tumeenda uwanjani watu akisema leo bao nyingi sikuelewa,>
Baada ya game kuisha nikasikia watu wanasema tulisema leo nyingi!!!!!!!!!!
Sasa sielewi kulikuwa na nnini hasa na maneno hayo!!!!!!!!!!!!!!111
Je tutafika huko twendako.??????????????
 
tumeenda uwanjani watu akisema leo bao nyingi sikuelewa,>
Baada ya game kuisha nikasikia watu wanasema tulisema leo nyingi!!!!!!!!!!
Sasa sielewi kulikuwa na nnini hasa na maneno hayo!!!!!!!!!!!!!!111
Je tutafika huko twendako.??????????????
inshalaah tutafika
 
[TABLE="class: contentpaneopen"]
[TR]
[TD="class: contentheading, width: 100%"]Hili la Simba lisiwe la kufurahisha wanachama tu [/TD]
[TD="class: buttonheading, width: 100%, align: right"] Send to a friend [/TD]
[/TR]
[/TABLE]
[TABLE="class: contentpaneopen"]
[TR]
[TD="class: createdate"] Saturday, 22 October 2011 09:49 [/TD]
[/TR]
[TR]
[TD] 0digg

Mwenyekiti wa Klabu ya Simba, Ismail Aden Rage

WIKI iliyopita, Mwenyekiti wa Klabu ya Simba, Ismail Aden Rage alikutana na waandishi wa habari na kueleza mikakati ya klabu hiyo hasa katika kuwekeza katika klabu hiyo.

Licha ya siku kadhaa kupita tangu kutolewa kwa mikakati hii, bado hatuoni kama tumepitwa na wakati kulizungumza jambo hili japo kwa ufupi kwa tija ya klabu na wanachama wake kwa ujumla.

Rage alisema wako katika mazungumzo na benki mbili nchini kwa ajili ya kuweka mtaji wa uwekezaji wa pamoja jengo la kisasa la Makao Makuu ya klabu hiyo iliyoko Mitaa ya Msimbazi na Mchikichi.

Hatua hii haiwezi kupita bila kupongezwa pamoja na kwamba imechukua muda mrefu kufikiwa.Tunasema imchukua muda mrefu kwa sababu, klabu hiyo tangu ianzeshwe mwaka 1936, sasa ina miaka 75.

Si nia yetu, na wala hatuna sababu ya kuwakatisha tamaa Simba, tukiamini katika safari ya kusaka maendeleo, suala la kukata tamaa linapaswa kuwa la mwisho kufikiriwa.

Hata hivyo, hoja yetu ya msingi ni kuitaka klabu ya Simba kusimama juu ya mstari wa kauli ilizotoa katika kuleta maendeleo. Isiwe ni mikakati ya kujifurahisha na kuwapamba wanachama wake.

Ukweli usiopingika kuwa ujenzi wa jengo la kisasa utasaidia kuinua pato la klabu, kuwapa wachezaji mahala pazuri pa kulala na hata kuendesha shughuli mbalimbali za biashara ambazo zote zitakuwa tija kwa klabu.

Ikiwa kutakuwa na ukumbi wa mikutano wa kisasa, ukumbi wa shughuli za harusi, hoteli, maofisi na hata ukumbi wa disko, kitakuwa kitega uchumi kizuri kwa klabu kuingiza mapato yake.

Vilevile maduka mbalimbali, supermarket na pia duka la kuuza bidhaa zenye nembo ya Simba, vyote hivyo vikiingia klabuni vitaboresha pato la klabu.

Mafanikio huja kutokana na kupanga mikakati na kuitekeleza, kinyume chake hakuna linaloweza kufanikiwa.

Katika hili, ni vyema maamuzi yakafikiwa katika hali ya uwazi hasa kwenye masuala ya pesa ambayo siku zote huwa kiini cha migogoro kwenye klabu.

Kama ni kampuni, kama ni klabu ziwekwe taratibu zake kisheria ili kutengeneza mazingira ya kuondokana na migogoro.Uwepo wa utaratibu wenye tija utasaidia kusimamia shughuli za kuendesha klabu.

Utaratibu huu kamwe hautakuwa na sababu ya kuangalia nani vinara wa vurugu, nani wanaongea sana, kinachotakiwa ni kupatikana watu wenye taaluma kwa kila eneo kuendesha shughuli za klabu.

Tunawapongeza Azam kwa kuona mbali. Simba na Yanga zina miaka zaidi ya 70 hazina vitu kama ilivyofanya Azam ambayo iko katika Ligi Kuu si zaidi ya miaka mitano.

Msingi wa Azam ulikuwa uwe wa kuiga kutoka Simba au Yanga lakini kwa vipindi virefu klabu zimetawaliwa na migogoro isiyokuwa na tamati na matokeo yake ni kushindwa kujipanga.

Tunaamini mikakati iliyopo Simba ikiwemo ya ujenzi wa uwanja wa kisasa maeneo ya Bunju, nje kidogo ya Dar es Salaam, vitasaidia kuiweka Simba katika nafasi maridhawa na kuonekana kuwa ni klabu.

Tunaona klabu kama ya Asec Mimosa ya Ivory Coast, ina kila kitu kinachostahiki kwa wanasoka kuanzia miaka 14 hadi timu za wakubwa. Timu hii imewekeza kikamilifu katika soka na ndivyo inavyotakiwa kwa Simba.

Hatutarajii kuona haya yanakuwa blabla ama kubakia kwenye makabrasha, kinachotakiwa ni kuanza utekelezaji mapema baada ya kukamilika kwa mazungumzo na wahusika ambao ni mabenki. [/TD]
[/TR]
[/TABLE]
 
Kuipenda Taifa Kubwa Simba Sports Club ni Raha duniani na ukisoma hii Comment ujue unaipenda Simba kwa Raha zote. naongea na wewe unayesoma hapa Simba oye.
 
Kuipenda Taifa Kubwa Simba Sports Club ni Raha duniani na ukisoma hii Comment ujue unaipenda Simba kwa Raha zote. naongea na wewe unayesoma hapa Simba oye.

Mbona kimya leo jamani? leo haulipendi taifa kubwa?
 
Simba walijiamini sana kabla ya mechi,kama kawaida soka la bongo eti Okwi kauza mechi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…