KOCHA Mkuu wa Simba, Milovan Cirkovic amesema hakuridhishwa na kiwango cha timu yake na hasa katika safu ya ulinzi.

Kutokana na hilo, kocha huyo amesema atalazimika kufanyia marekebisho safu hiyo kabla ya kuanza kwa mzunguko wa pili wa Ligi Kuu Bara.

Simba ilicheza mechi ya kimataifa ya kirafiki dhidi ya Tusker ya Kenya juzi na kutoka sare ya bao 1-1.

Akizungumza baada ya mechi hiyo, kocha Cirkovic alisema, timu yake ilicheza kiwango cha chini tofauti na ilivyocheza kwenye michuano ya Kombe la Mapinduzi Zanzibar.

“Lakini leo (juzi) beki nzima, hasa Juma Nyoso alicheza chini ya kiwango”. Akizungumzia maandalizi ya mechi ya Kombe la Shirikisho, kocha huyo alisema, bado ana muda wa kutosha kuiandaa timu.

Simba inatarajiwa kuanza michuano ya Kombe la Shirikisho ugenini Kigali, Rwanda ambapo itamenyana na Kiyovu ya huko Februari 18.

Naye kocha wa Tusker, Sammy Omollo alisema waliwazidi Simba katika mechi ya juzi hasa kwenye kiungo.

“Kama washambuliaji wangu wangekuwa makini wangeweza kushinda mechi”.
 
kila la kheli kwa maandalizi ya kombe la shirikisho..
 
Full time: Simba 2-1 Coastal; Hongera mnyama na washabiki wote wa mnyama.
 
wanamsimbazi mbona hakuna update za kuhusu uwanja au ndio changa la macho tusubiri uchaguzi ndio watu waamke?
 
wanamsimbazi mbona hakuna update za kuhusu uwanja au ndio changa la macho tusubiri uchaguzi ndio watu waamke?
Mkuu uwanja kabisa?!, Ngoja tusubiri maana hata tunaoshabikia simba hatuoni la maana, nina mpango wa kuacha kwenda uwanjani kwenye mechi za simba na yanga mpaka pale viongozi watakapokuwa serious.
 
Mkuu uwanja kabisa?!, Ngoja tusubiri maana hata tunaoshabikia simba hatuoni la maana, nina mpango wa kuacha kwenda uwanjani kwenye mechi za simba na yanga mpaka pale viongozi watakapokuwa serious.
Nitakuunga mkono kaka,kuna mtu anatutukana sana kuhusu suala hili hadi maumivu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…