yanga ndo timu pekee iliyowahi kuuza mchezaji
nje ya nchi na kung'aa katika vilabu mbali mbali
barani ulaya, mchezaji huyu alijulikana kama Nonda Shaaban al maarufu kama "papii". nonda ambaye aliwahi kutamba na mashujaa
hawa wa jangwani amepata kuchezea vilabu
kama val profesional ya south africa, FC zuurich
ya uswis, stade rennes na AS monaco zote za
ufaransa, AS roma ya italia akicheza pamoja na
francesco totti, blackburn ya uingereza na sasa anakipiga katika klabu ya galatasaray yenye
maskani yake katika uwanja wa ali sami yen
nchini uturuki.