Simba Sports Club achaneni na nia yenu ya kumfukuza kocha wetu Patrick Aussems kwani tutakuja kujuta na kulia akiondoka

huyu kocha alipewa contract ya mwaka mmoja na malengo ya kuifikisha simba nusu fainali caf hayajatimia anajua mwisho wa msimu hataongezewa mkataba, ndio maana kaanza kutafuta timu mapema, Asante Kotoko ya Ghana ilikuwa inamtaka
 
Kama yeye angekuwa na final say kwenye transfer tungesema haya ni makosa yake mwenyewe.

Lakini sasa imeuza key players watatu umekwenda kukusanya average players halafu unataka wakupe makombe?

Kama wameshindwa kufikia malengo yao wajiulize kwanza wao wametimiza vipi wajibu wao .?

Huwezi ukapata mafanikio with a squad full of veterans
 
Mwina Kaduguda anaongea EFM RADIO, 20 billions tzs zimeshaingia tiari kwene account ya simba, hapa tukifanikiwa kuuza na hisa kwa wanachama, waow, sipati picha simba ya baada ya miaka mitatu au minne huko mbele
Na nyie Mmeingiza kiasi? Au hisa ni za Mo pekee....Hisa Asilimia zenu mmenunua? Ka vipi Timu muacheni mhindi na Kocha atamleta mwingine....

Kaduguda anakula bata..hana habari na Hisa zenu.....hamna hela nyie...Mhindi kashamtia mfukoni subirini balaaa, Hati ashakabidhiwa ile ni Dewji Fc...hatari sana
 
Ausems ni bonge la kocha ila anatolewa tu kafara. Wakati wa usajili watu walitahadharisha hapa jamvini kuwa unapomuacha mchezaji kama Kotei, Okwi, Niyonzima unatakiwa ulete wachezaji wenye uwezo zaidi yao. Lakini viongozi walifanya walichojua wao matokeo yake wakaletwa wabrazili ambao uwezo wao ni wa kawaida sana halafu kufungwa na UD Songo, Mwadui na sare ya Prison zigo anaangushiwa Ausems.

Mo bila kuunda timu ya scounting ataendelewa kulishwa matango pori na watu wanomzunguka. Timu ya scounting inahitaji watu wanne au watano tu kutafuta vipaji ndani ya Tanzania na nje ya Tanzania kwisha. Itaokoa gharama sana na dirisha la usajili likifunguliwa tayari unakuwa na wachezaji mkononi unawasainisha tu kutokana na mahitaji ya timu tena kwa gharama ndogo. Leo Simba na Yanga zinamgombania Bakari Nondo wa Coastal wakati kacheza ligi msimu uliopita. Kama kungekuwa na timu ya scounting kipaji chake kingeonekana mapema badala ya kusubiri kumuona kwenye timu ya taifa. Leo mshahara wa Wawa ukimpa nusu yake Nondo atakupa huduma iliyotukuka au nusu ya mshahara wa Deo Kanda ukampa Miraji Athumani nina hakika atafunga magoli mpaka kwa 'ugoko"

Uongozi na bodi nzima ya Simba ijitathimini yenyewe kwanza na kurekebisha usajili kwenye dirisha dogo badala ya kukimbilia kumtimua Ausems. Kwa Simba ya msimu uliopita ilihitaji tu nyongeza ya wachezaji wasiozidi wanne tu ingekuwa moto. Ilihitajika tu kipa, beki wa kati, kiungo mkabaji (mkata umeme wa ukweli) na mshambuliaji mwenye uwezo kama wa Kagere basi. Na viongozi walipaswa wajue kuwa falsafa ya Ausems ni kushambulia mwanzo mwisho kwa hiyo walihitajika walete watu wa kazi kweli kweli kuanzia mbele lakini badala yake wakaleta wachezaji wanaowajua wao halafu leo wanajitia kumtimua Ausems.

Kwangu mimi Ausems atabaki kuwa bonge la kocha kwani ukilinganisha matokeo anayoyapata mpaka sasa na kikosi kilichosajiliwa anajitahidi sana inabidi apongezwe sio kutimuliwa.
 
Ni kocha mzuri sijaona mapungufu,na pia naamini ule usajili wa wabrazil sio yeye ni pressure kutoka kwa wengine,na usajili wa hao majamaa ndo ulitokucost club bingwa ,wametema kina kotei na okwi halafu wapya waliokuja hadi wazoeane na wengine inachukua mda
Nasubiri iwe ' Confirmed ' na Uongozi wa Simba SC ili niachane rasmi Kushabikia Soka la Bongo. Namkubali Aussems kwa 100%.
 
Nimesikia kocha wenu patrick eti alienda kufanya mazungumzo na totenham hotspurs?
 
Natamani Mungu aihadhibu Simba kwa kutokuwa na shukrani kwa Kocha aliyewapa mafanikio.
 
Nimeelewa kwanini Mkwabi alijiondoa kaduguda ni mpayukaji niliishangaa Simba kumwacha okwi kisa anataka pesa nyingo halafu unaenda kusajili ajibu hata haruna shamte walimsajili dkk za mwisho wakati ilijulikana muda mrefu kapombe akiumia hatuna mbadala bocco Ana tatizo la kuumia Mara kwa Mara tulipaswa ama tuongeze fowadi wa nguvu asaidie timu huyu mo ndio anataka kushindana na tp mazembe wakati anashindwa kuzuia wachezaji Bora wasiondoke
 
Mwina Kaduguda anaongea EFM RADIO, 20 billions tzs zimeshaingia tiari kwene account ya simba, hapa tukifanikiwa kuuza na hisa kwa wanachama, waow, sipati picha simba ya baada ya miaka mitatu au minne huko mbele
Ah....Kaduguda sio wa kumuamini ndugu pale alikuwa Swedi wameona pasua kichwa ndio akaletwa huyu kimkakati!
 
Umeshauri vizuri sana mkuu, ila mpaka leo mimi sijaekewa sababu ya msingi ya Simba kuwaacha Okwi na Kotei wakati wakijua mbee yao wanakabiliwa na mashindano ya klabu bingwa, uswahili, uswahili unaharibu sana mpira wetu.
 
Bila shaka wewe mtoa mada utakuwa na 10% kutoka kwa Mwalimu kama hao viongozi uliosema yawezekana wanataka hyo %. Sisi wanasimba kindakindaki tumechoka na uswahili Wa uongozi mzima pamoja na huyo beberu wako.
Na kuna wachezaji wengine pale uzee umeshaanza kuwataabisha, na miongoni mwao ni Kagere, Bocco, Wawa na Kapombe. Kwa nini tusifate nyayo za watani wetu Young Africans Sports Club "The Citizen Team" ambao kwa sasa wameanza kujiongoza kisasa zaidi!?
 
Bongo kocha anapewa mkataba wa miaka miwili ashinde ligi na afike makundi ligi ya mabingwa
 
He makubwa ...Yanga hi ya Jangwani au unamaanisha kitu kingine!
 
Kiufupi viongozi waliosajiri wachezaji wa style mmoja ni wapumbavu kweli wachezaji hawachezi direct football wanazunguka na mpira nyuzi 360 ,Ajib,chama,kahata,shiboub wote wanamchezo unafanana tu ,wabrazil ni bure kabisa ,ninaimisi simba ya mwaka Jana ilihitaji beki tu na replacement ya boko kufika fainali au nusu club bingwa Africa ,simba ya Leo bila miraji Athuman inayumba ,kweli simba tumefika huku?wao wamtimue kocha sisi hatutakwenda uwanjani wapumbavu sana
 
Kosa la Brazillians ni lipi elezea kimpira
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…