Inawezekana Senzo alikua ni mzri sana kwenye Management, Lakini kwa alilolifanya wakati anaondoka Simba ameonesha kua siasa za mpira wa Bongo zimeshamtafuna tayari. Ukiwa Professional uwezi ukaacha kazi kienyeji kiasi hicho.
Yule ana kibari cha kufanya kazi kwenye Kampuni ya Simba hivyo hawezi kufanya kazi Yanga bila kuwasiliana na Simba ili abadilishe kibali cha kazi.
Kwenye sheria za kazi uwezi kuacha kazi bila kuandika barua kwanza ya kuacha kazi kwa mwajiri wako.
Kwa jinsi alivyoonesha kutokua professional kwenye hili, Kwenda Yanga itakua ni hatua ya safari yake ya kwenda kwao sio kwa heshima ila kwa fedheha.