[h=3]Milovan atema watano Simba[/h] Posted by GLOBAL on May 28, 2012 at 9:56am 0 Comments 0 Likes

Milovan Cirkovic.
Na Khatimu Naheka
KOCHA wa Simba, Milovan Cirkovic, amekamilisha ripoti yake ambapo amesema nyota watano wapo katika upepo mbaya wa kutupiwa virago.

Kocha huyo aliyempoka nafasi Mganda Moses Basena katikati ya msimu uliopita, tangu aichukue timu hiyo amekuwa na mafanikio makubwa lakini zaidi amefanikiwa kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu ya Bara licha ya ushindani mkali kutoka kwa Azam na Yanga.

Akizungumza na Championi Jumatatu muda mfupi kabla ya kukwea pipa kuelekea kwao kwa ajili ya mapumziko mafupi, Milovan alisema ameshakamilisha ripoti na tayari ameshaikabidhi kwa mabosi wake lakini ameona kuna haja ya kupunguza nyota wanne mpaka watano.

Alisema sifa kubwa za wachezaji watakaoachwa ni wale walioshuka viwango vyao na walioshindwa kuleta upinzani wa namba katika kikosi…

Milovan Cirkovic.
Na Khatimu Naheka
KOCHA wa Simba, Milovan Cirkovic, amekamilisha ripoti yake ambapo amesema nyota watano wapo katika upepo mbaya wa kutupiwa virago.
Kocha huyo aliyempoka nafasi Mganda Moses Basena katikati ya msimu uliopita, tangu aichukue timu hiyo amekuwa na mafanikio makubwa lakini zaidi amefanikiwa kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu ya Bara licha ya ushindani mkali kutoka kwa Azam na Yanga.
Akizungumza na Championi Jumatatu muda mfupi kabla ya kukwea pipa kuelekea kwao kwa ajili ya mapumziko mafupi, Milovan alisema ameshakamilisha ripoti na tayari ameshaikabidhi kwa mabosi wake lakini ameona kuna haja ya kupunguza nyota wanne mpaka watano.
Alisema sifa kubwa za wachezaji watakaoachwa ni wale walioshuka viwango vyao na walioshindwa kuleta upinzani wa namba katika kikosi msimu uliopita.
Aidha, Milovan amependekeza aongezewe wachezaji wasiopungua wanne katika nafasi za ushambuliaji, kiungo na beki, lengo likiwa ni kuiwezesha klabu hiyo kufanya vizuri katika michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika msimu ujao.
"Tayari nimeshakamilisha ripoti yangu kuhusu timu na nimeshawakabidhi viongozi lakini kila kitu kuhusu masuala ya usajili nimeshazungumza na viongozi na nimeshawakabidhi kile kinachohitajika katika kipindi hiki.
"Lakini hilo la nani ataachwa siwezi kukwambia kwa sasa, isipokuwa nadhani wachezaji wanne mpaka watano wanaweza wasiwe nasi msimu ujao," alisema Milovan.
"Hatutapunguza tu, nimewaambia pia nahitaji kuongezewa wachezaji wanne, hasa katika maeneo ya ushambuliaji, kiungo na ulinzi," aliongeza Milovan ambaye anatarajia kurejea nchini baada ya wiki mbili.
 
WAnyama wana Tabia mbaya kumbe zile 5 zimefanya watu hawakulala, wanaanza ku sign kwa bila mpangilio kule sasa wanaleta Maximo nasikia 5 si mchezo bwana na bado safarihii tutapowapiga zengine watauza kiwanja jangwani pale japo nasikia wanakiuza ila mnunuaji hakuna nani anataka kuishi kwenye bwawa la mafuriko?
 


Baada ya Yanga kumchukua Kevin Yondani, Simba tumeamua kumchukua aliyekuwa beki na nahodha Shadrack Nsajigwa (Pichani Kulia). Tetesi zinasema Nsajigwa atatangazwa muda wowote kuwa mchezaji wa Simba
 


Baada ya Yanga kumchukua Kevin Yondani, Simba tumeamua kumchukua aliyekuwa beki na nahodha Shadrack Nsajigwa (Pichani Kulia). Tetesi zinasema Nsajigwa atatangazwa muda wowote kuwa mchezaji wa Simba

kwa hapa simba tutakuwa tumepata garasa kashaisha huyu jamaa
 
Thank you! The Woz's will be there, all branches


June 29 to September 5th!


DH & I have only had a few days there in previous times, diving & driving were our primary actions. Our latest DGS, who is due any day now, will be presented to his Woz relatives on this journey. This will be one more unique household time using out DVC!




my favolus play games free onlineare you like at-igame2play.com


i love play games online for freeat- igamesflix.com
 

???????????
 
[h=3]KAPOMBE AFURAHIA TUZO, LAKINI...[/h]
[TABLE="align: center"]
[TR]
[TD] [/TD]
[/TR]
[TR]
[TD]Kapombe kushoto, akipokea tuzo ya Mwanamichezo Bora, kutoka kwa Salim Amir mchezaji wa zamani wa kimataifa wa Tanzania. Anayeshuhudia katikati ni Makamu Mwenyekiti wa Simba SC, Geoffrey Nyange 'Kaburu'. [/TD]
[/TR]
[/TABLE]

KIUNGO chipukizi wa Simba SC, Shomary Kapombe amesema kwamba mafanikio anayoyapata hivi sasa ni changamoto nzuri kwake na hatalewa sifa, badala yake ataongeza juhudi ili afike mbali kisoka.
Akizungumza na BIN ZUBEIRY usiku wa jana katika ukumbi wa Diamond Jubilee, Dar es Salaam, Kapombe alisema kwamba amefurahi mno kutwaa tuzo mbili, Mwanamichezo Bora Anayechipukia na Mwanamichezo Bora wa Jumla wa mwaka Chama cha Waandishi wa Habari za Michezo Tanzania (TASWA), lakini hatalewa sifa.
"Nimefurahi kwa kweli, ila kwangu hii ni kama changamoto na ninawaahidi Watanzania kwamba sitalewa sifa na nitajitahidi nifike mbali,"alisema Kapombe.
Kiungo huyo anayeweza kucheza kama beki wa kati na kulia pia, alisema kwamba ndoto zake kwa sasa ni akitoka Simba akacheze Ulaya na kulingana na mafanikio yake ya sasa akiwa bado mdogo Kapombe alisema anaamini atatimiza ndoto zake.
"Naamini nitafika mbali, kwa sababu siri ya mafanikio ya mchezaji ni bidii ya mazoezi na kusikiliza mafundisho ya walimu wake, nami nitazingatia hilo,"alisema mfungaji huyo wa bao la kusawazisha katika ushindi wa 2-1 wa Tanzania dhidi ya Gambia Jumapili, ikitoka nyuma kwa 1-0 katika mechi ya kuwania tiketi ya kucheza Kombe la Dunia 2014.
Kapombe amemaliza msimu mmoja tu Simba SC tangu asajiliwe kutoka Polisi ya Morogoro, lakini kwa sasa tayari ni tegemeo la klabu yake na timu ya taifa. Kijana anacheza kwa bidii na ana kipaji, kiasi kwamba hata kocha wa timu ya taifa, Taifa Stars, Kim Poulsen anamtabiria kufika mbali.
"Kapombe ni kati ya wachezaji wangu ambao nina matumaini watafika mbali, namtakia kila heri na nampongeza kwa mafanikio yake,"alisema Poulsen alipozungumza na BIN ZUBEIRY usiku wa jana.
Pamoja na kukesha Diamond Jubilee usiku wa jana, lakini Kapombe ameondoka na kikosi cha Taifa Stars alfajiri ya leo kwenda Msumbiji kwa ajili ya mchezo wa marudiano wa kuwania tiketi ya kucheza Fainali za Mataifa ya Afrika mwakani Afrika Kusini dhidi ya wenyeji Jumapili, Tanzania ikitakiwa kushinda au sare ya mabao yasiyopungua 2-2 ili isonge mbele, kufuatia awali kulazimishwa sare ya 1-1.
 
[h=2]Okwi atua Orlando Pirates[/h]




Emmanuel Okwi


Klabu ya Orlando Pirates ya Afrika Kusini juzi imetuma rasmi barua kwa uongozi wa Simba ikimtaka mshambuliaji wake, Emmanuel Okwi, aende kufanya majaribio katika timu hiyo ya Ligi Kuu ya Afrika Kusini.

Akizungumza na gazeti hili jana, Makamu Mwenyekiti wa Simba, Geofrey Nyange 'Kaburu' alisema kuwa wamepokea barua hiyo na watamruhusu Okwi aende kufanya majaribio kwenye timu hiyo.

Kaburu alisema kuwa Okwi atajiandaa na safari hiyo muda mfupi baada ya kurejea nchini akitokea kwao Uganda aliko sasa kwenye kikosi cha timu ya taifa ya Uganda (Cranes).

Alisema kuwa klabu ya Orlando Pirates itamfanyia majaribio kwa muda wa wiki mbili na tayari imeshatuma barua ya kumuombea viza ya kuingia Afrika Kusini kwa sababu Okwi ni raia wa Uganda na hivyo anahitaji kupata viza.
"Kwa sasa Simba tunafanya usajili wetu kimya kimya, ila pia tuko mbioni kumuuza Okwi mipango ikienda sawasawa," alisema Kaburu.

Kiwango cha Okwi aliyezaliwa Desemba 25 mwaka 1992, kimeonekana kupanda zaidi kuanzia mwaka jana na tayari amekuwa akianza kwenye kikosi cha kwanza cha Cranes katika mechi za timu hiyo za hivi karibuni tofauti na ilivyokuwa huko nyuma.

Kaburu alisema vilevile kuwa Simba itaingia kambini mwishoni mwa mwezi huu
 
MAKAMU Mwenyekiti wa mabingwa wa Tanzania Simba SC Geoffrey Nyange ‘Kaburu' amesema club hiyo imekamilisha usajili wao kwa kukinasa kifaa kimoja kikali ambacho Yanga walikuwa wanakiwania.
Ingawa Kaburu hakutaka kutaja jina la mchezaji huyo, lakini uchunguzi wa BIN ZUBEIRY umebaini kwamba, mchezaji mwenyewe ni mshambuliaji wa Dong Tam Long An ya Vietnam, Danny Davis Mrwanda ambaye kweli Yanga walikuwa wanamtaka wakashindwana.
BIN ZUBEIRY inajua Mrwanda aliyewahi kuchezea Simba kabla ya kwenda ughaibuni, atasaini Simba SC wakati wowote kwa sababu mazungumzo baina ya pande hizo mbili yanaendelea vizuri.
Mkataba ambao atasaini Mrwanda ni ambao utamruhusu kuondoka wakati wowote atakapopata timu nje ya Tanzania.
Pamoja na ishu ya Mrwanda, Kaburu alisema kwamba mchezaji anayefunga usajili wa Simba ni beki wa kati wa kigeni, ambaye bado wanafuatilia uwezo wake ili kujiridhisha.

Lakini Kaburu amesema mahitaji yote ya Simba yametimia, kwa kusajili winga Kiggi Makassy, washambuliaji Abdallah Juma, Mrwanda, viungo Ibrahim Jeba, Patrick
Mbivayanga, Salim Kinje, Mussa Mudde, beki wa kushoto, Paul Ngalema na kupandisha wachezaji watatu wa U-20.
Aidha, Kaburu alisema ili kuboresha zaidi kikosi, wanafikiria kusajili beki wa kulia kwa sababu Nassor Masoud ‘Chollo' ni majeruhi wa muda mrefu na kuna uwezekano bahati ikamuangukia beki wa timu hiyo aliyekuwa akicheza kwa mkopo Villa Squad, Haruna Shamte.
Kwenye sentensi nyingine ni kwamba Kiggi Makassy ameripoti rasmi kazini, kwa mwajiri wake mpya Simba SC na kuanza mazoezi leo asubuhi. "Kiggi ameanza mazoezi rasmi leo,"alisema Kaburu kuhusu kiungo huyo waliyemuiba kwa watani wao wa jadi, Yanga SC.
 


Kikosi kilichoifyatua toto hapo jana, kutoka kushoto ni Abdallah Juma, Amri Kiemba, Haruna Shamte, Salim Kinje, Hassan Kondo, Haroon Othman, Paul Ngalema, Abdallah Seseme, Uhuru Selemani na Obadia Mungusa, na aliye mbele ni golikipa Hamadi Waziri.

Huku Majembe mengine yakiwa kwenye benchi kama yanavyoonekana hapo chini.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…