji

Cliford Mario Ndimbo
Ofisa Habari na Mawasiliano, TTF
Novemba 23, 2023

View attachment 2822429
Pia soma: Simba: Tuko mbioni kuilipa fedha Teungueth ya Senegal kwa ajili ya Sakho ili kujiepusha na kadhia ya kufungiwa kusajili
Hakua kingine ila tatizo ni communication barrier between Simba and Teungueth 😂
 
Ila mbona wanachama walifurahi mno ile siku mara baada ya manzoki kuingia ukumbini?
Wanachama was Simba ni tofauti na wanachama was yanga. Wanachama was yanga Wana uchungu na timu wakati wa Simba wako tayari kuuza kura zao kwa maslahi binafsi. Kama wanachama wangekuwa na uchungu Mangungu na Try again wangeshaondoka zamani.
 
Klabu kubwa Afrika, levo za Ahly, Mamelody… inakuwaje tena kudhulumu hela za usajili hadi kufungiwa?

Hivi Sawadogo alishalipwa?

Mdakuzi
B..., haya mambo ni madogo tu! Kilichotokea ni Simba kulipwa kwa awamu kwa tuliowauzia Sakho, na walitegemea awamu ya pili ya malipo ndiyo walipwe Teungueth.

Lakini, wao wamegomea hilo na wanataka angalau na wao wangelipwa nusu kwa hichohicho ambacho Simba ililipwa nusu. Kwa mambo ya AFL, hakukuwa na muda.

So watalipwa kabla ya dirisha la usajili kufunguliwa na tutasajili kama kawaida.

Ova
 
Maelezo safi kabisa, mngempa mtu smart kama wewe hivi pale idara yenu ya habari msingeshikika kwa ubora wa hicho kitengo.

Hivi ilikuwaje ukawa kolo jamani? Nikimjua aliyesababisha uwe hatutokaa tupatane, mimi kama Mwananchi na kwa maslahi yetu mapana ktk klabu tungepata hiki kichwa tungefika mbali!

Okay, huoni kama ni doa hili tayari? Haya mambo sio ya kuwekwa ktk rekodi za klabu makini, ikija kesi nyingine ya aina hii itakuwa vigumu kwenu kushinda hata kama nyinyi ndio wenye haki!
Tafakari b…
 
Ukiendesha club kubwa ya soka hayakosekani haya, ndiyo maana hata Yanga wanasumbuliwa na yule kocha wenu DJ mpaka leo, naye jambo lake liko FIFA.

Ni kawaida tu haya kwenye dunia ya soka. Hata mi naweza aliyefanya ukawa Utopolo, yaani kafanya tuwe na shida sana hata kwenye mazungumzo yetu. lol

Ova
 
Back
Top Bottom