[h=3]
Milovan atema watano Simba[/h] Posted by
GLOBAL on May 28, 2012 at 9:56am
0 Comments 0 Likes
Milovan Cirkovic.
Na Khatimu Naheka
KOCHA wa Simba, Milovan Cirkovic, amekamilisha ripoti yake ambapo amesema nyota watano wapo katika upepo mbaya wa kutupiwa virago.
Kocha huyo aliyempoka nafasi Mganda Moses Basena katikati ya msimu uliopita, tangu aichukue timu hiyo amekuwa na mafanikio makubwa lakini zaidi amefanikiwa kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu ya Bara licha ya ushindani mkali kutoka kwa Azam na Yanga.
Akizungumza na Championi Jumatatu muda mfupi kabla ya kukwea pipa kuelekea kwao kwa ajili ya mapumziko mafupi, Milovan alisema ameshakamilisha ripoti na tayari ameshaikabidhi kwa mabosi wake lakini ameona kuna haja ya kupunguza nyota wanne mpaka watano.
Alisema sifa kubwa za wachezaji watakaoachwa ni wale walioshuka viwango vyao na walioshindwa kuleta upinzani wa namba katika kikosi…
Milovan Cirkovic.
Na Khatimu Naheka
KOCHA wa Simba, Milovan Cirkovic, amekamilisha ripoti yake ambapo amesema nyota watano wapo katika upepo mbaya wa kutupiwa virago.
Kocha huyo aliyempoka nafasi Mganda Moses Basena katikati ya msimu uliopita, tangu aichukue timu hiyo amekuwa na mafanikio makubwa lakini zaidi amefanikiwa kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu ya Bara licha ya ushindani mkali kutoka kwa Azam na Yanga.
Akizungumza na Championi Jumatatu muda mfupi kabla ya kukwea pipa kuelekea kwao kwa ajili ya mapumziko mafupi, Milovan alisema ameshakamilisha ripoti na tayari ameshaikabidhi kwa mabosi wake lakini ameona kuna haja ya kupunguza nyota wanne mpaka watano.
Alisema sifa kubwa za wachezaji watakaoachwa ni wale walioshuka viwango vyao na walioshindwa kuleta upinzani wa namba katika kikosi msimu uliopita.
Aidha, Milovan amependekeza aongezewe wachezaji wasiopungua wanne katika nafasi za ushambuliaji, kiungo na beki, lengo likiwa ni kuiwezesha klabu hiyo kufanya vizuri katika michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika msimu ujao.
"Tayari nimeshakamilisha ripoti yangu kuhusu timu na nimeshawakabidhi viongozi lakini kila kitu kuhusu masuala ya usajili nimeshazungumza na viongozi na nimeshawakabidhi kile kinachohitajika katika kipindi hiki.
"Lakini hilo la nani ataachwa siwezi kukwambia kwa sasa, isipokuwa nadhani wachezaji wanne mpaka watano wanaweza wasiwe nasi msimu ujao," alisema Milovan.
"Hatutapunguza tu, nimewaambia pia nahitaji kuongezewa wachezaji wanne, hasa katika maeneo ya ushambuliaji, kiungo na ulinzi," aliongeza Milovan ambaye anatarajia kurejea nchini baada ya wiki mbili.